Ni wakati wa watumiaji wa injini za boti ndogo kugeukia injini za kichina

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,945
12,508
Ni wakati sahihi kwa watumiaji wa injini za boti kwa ajili ya uvuvi, utalii na matumizi binafsi kugeukia injini za kutoka China baada ya miaka mingi kutumia injini zenye brand kubwa kama Yamaha, Suzuki, Mercury, Honda, Envirude, Tohatsu na Torpedo.

China sasa wamekuwa wakitengeneza injini za boti kama Parsun na Calon Grolia.

Sasa kwenye uvuvi kumiliki injini ya boti imekuwa ni jambo kubwa na gharama za ununuaji zipo juu. Tukigeukia injini za China bei ni ya kawaida na zina utumiaji mzuri wa mafuta. Spea zake zipo na bei si ghali sana.

images.jpeg

images (1).jpeg
 
Hayatozimikia majini? Au kuwaka moto?
Mkuu ondoa shaka kuhusu kuzima au kuwaka moto, injini za boti zinashabihiana sana na injini za pikipiki.

Mfano injini ya boti yenye nguvu ya 15HP kama haiwashi kwa betri(electric starter) hii itatumia njia ya kiki na hii hazina mambo ya umeme sana zaidi ya moto wa spark plug.

Hapo hofu ya kuwaka moto hakuna, hizi injini zinapozwa na mfumo wa maji(water cooled) sio wa hewa (air cooled) ambao tungeofia chombo kikifanya kazi nzito mfululizo kuweza kuwaka moto.
 
Kitendo cha kutenganisha majini na nchi kavu (sumatra) hawakukutendea haki kabisa..
Mkuu kutenganisha nchi kavu na majini ilikuwa ni jambo la muhimu sana. Na sisi kama taifa tulichelewa sana. Sumatra ilikuwa imebezi sana kwenye nchi kavu kuzidi majini.

Nchi nyingi maji na nchi kavu vimetengwa kivyake. Kuwa na mamlaka ya usimamizi wa maji inaleta tija sana, sisi watu wa kusimamia majini walikuwa wachache sana. Kenya wenzetu wana Kenya Maritime Authority (KMA), South Africa wana (SAMSA), Australia ,Ghana (GMA).

Mamlaka sasa itafanya kazi zake kitaalamu,ingawa kuna upungufu wa vitendea kazi na wataalamu walioajiliwa na mamlaka kuhusu meli na usimamizi wa bandari.
 
Nilitania tu mkuu kwa maana ya kwamba upo vizuri nchi kavu na majini..
Asante pia kwa maelezo yaliyoshiba!
 
Mkuu ningependa kupata boti ya kutalii ziwa Victoria maximum seats ziwe nne.Napenda ile ambayo hata kama kuna mvua ziwani haiwezi nipiga.Kama naweza pata kwa hapa Tanzania ningeomba unipe bei yake kwa Tshs la kama zinapatikana nje(kuagiza) ningeomba unipe amount kwa USD.
🙏🙏
 
Mkuu ningependa kupata boti ya kutalii ziwa Victoria maximum seats ziwe nne.Napenda ile ambayo hata kama kuna mvua ziwani haiwezi nipiga.Kama naweza pata kwa hapa Tz ningeomba unipe bei yake kwa Tshs la kama zinapatikana nje(kuagiza) ningeomba unipe amount kwa USD.
🙏🙏
Mkuu hiyo boti ya watu wanne utapata isiyozidi mita 5. Sasa kwenye injini utachagua ipi yenye injini ndani(Inboard Engine) au injini nje (Outboard Engine).

Kama utahitaji kununua boti basi huu ndio wakati sahihi maana biashara ya kuuza boti sasa bei huwa chini kutokana na ugonjwa wa Corona.

Kwa hapa Tanzania wanaouza bei zipo juu sana. Ni bora ukaagiza Afrika kusini,Japan au China.

Boti hiyo ya unaweza ukapata kwa kuanzia USD 4000, vizuri tembelea Gumtree South Africa kuna boti nyingi zinauzwa kwenye minada.

Kama utaingiza nchini usiingize kama leisure craft utaje umeleta leisure fishing craft ili upate nafuu katika kodi maana kwenye uvuvi kuna msamaha kama zana za kilimo.
 
Mkuu hiyo boti ya watu wanne utapata isiyozidi mita 5. Sasa kwenye injini utachagua ipi yenye injini ndani(Inboard Engine) au injini nje (Outboard Engine).

Kama utahitaji kununua boti basi huu ndio wakati sahihi maana biashara ya kuuza boti sasa bei huwa chini kutokana na ugonjwa wa Corona.

Kwa hapa Tanzania wanaouza bei zipo juu sana. Ni bora ukaagiza Afrika kusini,Japan au China...

Nashukuru boss🙏🙏.Nikihitaji msaada zaidi ntakutafuta.
 
Mtandaoni ni kiasi gani!? Kuileta mpaka bongo

Na je kuwa dealer hapa tz kwa hizi mashine unahitajika kuwa na mzigo kiasi gani(mtaji)!?
Mkuu injini hizi mtandaoni zenye 6-8Hp wanauza USD600 na 25-40Hp bei ni kuanzia USD 1600-2000 hiyo bila shipping cost na tax.

Wanauza kuanzia injini 5 kwa jumla, kama ukiwa dealer unachukua injini kusafirisha sio gharama na kwenye kodi unaweza ukazipitisha kama zana za uvuvi.

Mimi ningekuwa vizuri ningechukua hata 10 hizi ukienda Mwanza,Mafia,Bukoba unarudi na cash.

Injini za boti bei zipo juu sana ukikuta 15hp ambayo ni used bila milioni 7 uchukui. Hizi za 6hp mpya unapata kuanzia million 3 na kuendelea.

Ukiwa dealer mkuu unaweza ukaleta na spea, spea mchina anatengeneza za kuingia kwenye Yamaha,Suzuki na Mercury.
 
Back
Top Bottom