Ni wakati wa Kurudia Vijiji vya Kujitegemea (Vijiji vya Ujamaa 2.0)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,375
19,377
Ukitaka viite jina lolote, Kibbutz, self-contained cities, 30 minutes city, vijiji vya kujitegemea au ujamaa, na kama Kijiji ni neno duni basi tuviite miji inayojitegemea.

Umoja ni nguvu.., na hakuna kiumbe ulimwengu huu ambaye hategemei kiumbe mwingine.., hata simba bila kumfanya swala kitoweo basi ni budi ajifunze kula nyasi…, Ubepari ambao tunaona unafaa na kuusifia kwa kuleta bei ndogo na ushindani unategemea unyonyaji wa masikini ili kuweza kupata rasilimali na nguvu kazi kwa bei nafuu…, na tunapoelekea idadi ya watu inazidi-kukua na rasilimali kupungua, bila kujenga jamii ambayo msingi wake ni watu, kufanikiwa kwake si kwa muda mrefu.

Hapa ujamaa naongelea kutegemeana katika uzalishaji, siongelea extremes za Kibbutz huko Israel ambapo jamii ya wakulima walikuwa wanagawama kila kitu kwa usawa yaani hata ukiwa unafanya kazi nje unachopata unawapa Kijiji ili mgawane sawa…. Na kila kazi iliyopo mnafanya kwa zamu….., HAPANA…, nachoongelea hapa ni kazi zilizopo ili kuzalisha kinachohitajika kwa wote ziweze kufanywa na yeyote anayetaka ili aweze kujipatia fedha za kujikimu.mgawanyiko wa kazi kulingana na idadi ya watu ili kila mtu aweze kufanya kazi kidogo iwezekanavyo bila kupunguza uzalishaji, na aweze kupata kipato cha kujikimu katika mji.., pia chochote cha ziada ambacho kinatakiwa na hakizalishwi katika jamii kuweza kununuliwa kwa ujumla hivyo kupata punguzo la bei

Kwa ufupi sio kugawana mapato baada ya kazi bali kugawana kazi ili kupata mapato, na ili kuwepo kwa usawa, utofauti uwepo kwenye anasa mtu anazoweza kutumia kipato chake na sio mambo ya msingi kama nyumba, elimu, afya mafao ya uzeeni n.k.

Miji Janja yenye Ufanisi (Smart City)
Miji ambayo kila data inajulikana. Idadi ya mahitaji na matumizi, idadi ya wagonjwa na uhitaji wa madawa, hii itapelekea kutokuwa na upotevu na uharibifu wa malighafi na kupelekea uzalishaji wa wakati kulingana na mahitaji, na kwenye afya kwa kupata data mapema itapelekea uwezekano wa kuzuia magonjwa badala ya kuhangaika kutibu.

Sio Nyumba kwa Wote tu, bali Uwezo wa Kuishi kwenye Nyumba Hizo
Nyumba bila uwezo wa wenye nyumba kuweza kumudu Maisha katika nyumba hizo ni kujenga magofu na makazi ya masikini ambayo mwisho wake hakuna atakayetaka kuishi. Kabla ya mtu kupewa ufunguo wa nyumba ya mji husika ni lazima apewe ujuzi wa kufanya kazi zilizopo katika mji ili aweze kumudu Maisha. ya mji huo.

Kugeuza Uchafu kuwa Malighafi
Katika karne ambayo mazingira yanachafuliwa kila kukicha miji inatumia gharama kubwa sana kukusanya uchafu na kuutupa, wakati uchafu huo ungeweza kutumika kuwa malighafi,mfano; kinyesi kama mbolea ya mazao ya nishati, haja ndogo kuwa recycled na kutumika tena kwenye maji ya chooni na maji yote ya kuoga na vyombo kutumika kwa umwagiliziaji, kila jengo kukusanya nguvu za jua na kila nyumba na wenye nyumba kukusanya mabaki na uchafu kutumika kwenye Biogas plants kwa ajili ya nishati.

Usafiri wa jamii wa Uhakika
Kupunguza gharama za usafiri na nishati kwa usafiri wa jamii kutumia umeme na kila kona ya mji na sehemu za kazi, kuwa na usafiri wa uhakika, hii itapunguza upotevu wa muda unaotokea sasa kwa watu kusafiri kila siku,muda ambao unaweza kutumika katika uzalishaji au anasa ambazo zitachangia katika mapato ya mji.



Katika karne ya Teknolojia, kila kiwezacho kufanywa na Mashine kifanywe na Mashine
Ni ukweli usiopingika kazi nyingi za kujirudia zaweza kufanywa na mashine, kwahio kuliko kungangania kazi ziendelee kufanywa na watu kwa jina la kupata ajira ni vema kazi nyingi zifanywe na mashine kwa faida ya wote.., zile chache zinazobaki zivunjwe kuwa kazi nyepesi ili ziwezwe kugawanywa kwa jamii.., mwisho wa siku kila mwanajamii afanye kazi chache iwezekanavyo na kupata muda wa kupumzika na kufurahia Maisha., Malipo, manunuzi, mahesabu, sharia, kupangia watu kazi na usimamizi wa kazi vyote vinaweza kufanywa na mashine kwa ubora kuliko binadamu na vifanywe na mashine…, hivyo kazi za ubunifu, starehe, uangalizi wa wagonjwa na wazee, mipango ya maendeleo n.k. vinavyohitaji inteligensia zitafanywa na wananzengo.

Nini Ubaya wa kujitegemea na Je Mbadala ni Bora ?
Tunaposema ujamaa unaleta umasikini bepari wa nchi ziliondelea atakuelewa, lakini masikini wa nchi zinazoendelea anaweza tu kukubali propaganda hizo kwa vile uwepo wake ni misingi ya ubepari, Je ni bora kuwa na hii miji ambapo kila mtu ana kazi za kumwezesha kupata malazi mavazi na chakula au kuendela na hali ya sasa ambapo wachache wanasaza na wengi wanaishi kwa kutegemea hisani za wanasiasa na makombo ya mabepari ?

Watu ili Wajitegemee lazima wapewe Ujuzi na Walipwe pesa ya Kujitosheleza
Watu kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa kupata mkate wao wa kila siku na familia zao na kuwa na uhakika wa kesho yao ndio njia pekee ya maendeleo ambayo hayatamuacha mtu yoyote nyuma.

Watu wajitegee sio kutegemea Mwekezaji au Serikali
Serikali inaendeshwa na watu wachache kwa niaba ya wengi, na tangu enzi za zama za kale, binadamu ni mchoyo kiuhalisia, kabla hajaangalia wengine anajijali yeye na watu wake, sasa ukizingatia wanasiasa ni watu wa kupokezana vijiti kila baada ya miaka kadhaa, hivyo kila wanapopewa kazi ya kuangalia na kuigawa keki ya taifa na muda wa kufanya hivyo ni mchache, basi utaona kwamba muda mwingi wa uongozi wao watakuwa kwanza wanajigawia keki kabla ya kukumbuka jamii…

Mwekezaji yeye anajali faida kabla ya ustawi wa jamii husika…, hivyo kujilimbikizia mali huku akitoa kwa jamii kidogo iwezekanavyo. Hivyo basi kama watu wana ujuzi na kwa ujuzi huo wanaweza kuzalisha.., na mazalisho hayo yanahitaji mtumiaji, iweje wategemee mwingine awazalishie ili awalipe kiduchu hata kupata shiida kununua kile walichiozalisha?

Je hii miji ya Ujamaa inayojitegemea inaleta umasikini ?
Wengi watasema hio sio njia muafaka na italeta umasikini.., swali ni umasikini kwa nani ? Yule ambaye anategemea wafanyakazi wa ndani na kuwalipa pesa kidogo ili yeye afanye kazi ya kuajiriwa pengine na kuwa mtu wa kipato cha kati, au huyo dada ambaye badala ya kuwa kijakazi atakuwa na kwake na kuweza kujipatia kipato yeye na familia yake.., au wale wapangaji, machinga na mamilioni ya wananchi ambao sio tu kwamba hawajui kesho yao, bali kila asubuhi wakiamka hawajui kama jioni watapata kitoweo…?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom