Ni wakati wa TISS kubadilika

escapee

Senior Member
Feb 1, 2020
133
210
Tanzania Intelligence and Security Service ni idara iliyo kama roho ya Taifa. Ikitokea Taasisi ikapwaya basi ni dhahiri taifa halitakua salama kisiasa, kiuchumi na Kibiashara.

SIASA
Ikiwa TISS itakosa weledi na upambanuzi wa namna siasa zinavyo paswa kuendeshwa, kulingana na dira ya uelekeo wa taiafa, ni lazima nchi ididimie. Kutakuwa na siasa zisizo na dira ya pamoja, ikiwa ni pamoja na vitendo vya rushwa na makundi makundi yenye visasi.

BIASHARA
Hii huambatana na njia zote za uzalishaji mali kama kilimo,ufugaji,uchimbaji madini, usafirishaji, utalii nk.

Hivyo kama TISS hawataweza kusimamia vema na kudhibit mamlaka zote zilizopo kwenye taasisi za uzalishaji mali, Taifa halitakuwa salama.

UCHUMI
Udhaifu wa idara ya usalama katika uchumi hupelekea nchi kuwa na uchumi hovyo.Siasa zisizo na dira hulifanya taifa kuwa na taasisi mbovu mbovu zinazo husika na kukuza uchumi.

Katika hayo yote unatambua kwamba Tiss inawajibika katika kila jambo ndani ya Taifa, iwe elimu, afya, majanga, siasa, ulinzi na mengine mengi. Na hayo yote yanawezekana kukiwa na siasa safi.

Hivyo sasa ni wakati wa TISS kubadirika kukitawala chama kilichopo madarakani, kwa kulinda misingi imara ya chama na ufwatwaji wa katiba ya Jamhuri. Na siyo wanachama wa ngazi za juu kuwa na nguvu dhidi ya taratibu za kikatiba.

MAGUFULI
Ni mwanaume miongoni mwa wanaume walio lipigania taifa hili. Kipindi cha nyuma ilikuwa mwenye madaraka anasujudiwa, kumuona DC, DED, OCD, DSO ilikuwa issue. Lakini sasa tuna share nao vingi hata mtaani angalau wanatafuta kiki.

Ameweka nidhamu na woga kwa watumishi na viongozi mbalimbali kwenye nyadhifa tofauti. Ni muda sasa TISS kuanza kuyajengea mfumo imara wenye watu wanaodhibitika katika uendeshwaji wa Taifa.

TISS iwe nauwezo wa kuwatengeneza kina Magufuli wengi wanaoweza kudhibitiwa na mfumo imara anao tuatara, huku yeye akiutumia mfumo huo kuongoza Taifa.

NB.
TISS msaidieni Magufuli kutengeneza mifumo imara inayo lisimika Taifa. Mifumo hiyo iwe na nguvu katika utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa sheria.

Magufuli aiogope TISS, na TISS imwogope Magufuli endapo yoyote kati yao hatafanya ufanisi kwa misingi ya kikatiba.

Magu ameonesha njia wengine jengeni misingi,kwani kazi aliyo ifanya huyu Mzarendo ni kubwa, jamaa anaweza.

Hapa nipo sehemu inaitwa Malampaka, Simiyu. Nina gari binafsi Kulga V nimetoka Dodoma naeelekea Sirari, aiseee natembeaaaaa. Speed 100-130. Jamaa MAGU kajenga barabara mpaka Bariadi.

MAGU THE MAN
 
Kama wataendelea kujaza green guards huko TISS usitegemee mabadiliko yoyote mpaka Yesu arudi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ushauri ni ushauri tu kaka,haijalishi umetoka kwa kigugumizi ama pambio.Rudia kusoma jina lako la utambulisho.
Sasa kama Mtu Uandishi wake tu anakoseakosea Kuandika vyema maneno yake, hivi hata huo 'Ushauri' wake utazingatiwa kweli na hao sijui TISS?
 
Ushauri ni ushauri tu kaka,haijalishi umetoka kwa kigugumizi ama pambio.Rudia kusoma jina lako la utambulisho

Bandiko laweza kuwa lina Ujumbe 'murua' kabisa ila katika Saikolojia ya 'Uwasilishaji' ukikosea Kuandika mambo vyema 'unalilifisha' mno Kimjadala.
 
escapee,

Tatizo kubwa TISS ya sasa hivi wengi huteuliwa kwasababu ni CCM au marafiki wa viongozi na ndugu wa viongozi si kwa weledi na utaalamu wa kusaidia taifa, ndiyo maana TISS wameshindwa kulisaidia taifa katika nyanja ya uchumi maana wengi wanao teuliwa si wazalendo, TISS ni taasisi inayotaka wazalendo.
 
escapee,

Nimefurahi kusoma maoni yako kuntu.

Kwenye eneo la biashara na uchumi, ni muhimu tukawa na defined policy ya mahusiano ya nje ambayo ndiyo yawe operandi ya taasisi zatu.

Umuhimu ktk kuwekeza kwenye ujasusi wa uchumi na maendeleo ni muhimu sana hasa ikiundwa taasisi chini ya Baraza la Usalama la Taifa itakayokuwa na mkurugenzi wake ishughulike na eneo la biashara na uchumi kwa maslahi ya Taifa.
 
Mfumo wa TISS ni mgumu ni wa kurithi tangu uhuru 1961; wao wapo kuhakikisha assistance ya Serikali ya CCM.

Nchi za wenzetu TISS ndiyo think tank na mshauri mkuu wa Uchumi, Siasa, Usalama na mambo yote ya kiiteligensia hasa naendelea ya kisayansi etc

Tusiwalaumu, huu ndiyo mfumo tangu uhuru ambao taasisi hii haijabadilika, hata ungekuwa ni wewe ungetekeleza haya haya sababu mtu mmoja huwezi kubadikisha mambo ya mfumo mzima.

Kati ya mambo ya kuangalia baada tu ya uchaguzi mkuu ni mfumo wa idara hii na ile ya habari na maelezo pamoja na review kubwa ya Tume ya uchaguzi kwa ustawi wa taifa letu.

Cc. @TunduLissu
 
Back
Top Bottom