singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
IJUMAA iliyopita Rais John Magufuli alitimiza siku 100 akiwa madarakani, baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana na kuapishwa rasmi Novemba 5.
Tathmini zilizofanyika kuhusu utendaji wa kiongozi huyo ndani ya siku hizo 100, imeonesha na kubainisha kuwa ni Rais anayetenda kile anachokisema na amekuwa akitekeleza kwa vitendo ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni.
Kwa kipindi cha miezi miwili, Rais huyo amekuwa gumzo ndani ya Tanzania, nchi jirani na duniani kote na amekuwa akitumika kama mfano wa Rais anayejali na kuweka mbele maslahi ya wananchi wake; na si watu wachache.
Ndani ya siku 100, kiongozi huyo amefanikiwa kuboresha huduma za afya, kuhakikisha elimu inatolewa bure kuanzia shule za awali hadi kidato cha nne, kuongeza mapato ya nchi, kubana matumizi yasiyo ya lazima, kuhamasisha uwajibikaji kwa watumishi wa umma, lakini pia kupambana vikali na vitendo vya ufisadi na rushwa.
Na hata katika hotuba zake, Dk Magufuli amekuwa wazi akiweka msimamo wake kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano, itahakikisha inaweka mbele maendeleo ya kiuchumi ya nchi na kuinua maisha ya wananchi kwa kuhakikisha keki iliyopo, inagawanywa sawa kwa sawa; na si kwa wachache.
Hata juzi alipozungumza na watanzania kupitia mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam, alikazia msimamo wake kuhusu nia yake ya kuboresha huduma kwa watanzania na kupambana na wote wanaotumia vibaya madaraka yao. Aliwataka watanzania nao kujitathmini wanaifanyia nini nchi yao.
Kauli hiyo ya Rais Magufuli ina ukweli, kwani pamoja na watanzania wiki iliyopita kutumia muda mwingi kutathmini utendaji wa kiongozi huyo na Serikali yake, tulisahau kujitathimini sisi wenyewe, tumeifanyia nini nchi yetu ndani ya siku hizo 100.
Ukweli pamoja na kwamba kiongozi huyo na Serikali yake kwa sasa wanatimiza kwa vitendo kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu, kila mtanzania ana wajibu kuunga mkono hatua hiyo na kuwajibika kuijenga nchi yake.
Yapo masuala mengi ya kusaidia kuijenga nchi, ikiwa ni pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kwa watumishi kuwajibika ipasavyo kwa kuchapa kazi katika shughuli za maendeleo, kufuata na kutii misingi ya Sheria bila shuruti na kubwa zaidi kuweka uzalendo kwanza.
Taifa ni umoja na pasipo umoja hakuna taifa. Kwa kiongozi yeyote yule makini na mwenye nia ya dhati kwa nchi yake, atafanya kila liwezekanalo ili watu wake wawe wamoja, kwa kuwa pasipokuwa na umoja, taifa lolote halitaweza kufikia malengo yake.
Hivyo basi ni muhimu pia kutambua kuwa Serikali haiwezi kujenga nchi peke yake, pasipo jitihada za dhati na kujitolea kwa raia wanaojenga nchi hiyo. Nchi itajengwa kutokana na jitihada za kila mtu kuanzia Serikali mpaka ngazi ya chini kwa wananchi.
Hilo litawezekana, endapo kila mmoja wetu atakuwa mstari wa mbele kufanya kazi katika kufikiri na ujenzi wa taifa. Tayari Rais Magufuli na Serikali yake, wameanza vizuri katika kusimamia na kuratibu mifumo itakayosaidia uchumi wa mtu mmoja na uchumi wa taifa, kulinda haki za raia na kulinda taifa dhidi ya maadui wa nje.
Lakini, sasa ni wajibu wa kila raia kutumikia taifa letu kwa dhati na kwa moyo wote. Wakati wa kulalamika na kuionyoshea mkono Serikali umepita. Sasa ni wakati wa kufuata nyayo za Serikali na Rais Magufuli kwa kuwajibika ipasavyo ili kulipeleka mbele gurudumu la maendeleo nchini kwa manufaa ya Tanzania.