Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Kila mfuatiliaji wa masuala ya kiuchumi atakuwa amegundua kuvunjika kwa daraja lililokuwa likiunganisha sekta binafsi na serikali kwa maendeleo ya nchi.
Aina ya mwenendo ambao serikali yetu umeuchagua una madhara makubwa kwa RAIA na ni lazima tupige kelele kusudi mtazamo wa serikali ubadilike.
Serikali imekuwa ikifanya yafuatayo kudidimiza sekta binafsi:
1.Serikali inawaaminisha wananchi kwamba sekta binafsi ni wanyonyaji na siyo wadau muhimu katika uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Kwa mfano, kuna wakati wizara ya Elimu ilianza kampeni ya kuweka school fees ceiling price, hii ilikuwa sawa na kuuaminisha umma kwamba ada za shule binafsi zimekaa kinyonyaji.
2. Serikali inawagawa wadau wa sekta binafsi na kuingilia Uhuru wa soko.
Rejea kauli ya Rais alipoipigia chapuo benki ya NMB dhidi ya benki nyinginezo. Kwa lugha ya masoko JPM aliwapa free public confidence NMB wakati yeye anastahili kuwa neutral kama kiongozi wa serikali. Suala LA serikali kuwa na hisa NMB siyo sababu Bali lengo ni kuwagawa wadau. Mbona serikali inaimiliki TPB BANK karibia kwa asilimia zote lakini hajaipigia promo?
3.Serikali inawachukulia wadau wa sekta binafsi kama wapiga dili.
Mtazamo hasi huu umepata nguvu sana hususani miongoni Mwa RAIA wasiojielewa. Kwa mujibu wa ripoti ya CAG serikali hii hii inayotamba kuzingatia sheria na kuzuia ufisadi imeripotiwa kutumia mabilioni ya shilingi pasipo kufuata sheria za manunuzi. Hiyo ishara ya kutokutaka sekta binafsi ishiriki katika mipango ya maendeleo kimya kimya.
NINI KIFANYIKE?
Ni wakati sasa wa wadau wa sekta binafsi kukaa mezani na kujadili mustakhabari wa RAIA tunaoamini hakuna maendeleo bila uthabiti wa sekta binafsi.
Ni lazima serikali iheshimu soko huria. Wafanyabiashara wanafunga biashara kwasababu pamoja na mambo mengine makadirio ya kodi yamekuwa makubwa kuliko kawaida.
Badala ya ajira Mpya kuongezeka hata zilizopo zinakufa?
SASA SEKTA BINAFSI ITOE TAMKO ILI SERIKALI IFAHAMU MWENENDO WAKE