Ni wakati wa wanachadema kumuelewa Dr. Slaa na kumuwajibisha Mbowe!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Dr Slaa hakukataa hivi hivi kudahili makapi ya CCM bila mpangilio.

Hii ni kwa sababu Dr Slaa alikuwa na mpango mkakati wa kuunda Chadema yenye nguvu kwa maslahi ya upinzani na watanzania kwa ujumla.

Jambo hili lisingeweza kufanikiwa kwa kutegemea makapi tena yenye sifa chafu kutoka CCM.jambo hili lilihitaji wanachama asili wanaounda chadema kutokea kwenye msingi.

Ilifaa kuwe na utaratibu maalumu zaidi ya biashara za kununuliwa katika kudahili oil chafu na makapi kutoka CCM.

Wengi wa wanachadema mamluki walidhania kuwa Slaa ni mbishi,asiyejua mahesabu au aliyehongwa na CCM.HIVYO maoni ya Slaa juu ya utaratibu wa kuchukua makapi ya CCM yalipuuzwa.

Juma Duni hajji aliondoka Chadema mara baada ya uchaguzi ilihali ushirika wa UKAWA ukisemekana bado upo...sasa kilichomtoa Chadema ni kipi??

Lawrance Masha anaondoka Chadema akitaja hoja za msingi kabisa kwamba yale aliyoyaamini kuwa yanafaa ndani ya Chadema sio ya kweli bali ni ujanja ujanja wa kula ruzuku za serikali na wafadhili tu.

Mwenyekiti Mbowe anatakiwa ajiuzulu kwa kwenda njia ya kushoto kabisa ukilinganisha na matarajio ya Chadema kama chama na matarajio ya wananchi kwa chadema.

Hoja ya kwamba kupigania demokrasia na haki inahitaji uvumilivu haimaanishi lawarance Masha ndio kakosa uvumilivu bali ni Chadema yenyewe iliyokosa pumzi ya kujiamini na kujisimamia bila utegemezi wa makapi ili kufikia tamati.

Chadema ya Mbowe inaamini kutuletea mabadiliko,kupigania haki na demokrasia nchini huku ikitaka kuwatumia wale wale tuliowasema wanakandamiza haki,mafisadi na wabadhirifu...Huu ni ujuha ambao hata mtoto mdogo anaushangaa.

Mwenyekiti Mbowe kubali kuwa umekosea sana kutaka kuipandisha Chadema kwa makapi yaliyotaka kusababisha CCM ife.

Leo hii ninafurahi sana kuona somo la kwanza kutoka kwa Masha linaandikwa na kusomwa...tuendelee kusubiri somo la pili na hatimaye injili takatifu.

Nategemea Kingunge...Sumaye...Makongoro na hatimaye lowassa kurejea CCM na watafanya hivyo hivi karibuni au baadaye katika wakati utakaoumiza sana.

Mwenyekiti Mbowe atupe sababu ya kwa nini wanachadema wanahama na sio kutubabaisha na porojo za watu kuhongwa kama ilivyokuwa kwa madiwani...Masha hajahongwa ameamua kidemokrasia kabisa hata katibu Mashinji amekiri hivyo.

CCM ilipata tiketi ya kutawala milele mwaka 2015 kwa uzembe au makusudi ya Mbowe.
 
Chama kimeshika majiji yote chini ya mbowe kwako ww mafanikio ni nini?mtu yeyote anaye kubali kununuliwa hulaaniwa fuatilia historia ya yuda escaliuti
Kushika majiji yote ilikuwa ni "pi" kwa kuwa kazi kubwa sana ilifanywa na Slaa na wanachadema asilia.2015 ilikuwa ni zaidi ya majiji kama ushauri wa Slaa ungefuatwa.

Opportunity iliyopotea 2015 inabadilika na kuwa kaburi la Chadema.
 
CCM aliondoka Nyalandu kwa sababu ambazo aludai ccm imepoteza dira. Leo CHADEMA anaondoka Masha kwa sababu pia chadema haina dira.

Hii ni hatari kwa wanachadema ambao waliingia kwenye chama hicho kwa kukumbwa na propaganda tu.
 
tulionya tangu mapema kwamba ujio wa Lowasa na wenzake kutomka ccm tena walitoka baada ya kukatwa ccm, lilikuwa ni kaburi la chadema. ukweli na uongo huwa havikai pamoja. Mbowe huu ni muda muafaka wa kujiuzuru uenyekiti na kumuomba radhi dk Slaa.
 
tulionya tangu mapema kwamba ujio wa Lowasa na wenzake kutomka ccm tena walitoka baada ya kukatwa ccm, lilikuwa ni kaburi la chadema. ukweli na uongo huwa havikai pamoja. Mbowe huu ni muda muafaka wa kujiuzuru uenyekiti na kumuomba radhi dk Slaa.
Wito huu kwa Mbowe ni wa siku nyingi...namfananisha na Mugabe.
Mbowe hana sababu mpya ya kusingizia hili anguko na aibu ya Chadema.
 
Walishasema kama mtu aliyepanda tren wapo watashuka na wengine watapanda hiyohiyo tren wapandaji hawajulikani ni wema au waovu ila wanaoshuka na mlobaki mkiendelea na hiyo safari yenu salama mjue walioshuka ni watu wema

lakini daima wanaopanda huwa ni wawasiwasi hamjui wana namabegi ya milipuko au ni manyofo wa mabegi yawatu na mifukoni mwa abiria mliomo ndani ya hiyo treni isiyofikaga safari yake

Ndomana slaa alikua abiria mwema aliyeshuka njiani na walioendelea wanafasiri salama mpka leo japo hawafiki hiyo safari

Angalizo ni hao abiria wanaopanda bila kukwakagua mjue hiyo safari itakuja fia njiani tu.
 
Kwanza ungetueleza, how you, as an individual, would benefit with Mr. Mbowe's resignation.

Pili, una-comment nini kwa wana Chadema au wapinzani wanaovihama vyama vyao na kujiunga na ccm.

Tatu, je m- ccm akihamia say Chadema na huku akiwa na tuhuma za ufisadi ambazo serikali imeshindwa kuzithibitisha je Chadema wamhukumu tu wao bila mahakama kuhusishwa?

Nne, nini maoni yako kwani hata wakuu wa chi hii nao hawako salama saaana kwani nao wana hizo tuhuma, unafikiri kwa maoni yako nini kifanywe? Please tell us.
 
Acha vijana wa ufipa waje uone hilo povu Lao!
Maana wao hawapendi kuambiwa ukweli dawa yao ni uongo tu.
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom