Ni wangapi wanakumbuka jina la mwalimu wa darasa la kwanza?

mwalimu Zongo huyu alitufundisha kuanzia kuimba na kuongea kwa kuimba ule wimbo maarufu wa mdundiko waaa pugu manzese kaliakoo! haikuwa kazi rahisi kuitamka hiyo.
akaja mwanaume alikuwa anaitwa Kabogoyo huyu sikumpenda bakora zilikuwa nyingi mno tena za mgongoni alipohamishwa nikashukuru! sintamshahau aliniandikia sifuri sijui kusoma kisa nilichelewa kuanza kusoma kwa hofu niliyokuwa nayo juu yake lakini masomo mengine nikafauru sasa sielewi ilikuwaje niwe na sifuri kusoma niweze hesabu na mwandiko?
nakumbuka hata nikitumwa pombe kilabuni na babu nikimwona huyu namwogopa inabidi nizunguke asinione kuingia na kidumu changu acha kabisa!
 
Kiukweli maisha yangu yote ya elimu kuanzia nursery hadi uni sikumbuki jina la mwalimu yeyote zaidi ya fala mmoja alikua discipline master nikiwa form two anaitwa Gibson, yule ms@nge nammind mpaka leo!

Sent using Jamii Forums mobile app
teh..teh...te..hh.....alikunyooooosha! sijui tumuite aje hapa naona unatusumbua
 
najaribu kutafuta niliosoma nao siwaoni kweli kusoma bush ni tabu kidogo ukiondoka umewaacha wengi sana na miaka ya 80 kurudi chini waliokuwa wanaenda sekondari ni 5% na ukitoka kijijini haurudi tena kwa nafasi unajifanya wa mjini.
uzi mzuri sana hongera
 
Mwl. Makwasa alinifundisha na kunifanya niipende shule, ila sasa kuna huyu alikuwa anafundisha darasa la mkondo B, Mwl. Kayungi (Mlokole pia ni muhaya) Sikuwahi kumpenda wala kuja kumpenda ukisikia mwalimu kwa sababu ya matatizo ya familia ni huyu, alikuwa mkali, katili, asiyekuwa na upendo anachapa watoto kama anachapa watu wazim. (1996 Shule ya msingi Mazoezi Bunda)
 
mpaka sasa sijampata hata niliyesoma naye inamaana wote wapo kilabu cha pombe hawakuweza kufika mjini? kama ni hivi basi kazi bado ipo tujipange kuwachomoa wenzetu hali si hali! haiwezekani darsa la watu 88 kwa wakati ule hakuna hata mmoja jamii forum hata kama tulifauru wachache lakini du! tuwe na adabu tukiwa mjini sio tunabinuabinua makalio wakati mjini hatuna ndugu.
 
Duuu! jamani wanafunzi wenzangu niliosoma nao Kijijini wajameni kuree Kibumaye shule ya Msingi S.L.P 172 TARIME-MARA
MKO wapi? hamuwataji waalimu wetu? hamumo humu kweli? ngoja nitafute zaidi ndo ntajua aliyeendelea!

SHADRACK GIMAKWI- daa alikuwa mkorofi. hasa kuwahi number. usafi! hee!
LUCY BONGE.
MRS BENIGNA na BINTI YAKE PILI MACHEMBA uko wapi?
WEREMA.
GHIKARO ALEXANDER
BABU SAMSON POA NA BINTI YAKEE NDEGE SAMSONI
Hawa ni chekechea mpaka la kwanza. But nilikuwa sijui kusoma tu, kuandika mashalah!.
 
Kwa utafiti wangu wa haraka nimegundua kwamba elimu yetu watanzania imeanza kuharibika miaka ya 90..hivi unaandikaje jina la mwalimu au shule kwa kuanza na herufi ndogo?
Hivi vitu vidogo ndo ulikuwa msingi wa mwanzo katika elimu ya mwanafunzi.
Mkuu kwa kauli yako hii naona wameanza kujirekebisha, unaona anyekufuatia hapo chini huko nyuma aliandika utumboutmbo. baada yako kusema amejirekebisha.
Bora sisi wakongwe eti?
 
najaribu kutafuta niliosoma nao siwaoni kweli kusoma bush ni tabu kidogo ukiondoka umewaacha wengi sana na miaka ya 80 kurudi chini waliokuwa wanaenda sekondari ni 5% na ukitoka kijijini haurudi tena kwa nafasi unajifanya wa mjini.
uzi mzuri sana hongera
Kweli mkuu umenigusa hadi kwa mfupa. hata mimi siwaoni humu wajanja walokuwa untouchable wa darasa na km ulikuwepo kijiji kile sijawahi kanyaga. kwa hiyo ulisoma JUMA NA ROZA MKUU? haya maandishi makweta aliyapinga eb angalia,

WIZARA YA ELIMU YA TAIFA.
SHULE YA MSINGI KIBUMAYE.

S.L.P 172
TARIME-MARA
 
Back
Top Bottom