Ni wakati wa mavuno kwa waganga wa kienyeji na madalali wao

Waganga wa kienyeji watu wabaya sana
JamiiForums-954772894.jpg
 
naona vita ya kupinga ushirikina. mkuu hata upige kelele vipi, hayo mambo ndio dini za watu kama ambavyo mnavyoabudu sanamu la bikira maria na mengine..kila mtu ana uhuru wa kuabudu anachoamini
haya mengine ni porojo tu na lazima kila mmoja aheshimiwe na anachokiamini. sio lazima wote muabudu au kuamini the same.
 
Machoni pa wengi tunakataa kuwa hakuna ushirikina lakini nyuma ya pazia tunauabudu tena kwa heshima zote.

Ni kipindi kuelekea uchaguzi mkuu. Karibia kila mgombea anatafuta support na booster ya nguvu za giza.

Kuna fedha nyingi sana zinawekezwa kwenye hili eneo na ni wakati wa waganga kuzipiga bila huruma.. Udalali uko kila mahali. Hata kwenye ushirikina pia.. Hivyo kipindi hiki ni kipindi cha neema pia kwa madalali wa waganga wa kienyeji...

Ukitaka kujua kuwa ni kipindi cha neema angalia hata yale matangazo ya nguvu za kiume fulimasoni na pesa za majini yamepungua sana.

Yote juu ya yote ni kipindi kibaya na cha huzuni kubwa kwa wanyama kama kuku wa kienyeji, mbuzi na ng'ombe na hata kondoo pia.. Kwa baadhi ya matukio hata watu wanaopotea pia... Na kwa sehemu ajali zinazouwa kwa wingi.

Hiki ni kipindi cha kukuta nazi zimepasuliwa njiapanda ama kukuta vitu vya kishirikina pembezoni mwa barabara, ofisini ama hata kwenye nyua za makazi..
Kipindi hiki familia za waganga wa kienyeji wanazikinai nyama.. Wanakula supu, wanachoma, wanaoka, wanabanika, wanakaanga..

Vichwa hawali
Makanyagio hawali
Utumbo hawali.. Wanatupa.. Ni full kujiachia

Ni kipindi cha kumsahau Mola kwa muda na kufanya makafara na mazindiko ya kila aina.. Ni kipindi cha kuwa mateka kwa muda.. Mateka wa waganga kwakuwa utafanya kila atakachokuambia bila kuhoji.. Hata akikwambia kamlale mwanao wa kumzaa hutakataa na utafanya kwa utiifu mkubwa

Kuna hasi na chanya kila mahali.. Watakaofanikiwa utawaona nyumba za ibada wakimshukuru Mungu.. UNAFIQUE..! Watakaokosa wataambiwa walikosea masharti na watalia kimya kimya...

Wanasiasa hawa waone hivi hivi....
View attachment 1509186
Tupo pamoja kimaono kwamba siasa ni mchezo mchafu. Ni wachache sana ambao wanafanakiwa katika ulingo huu kwa kudra za Mwenyezi Mungu.
 
Ahsanteni watia Nia! Naona mnaanza vita vya kiufundi wa kisayari. Mzigo umeokotwa mbele ya Branch ya CCM Malindi
JamiiForums-320044438.jpg
 
Taasisi zinazojishughulisha na uhifadhi wa wanyamapori nao wanatakiwa kuwa ngangari kwa doria na upelelezi wa kina

Vinginevyo wanyamapori pendwa kwa Ulozi watakuwa taabani kwa majeruhi na vifo na kuacha uzao wao ukiteseka.

Wanyama kama 1- fisi
2- Simba
3- Nyumbu
Nk.
The list is not exhaustive. 4.Ngekewa
5.Nhungunhughu
6...
 
Masharti feki..

 
Back
Top Bottom