Ni wakati wa Serikali kupandisha mishahara ya watumishi wa umma, hakuna kisingizio cha kutopandisha, uzalishaji umeongezeka

Ni kweli, lakini serikali hii inapika data sana, hivyo sio rahisi kuongeza mishahara maana makusanyo wasemayo sio ya kweli.
Sisi tunaamini mamlaka zenye kutoa data,kama wanadanganya watakuwa na makosa.

Kwa nini wadanganye? Ili wapate faida gani?
 
Wanabodi hili ni bandiko la kuelezana ukweli,na kama viongozi wetu ni wakweli basi hakuna haja za kusubiri mpaka mei mosi ifike ili mishahara ya watumishi wa umma iongezwe.

Mwaka 2017 kwenye mkutano mkuu wa 33 wa ALAT jijini Dar es salaam rais JPM alisema hawezi kuongeza mishahara ya watumishi wa umma sababu uzalishaji ulikuwa chini na hivyo serikali ilikuwa bado na mzigo mkubwa kuwahudumia wananchi.

Rais JPM alisisitiza kuwa wananchi wanatakiwa wahimizwe kulipa kodi na kufanya shughuli za uzalishaji ili pato la taifa liongezeke.

Hivi sasa TRA wanakusanya Tril 2 kwa mwezi ongezeko ambalo ni kama 50% ya kusanyo la bil 800 walizokuwa wanakusanya wakati wa awamu ya nne. Hivyo ni dhahiri kuwa sasa uzalishaji umeongezeka kama alivyotaka Rais JPM. Na kwa mantiki hii serikali inaouwezo wa kuongeza mishahara huku ikiwahudumia wananchi vizuri tu bila shida.

Ni aibu kubwa kwa taifa ambalo limeingia uchumi wa kati,huku mfumuko wa bei upo juu na kuna Mtanzania analipwa sh 390000 kama basic pay. Akikatwa kodi anabaki na sh 360000. Hapo mtu utaweza kuishi kwa raha?

My take; TUCTA na vyama vya upinzani viibane serikali ili iwakumbuke kupandisha mishahara watumishi wanaohangaika kwa kipato kidogo huku kila siku wanasota kuwatumikia wananchi.
Hakuna kilichoongezeka hapo,ni Swaga za kisiasa tu,awamu ya nne billioni 800,zilikuwa hazihusishi,mapato ya halmashauri,mapato ya Idara za utalii,Wala mapato yatokanayo na faini mbali mbali za makosa ya jinai,
Sasa hv,jiwe na TRA yake ndio waanokusanya mapato,hakuna halmashauri inayoruhusiwa kukusanya mapato,
Pili anayetoa hizi takwimu,hawezi,kusema ukweli maana Jiwe,anataka useme kile kinachompendeza tu.
 
Sisi tunaamini mamlaka zenye kutoa data,kama wanadanganya watakuwa na makosa.

Kwa nini wadanganye? Ili wapate faida gani?

Aina ya siasa ya sasa inapelekea kusema uongo ili kuhadaa umma kuwa awamu hii inafanya vyema sana.
 
Ni kweli, lakini serikali hii inapika data sana, hivyo sio rahisi kuongeza mishahara maana makusanyo wasemayo sio ya kweli.
Mtasubiri Sana hata hilo lije kutokea. Hapa bora kusema ongeza tano.
 
TUCTA haiweze kusambaratika kwa sababu za nyepesi ulizoziweka hapa sema TUCTA ya sasa ina viongozi dhaifu sana uenda tulikosea sana kuchugua ni kama ccm ilivyokosea na kumleta huyu mzee wenu, huu ni mwaka wa uchaguzi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA binafsi nina imani kupitia mimi TUCTA inaenda kupata kiongozi imara sana na kurejesha makali yake, tumaini pekee la wafanyakazi ni mimi kuingia hapo juu niwapiganie siyo hawa viongozi waoga tulio nao sasa
TUCTA ni kama joka la kibisa.
 
Hakuna cha viongozi wala baba yakena viongozi ndipo tulikofika kama taifa hao wakilaumiwa pamoja na wengine wanaonewa tu.
 
TUCTA haiweze kusambaratika kwa sababu za nyepesi ulizoziweka hapa sema TUCTA ya sasa ina viongozi dhaifu sana uenda tulikosea sana kuchugua ni kama ccm ilivyokosea na kumleta huyu mzee wenu, huu ni mwaka wa uchaguzi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA binafsi nina imani kupitia mimi TUCTA inaenda kupata kiongozi imara sana na kurejesha makali yake, tumaini pekee la wafanyakazi ni mimi kuingia hapo juu niwapiganie siyo hawa viongozi waoga tulio nao sasa
Hizo pesa mnazopiga huko TUCTA mjue zina malipo yake hata kama sio leo ila mjue mtazeeka na kufa vifo vibaya. Karma lazima iwaandame.

Hivi hapo TUCTA mmeshindwa hata kuishitaki serikali hata kama mtashindwa kesi mahakamani basi watumishi wataamini kwamba mnapambana. Mnaona ni hasara sana kuwalipa wanasheria sio.

Hovyo kabisa. Endeleeni kugombania madaraka na kujilipa mishahara minono na malupukupu ya kutosha mkidhani nyie ni wajanja sana.
 
Nauliza,ingekuwa mimi ningedoubt kama serikali inakwama kufanya mambo yake. Lakini naona wanakomaa huku watumishi wanaumia.

Umepitia deni la taifa limepanda kwa kiasi gani ndani ya hii miaka mitano? Huko ndio siri yote iliko.
 
Back
Top Bottom