Ni Wakati Wa Mabadiliko, Leo Tumia Saa Moja Kufanya Jambo Hili Muhimu

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,473
2,000
Sehemu kubwa ya watu tumekuwa tunaishi maisha ambayo hatujui kwa nini tunafanya tunachofanya. Yaani sasa hivi ukasimamishwa na kuulizwa kwa nini leo unaenda kazini utajibu kwa sababu nataka nipate hela ya kuendesha maisha. Kwa jibu kama hili ni vigumu sana kuweza kufikia mafanikio kupitia hiko unachofanya.
Watu wengi wamekuwa wakiishi maisha waliyoishi jana na kuyaishi tena kesho.

Umekuwa ukienda kwenye kazi yako kwa sababu jana na juzi pia ulienda. Umenunua kitu fulani kwa sababu kila mtu anayekuzunguka amekinunua. Unaishi maisha fulani kwa sababu kila anayekuzunguka anayaishi.
Inaweza kuonekana ni kitu kizuri kwa sababu huachi nyuma ila ni maisha magumu sana na ya mateso. Ni maisha ambayo yatakufanya uishi kama mtu asiyejua ni wapi anaelekea.

Ni maisha ambayo yanakufanya uende kazini, ufanye kazi usiyoipenda ili kupata mshahara ambao hautoshelezi na kwenda kulipa madeni, baada ya hapo mzunguko unaanza tena. Ni maisha ambayo yatakufanya uende kazini kila siku kwa miaka zaidi ya ishirini na kuja kustuka pale ambapo una staafu huku hujafanya maandalizi yoyote.

Soma; Hivi ndivyo Unavyokufa na Miaka 35 na Kuzikwa na Miaka 65

Ni maisha ambayo hayawezi kukufanya utumie uwezo mkubwa uliopo ndani yako. Utaendelea na maisha hayo mpaka lini?

Umeishi hivyo mwaka jana, umeishi hivyo mwaka juzi na hata mwaka huu unaoelekea kuisha nao umeishi maisha hayo hayo. Umeishi kwenye mzunguko huu wa amka asubuhi, nenda kwenye kazi ambayo huipendi, fanya kazi kwa nguvu sana, lipwa mshahara ambao haukutoshelezi, nenda kalipe madeni, anza kukopa tena na mzunguko mzima unajirudia.

Swali ni je utaendelea na maisha hayo mpaka lini? Je umekubali kufa na miaka 35 na kusubiri kuzikwa na miaka 65? Kama jibu ni ndio nakutakia kila la kheri, maana hakuna awezaye kukusaidia kama mwenyewe hujakubali kubadilika. Kama jibu ni hapana, hongera sana maana unaweza kubadili hali hiyo na kudai uhuru wa maisha yako ambao ulikuwa umeupoteza.

Leo tarehe 01/12/2014 ni siku ya kwanza ya mwezi wa mwisho kwa mwaka huu 2014. Tumia siku ya leo kuanza safari ya mabadiliko kwenye maisha yako. Tenga saa moja leo na tumia muda huu kutafakari maisha yako kuanzia mwaka huu umeanza. Fikiria ni vitu gani ulipanga kufanya na ni vipi umetekeleza. Pia fikiria ni vitu gani umeshindwakutekeleza na ni kwa sababu gani.

Fikiria hayo tu na usiweke malengo yoyote kwa mwaka 2015 leo. Nakuambia hivi kwa sababu kuna kosa kubwa sana ambalo umekuwa unalifanya kwenye kuweka malengo yako. Leo yatafakari maisha yako na fikiria ni jinsi gani unaweza kuyaboresha.

Wakati mwingine tutakuja kusaidiana hatua kwa hatua kuandika malengo ambayo ni lazima utayafikia.
Usiache siku ya leo ipite bila ya kufanya tathmini hii muhimu. Kama unaona huwezi kupoteza saa moja kufanya zoezi hili muhimu naomba nikukumbushe kwamba mpaka kufikia leo umeshatumia masaa 8040 kati ya masaa 8760 yaliyopo kwenye mwaka huu 2014. Hivyo ni muhimu sana kwako kutenga saa moja kabla hujapoteza masaa mengine mengi kwenye maisha yako.

Mwezi huu wa 12 AMKA CONSULTANTS imekuandalia mambo mengi mazuri sana ya kukuandaa kuianza 2015 ukiwa na nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko kwenye maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA!

Makirita Amani.

Kwa ushauri andika email kwenda ushauri@kisimachamaarifa.co.tz
 

grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,457
1,500
Mkuu huo ujumbe umegusa moyo wangu sana. Kila mara nafikiria nikitangulia mbele ya haki leo hii nitaacha nini cha kuwafanya wanangu wajisifu kuwa na Baba kama mimi
 

grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,457
1,500
Mkuu mbona hiyo link uliyotoa hapo juu imenirudisha kwenye orodha ya majukwaa ya JF?
 

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,372
2,000
umesomeka kiongozi uwezo mkubwa uliomo ndani yako [infinite inteligence) kiroho zaidi cheers...thumb up
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,712
1,225
Inasound vizuri.

Issue ya watu kufanya kazi wasizozipenda imekua janga la taifa kwa nchi masikini hasa Tz. but source ni ujinga, maandalizi mabovu ya wazazi na elimu isiyo na tija.

hicho ulichokizungumzia ni muhimu but hakitumiki vyema na watu stahili na kinyume chake tunaengeza idadi ya mafisadi. i know you know what going on now in TZ. (escrow) ni ngumu sana kupata maendeleo ya m1 m1.
 

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,473
2,000
Inasound vizuri.

Issue ya watu kufanya kazi wasizozipenda imekua janga la taifa kwa nchi masikini hasa Tz. but source ni ujinga, maandalizi mabovu ya wazazi na elimu isiyo na tija.

hicho ulichokizungumzia ni muhimu but hakitumiki vyema na watu stahili na kinyume chake tunaengeza idadi ya mafisadi. i know you know what going on now in TZ. (escrow) ni ngumu sana kupata maendeleo ya m1 m1.
Ni kweli mkuu, ila pamoja na mambo yote bado kila mmoja wetu anaweza kuchukua hatua na kubadili maisha yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom