Ni wakati wa wanachadema kumuelewa Dr. Slaa na kumuwajibisha Mbowe!

Hivi Ccm ni lini mlishawahi kuchagua/kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama chenu toka chama kiundwe????.
 
Maccm achaneni na mambo ya Chadema, tunajua Dr. Slaa yuko kwenye payroll yenu kama Chadema inaharibikiwa si ndiyo furaha kwenu? Wacheni umbwiga, pambaneni na ya kwenu.
Mada ipo nje ya upeo wako wa kufikiri. Waache wataalamu wa njia ya kuelekea ikulu watuelekeze wapi tumekosea mpaka tumepotea namna hii!
 
Fair meningitis!
Meningitis iliyoboreshwa, isiyoweza kuua.
Mstari kwa mstari hadi mwisho ni madini tupu bila makinikia.
Sasa atakayekuchongolea mdomo kwa hili, muwekee "star" na "kumnote" ili baadaye asije akatusumbua kujikosha.
Maneno yote uliyoongea ni sahihi 100%, sichangii kurekebisha neno lolote miye.
 
Someni Falsafa, Itikadi na Madumuni ya CHADEMA ndo mtaelewa.

Huwezi kukataza watu wanaotakiwa kujinga na chama cha siasa eti kwa hoja dhaifu za ufisadi ambao hata ukiambiwa uthibitishe huwezi ni ujinga.

Dr. Slaa sitaki kumzungumzia kwani askari aa kweli hupambambana akiwa ndani na si kutoka nje. Lakini pia huwezimfananisha na hao wanaohama na kwenda CCM ambako kimsingi ndiko kuliko na tatizo la kimfumo wa kiutawala.

Sikilizeni mwanachama yeyote wa chadema kama anamakosa anatakiwa kushikwa na kushitakiwa kama mhalifu mwingine, mleta hoja hebu nieleze ni mahakama ipi walipelekwa hao unaoita makapi, wahalifu, wachafu walipelekwa hata baada ya kupokelewa na chadema? Au serikali huwaogopa wakiingia Chadema? Kama siyo basi tuache kusema uongo na kuleta porojo hapa.

Kuhusu Mbowe, yule alichaguliwa na wanachama kwa mujibu wa katiba ya chadema na ubaya wa mwenyekiti huwezi kuonwa na kulazimishwa na Maccm, hivi nani mwenyekiti mbaya kati ya Magufuli wa CCM aliyebadili kifungu cha katiba kulazimisha kuwa mgombea wa bila kupingwa na yeyote na Mbowe wa CHADEMA?

Acheni unafiki tuwe tunasema ukweli. Maenyekiti aa ccm Magufuli wakati wa kutafuta wabunge wa EAC jina la Shairoz Banji alilitoa tena bila hata kujadili kwa kusema jina hili toa kabisa halipaswi hata kujadili Je hapo nani mwenyekiti wa hovyo kati ya Magufuli na Mbowe!?

Tujisahihishe, kwani mwanachama aa ccm si shetani kama mnavyotaka kutuaminisha.

ujinga ni kujua ujinga
 
Umesahau kuwa nyie mkiambiwa ukweli mnawamiminia risasi za SMG wakosoaji?

Ule ambao huwa anaongea lissu kwa kuwahadaa vijana na wafuasi wake wasiokuwa na upeo wa kudadafua zaidi ya kumshabikia (mtu anayedai tususiwe na tunyimwe misaada kisa ana maslahi binafsi na kutafuta cheap popularity sioni mchango wake kwenye maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mtu ambaye yupo kimlengo binafsi ama wa kutetea chama na si watanzania Mimi huwa nampuuza tu (Lissu)
 
Hivi Ccm ni lini mlishawahi kuchagua/kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama chenu toka chama kiundwe????.
Haikuwahi kufanya uchaguzi lakini ni bora wanaopokeana kijiti wanakuja na upeo na uwezo tofauti kuliko aliyekaa madarakani na kujimilikisha chama cha wananchi.
 
Mpaka sasa Chadema wapo katika njia sahihi, hakujawahi kuwa na chadema yenye utulivu na nguvu kubwa kuliko hii ya sasa, huo ushauri wenu mpelekeeni mwenyekiti wa ccm
Hilo ndio tatizo linalowakumba chadema ya kizazi hiki hata makosa kadhaa yanayofanywa na viongozi wanayafumbia macho. God bless CHADEMA
 
Sasa kama anahama 1, afu mkutano wa mtaa wanaingia 200 kuna shida gani?

Maajabu ni kuwa CCM ndio wanakerwa sn na uenyekiti wa MBOWE kuliko wana CHADEMA wenyewe!!
 
Mnamwona Mbowe mjinga wakati amewachukulia nusu ya nchi afu unaumia tena unataka akuchukue wewe

Ccm mnataka Mbowe aachie kiti ili mwahadae wanachadema ?Na kama kweli una Nia njema na Chadema kwanini hujui issue iliyomtoa Dr ,Slaa kwenye Chama
 
Back
Top Bottom