Ni wakati wa kujitambua (Jua ulikotoka)

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,834
Nawasalimia wana JF wote. Wale waliopo kwenye mfungo mzidi kubarikiwa na mzidi kuongeza juhudi katika imani yenu.

Ninaendelea kuongelea haya maswala ya kujitambua na kujua uhalisia wa dunia na viumbe mbali mbali. Kuhusu sayari na vitu vyote vinavyounda ulimwengu wa damu na nyama.

UTANGULIZI

Kuna mada zangu chache nimejaribu kuzitoa kuna baadhi wamezielewa lakini kunawengine bado zaidi ya yote kuna wengine hawataki kabisa hata kuingiza ujuzi wowote katika akili zao, labda huenda dini au imani zao zimewafanya wasitake hata kutafakari wao pekee.

Katika kusoma vitabu vya dini tofauti tofauti nimekuja kugundua kwamba hakuna dini inayosema ukweli 100% kuna mambo yaliyo mazuri lakini ukienda ndani zaidi na zaidi utakuta kwamba hizi dini asili yake ni tamaduni za jamii fulani. Ni vyema tukatambua kwamba uwepo wa dini umefanya angarau kidogo wanadamu wawe wastaarabu. Lakini hizi dini zimekuwa zikichukuliwa vibaya kizazi baada ya kizazi na kupoteza maana halisi ya asili ya dini hiyo.

Ninataka leo kuongelea hatua kwa hatua kujitambua na kuelewa kwanini wewe upo hapa ulipo? na unaenda wapi? umetoka wapi?

TAMBUA UWEZO WA AKILI
Akili yetu huwa inazaliwa na kufa. Akili zetu ni kama mmea unaomea katika mazingira tofauti tofauti. Mmea huo ukiwekewa mbolea utasitwi vizuri lakini usipokuwa kwenye mazingira mazuri unaweza ukadumaa na hatimaye kutokuzaa matunda mazuri. Vile vile akili zetu ni kama mkanda wa kurekodi, Unarekodi matukio yote na kuwekwa kwenye database. Kila tukio kwa kila sekunde huwa linakuwa na Unique key kwenye hiyo database. Kadri ya siku zinavyosonga mbele database huwa kubwa na inakuwa na data nyingi sana.

Matukio mengine huwa yamejificha sana, na inakuwa vigumu kwa kumbukumbu processing system kuyavuta ya kaja kwa mda unaotakiwa. Na matukio mengine hupotea kabisa. Kwa mfano japokuwa ulikuwa upo makini kwa dakika kumi zilizopita ni vigumu kukumbuka matukio yote. Kama umeshindwa kukumbuka matukio ya mda wa dakika kumi zilizopita je utaweza kukumbuka matukio yako ukiwa na umri wa miaka miwili? Kunapicha moja najaribu kujenga ili ninapoendelea tuweze kuelewana.

Milango ya fahamu ndio njia pekee ya kuinginza data kwenye database ya akili. Na kadri mtu anavyo zidi kuingiza vitu ndio akili yake inavyozidi kupanuka. Milango sita ya fahamu:
1. Taste
2. Touch
3. Thought
4. Smell
5. Hearing
6. Sight
Akili hujihusisha na mambo ya hapa duniani.

JITAMBUE
Akili ni matokeo ya kuwepo kwa mwili. Lakini sisi ni zaidi ya uwepo wa mwili. sisi ni sehemu ya uumbaji wa ulimwengu. Katika uumbaji wa ulimwengu tumejihusisha kwa sehemu kila mmoja. Sisi ni zaidi ya vitu vinavyoonekana na visivyoonekana.

Mtu anapozaliwa huwa na uwezo mkubwa sana wa kujua ni wapi alikotoka na anaelekea wapi. Kitendo cha kuanza kujaza akili vitu vya dunia tu na kusahau kuijaza akili asili na uwezo tulionao, tunajikuta tumekuwa wategemezi wa hii dunia ambayo tumeiumba sisi. Dunia hii tuliyoiumba ina siri kubwa sana na hatuwezi tukazijua hizo siri mpaka tutakapoanza hatua ya kujitambua.

Ili kurudi katika asili yetu ya mwanzo ni kuhakikisha kwanza tunaanza taratibu kufanya mazoezi ya kuzima milango ya fahamu. Hili swala linaenda hatua kwa hatua. Milango ya fahamu kama macho na masikio ni rahisi kuzima lakini "thought" huwa ni vigumu sana na inatakiwa kwenda hatua kwa hatua. Mtu anapozima hiyo milango ya fahamu anakuwa na uwezo sasa wa kuanza kuwasiliana na nafsi yake (Roho yake).

Hatua hiyo huenda hatua kwa hatua mpaka mtu anaanza kujitambua. Kuzima milango ya fahamu na kuanza kuwasiliana na roho yako huitwa "Meditation" Unapoendelea kuwasilia na roho yako utaanza kugundia vitu vingi sana na utajitambua.

HITIMISHO
Tungeanza safari hii ya kujitambua hakika tungeanza kuelewa vitu vingi. Nimeweka file la pdf kuhusu meditation ninakusihi upitie uweze kujua hatua za mwanzo na ujifunze.

Ahsante wote.


View attachment Meditation.pdfView attachment Meditation.pdf
View attachment Meditation.pdf
 
Asante dada mzuri ubarikiwe, sio kila siku tunajaza mambo ya MMU na Siasa kichwani
 
Naihitaji hii elimu mkuu Annael...kwa dhati kabisa...
Nahisi kuna vitu vingi havipo sawa maishani mwangu....
 
Last edited by a moderator:
Mbona vitu vizuri kama hivi vinaachwa kama vile havina thamani? Ukienda kwenye majukwaa ya mapenzi, siasa utani n.k utakuta watu wamejazana ovyo. Lakini hili jukwaa la intelligence watu wanachungulia tu sijui kwanini.
Hasa elimu hii ya kujitambua/elimu nafsi ndio kabisa huoni watu. Na hii inachangiwa na dini ambazo ndio kifungo kikuu cha kutokujitambua.
 
Back
Top Bottom