Ni wakati sasa wa kufanya maridhiano.

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Amani na iwe kwenu!

Ni ukweli usio pingika kuwa Nchi yetu imeoza kila idara mpaka inatisha.Inaonekana kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita kila kiongozi eneo alilopo alijimilikisha kwa kadiri alivyo taka na kutumia mali za umma kama mali yake binafsi.Kwakuwa karibu kila idara imeoza, na kama kufukuza Rais atafukuza mpaka achoke, wakati sasa umefika serikali ifanye maridhiano na wafanyakazi wote wa umma waliofanya makosa mbalimbali ya kiutendaji wakiri makosa yao na warudishe mali walizo jipatia kwa njia zisizo halali na waape kuwa kuanzia sasa watakuwa waaminifu kwa serikali na kwa umma wa watanzania.

Ninacho kiona sasa ni kwamba wafanyakazi wa serikali wakiambiwa mheshimiwa Rais atatembelea sehemu fulani ghafla amani inatoweka na ujio wake unaonekana kama ni nuksi fulani.Ziara za Waziri mkuu na mawaziri siku hizi hazichukuliwi tena kama ni neema fulani au bahati kutembelewa na kiongozi wa juu serikalini, bali watu waanaanza kujiuliza ni nani zamu yake ya kutumbuliwa inafuata.Katika mazingira haya serikalini hakuwezi kuwa na tija zaidi ya hofu na amani kutoweka.

Kwa mkutadha huo ndio maana napendekeza kuundwe tume ya maridhiano ipitie ripoti za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, ibaini wote walio tuhumiwa kufuja mali za serikali kisha uwekwe utaratibu wa namna ya kurudisha au kulipa.fukuzafukuza ni nzuri kwa kuwa inaleta aina fulani ya nidhamu kazini lakini pia inaua uwajibikaji na ubunifu.wengine wamesha anza kusema aaa serikali haina shukrani hata mtu ukiwa hujawahi kuandikiwa onyo akija mwanasias kosa dogo kazi huna! huo siyo mwelekeo mzuri katika kulijenga Taifa.
 
Back
Top Bottom