Ni wakati wa Taifa kuwekeza kwenye mpira na kuachana na mpira hamasa na mpira maombi

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
9,019
21,913
Kila mmoja ni shahidi kwa ili liliotea leo. Sisi kama taifa tuna safari ndefu kufikia mafanikio ambayo kila mtu anatamani kuyaona. Inatafakarisha tunataka kwenda mbele ikiwa vyanzo vinavyoweza kutupeleka mbele ni dhaifu.

Leo hii serikali kupitia wadau wa michezo wanaweza kuchangishana fedha kuhakikisha timu yetu inashinda ili isonge mbele. Ni nyema. tunasahau kwamba nyuma ya mafanikio kuna uwekezaji. Kama tunaweza changishana kufikia kiasi cha billion shilingi tunahishindwa vipi kuwekeza katika miundo mbinu ya mchezo wetu mfano viwanja.

Huwezi ukawa na wachezaji wanaocheza katika mazingira mabovu kupitia ligi yetu.wachezaji wanaofahamu kupiga pasi kumi ni kosa kisa mazingira ya uwanjani. Tuwekeze kwenye miundo mbinu itawajengea wachezaji uwezo na hali ya kua bora na siyo kukimbia ovyo kama wako majarubani kuogopa mdudu kamasi.

Kama maombi yangekua yanacheza hakuna taifa lingejikita kujenga mazingira wezeshi kuanzia vijana hadi wakubwa. Kama hamasa ingekua inacheza hakuna timu iliyonyumbani ingefungwa hii dunia

Tuache siasa za mpira ni chanzo za kutugawa pia. Safari ya kuvuka kundi ili ni ngumu sana.
 
Soka la Tanzania ni sehemu ya kutafutia umaarufu. Hatuna wasimamizi wa soka bali tuna wasimamizi wa matumbo yao kupitia soka.

Miaka 60 ya Uhuru tunakosa kutambulisha taifa letu kimataifa kupitia michezo hata kurusha tufe? Olimpiki washiriki watatu wanasindikizwa na genge la wahuni 10 kisha tutegemee ushindani kwenye soka au michezo nchi hii!

Tuna upumbavu sana sisi.
 
Soka la Tanzania ni sehemu ya kutafutia umaarufu. Hatuna wasimamizi wa soka bali tuna wasimamizi wa matumbo yao kupitia soka.

Miaka 60 ya Uhuru tunakosa kutambulisha taifa letu kimataifa kupitia michezo hata kurusha tufe? Olimpiki washiriki watatu wanasindikizwa na genge la wahuni 10 kisha tutegemee ushindani kwenye soka au michezo nchi hii!

Tuna upumbavu sana sisi.

Ni kweli tuna changamoto nyingi sana, wizara ya michezo inashindwa kuipa nguvu michezo. Matokeo yake ata michezo ya kurusha vitufe au kupiga makasia tuanashindwa shiriki.

Tuna safari ndefu kupitia siasa zetu na siasa za chama tawala
 
Tatizo la tz wadau wote - wananchi, serikali, vyama vya siasa, wanasiasa, makampuni na wadau hatutaki kuwekeza kwenye soka. Tumejikita katika kuwekeza kwenye Simba na Yanga tu. Utashangaa makampuni yanapigana vikumbo kuwanunulia yanga na simba jezi na mabasi na kuziacha timu zingine zinakodi hiace na Coaster.....kisha tunaota tuwe na timu bora ya taifa ili hali tunawekeza ktk timu za kishangigi
 
Back
Top Bottom