Ni wakati upi unajisikia amani Kati ya usiku na mchana

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,544
44,691
Wakuu mwili wako na nafsi yako inafurahia Zaid muda gani ukiwa macho mchana unafanya maisha na mishemishe zako au Bora usiku tunapoenda kulala ndio unahisi viungo vinajinyoosha vizuri.binafsi Mimi nimekumbwa na Hali ya kupenda kulala usiku kwani kujifunika blanketi na kujikunyata huku ukiota baadhi ya vindoto Ni Raha Sana.

Kukikucha shida zinaanza kukimbizana na kazi mwili unachoka na vilevile Dhambi nyingi nazitenda mchana yaani kiufupi mchana kwangu siukubali kwani nakuwa na mawazo mabovu. ningekuwaga Nina hela nyingi ningeajiri watu kazi Yao kuniletea tu hesabu.ningekuwa nalala sana ningekuwaga naamka asubuhi nafanya mazoezi ya mwili naota jua kdg huku nikipitia nyuzi zenu nakula msosi halafu saa nne asubuhi narudi Tena kulala naamka mchana saa tisa nakula Tena msosi nakunywa maji Sana Kisha napiga Tena matizi na kuoga Kisha nalala saa 11 mpk usiku huko naamka naswali,nacheki baadhi ya mambo then nalala Tena.

Ni raha Sana kulala japokuwa Ni katabia Cha uvivu nikafanikiwa kufaulu nikaingia mbinguni Basi nitamuomba mwenyeziMungu anipe tu usingizi wa kutosha usingizi mwingi.ni mtazamo wangu tu naomba isije kuwa pepo la mauti linaninyemelea.
 
Sahivi ni 50\50 ila kuna wakati nilipata amani zaidi usiku because I had someone to cuddle
 
Back
Top Bottom