Ni wakati sasa vyama vya kitaaluma kusaidia kuikomboa nchi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
katika historia yetu tunaambiwa vyama vya wafanyakazi vilishiriki sana katika kuikomboa nchi yetu kutoka katika utawala wa ukoloni.

ipo dhana miongoni mwetu tulio wengi kudhani kuikomboa nchi ni jambo la wakati mmoja tu ambalo ilikuwa ni kuwaondoa wakoloni.

kiuhalisia kuikomboa nchi ni jambo endelevu kama ilivyo kulinda afya ya mwanadamu. yapo mambo mengi ambayo yanatishia uhuru wa mwanadamu ikiwemo ujinga na umasikini na haya hubadilika kulingana na wakati. hivyo mwanadamu hutakiwa daima kuwa katika mapambano ya kujikomboa.

changamoto ni nyingi na kwa bahati mbaya sana siasa pekee kwa sasa zinaonekana kutokudhi mahitaji yote ya wananchi katika kujikomboa.

ni wakati sasa vyama vya kitaaluma kurudi katika kutoa mchango katika mapambano ya nchi yetu.

kwa nini hatuoni umoja wa wakulima kwa sasa kuangalia si kwa mantiki ya kuandaa migomo ya wakulima bali kuangalia changamoto za wakulima kwa kutumia utaalamu na uzoefu wao na kushauri serikali ni kitu gani iwafanyie kuboresha sekita yao.

ni kwa nini hatuoni chama cha wahandisi ambacho si kile kinachotekeleza maagizo ya serikali bali umoja ulioundwa kuwaunganisha wao kama wao na kukaa pamoja kujadili changamoto ambazo wanakabiliana nazo na kushauri serikali ni njia ipi inaweza kufanya taaluma yao kuwa na tija kwa nchi.

wapo wanataaluma ambao wao wameunda vyama vyao kama madaktari, walimu, wanasheria, wafanya biashara lakini ni kwa bahati mbaya sana makundi haya tunayasikia katika kudai nyogenza za mishahara, kupinga kodi tu,

tunatamani makundi haya kutambua kuwa zipo changamoto nyingi ambazo yawezekana serikali ikizitatua taaluma zao zinaweza kutoa tija kubwa katika ujenzi wa nchi.

kila taaluma ikiunda kikundi cha kuwaunganisha wanataaluma na kukaa kujadili kwanza kutambua wajibu wao katika jamii, wajibu wao katika kuiwezesha serikali kupitia kodi na utendaji wa kitaalamu, kutambua wajibu wa serikali kwao katika kuwawezesha kutumia uwezo uliopo.

kwa mtindo huu wanataaluma watatoa msukumo mpya katika kuibadilisha jamii yetu kupiga hatua za kimaendeleo.

hii itasaidia pia kutatua tatizo la elimu katika jamii yetu linaloonekana kuwa katika mifumo ya elimu zilizo rasmi lakini uchunguzi wa kina ukionyesha tatizo kubwa ni elimu ambazo haziko katika mifumo rasmi kwa wanataaluma kushindwa kulink taaluma zao na jamii zao na hivyo kutotoa mchango wao ipasavyo.

ni rahisi sana leo hii taaluma moja kuleta madai ya ambayo kiuhalisia hayaendani na kipato cha jamii kwa wakati huo bali yanachukuliwa kutoka katika jamii zilizopiga hatua zaidi. ni rahisi sana wanataaluma kubaki kujenga matumaini juu ya majibu mepesi yasiyotatua hoja zao kutokana na kutokuwepo mfumo wa wao kukaa kuchambua changamoto zao na kuzielewa na kupima uwezekano wa utatuzi.

kama hakuna anayewafanyia haya nyinyi basi yafanyeni wenyewe, lakini pia mkiunda umoja wenu kwa mantiki hiyo mnarahisisha vyombo vyenye wajibu kuwasilikiza na kuwaelimisha.

mkiunda makundi yenu mkazijua changamoto zenu kwa undani mtaondoa bla bla katika siasa kwani wale wataokuja kuwaahidi itabidi wafanye kazi za ziada kuzijua changamoto zenu na suluhisho zake.
 
Elimu yako ya mara ya mwisho kukaa darasani
Ilikukomboa kifikra mkuu.

Wasomi wetu wa karne hii ni wepesi mno kutawaliwa kwa kutumia tende na halua.

Ni tofauti kabisa na enzi za kina Mwanamtwa Mkwawa na Mirambo na wengine ambao elimu zao zilikua ni ndogo sana sana.

Ukitegemea wasomi wakuletee mabadiliko ya kisiasa itakua ni ndoto ya alinacha.

Sijawahi kuona SACCOS ya Maprofesa na Madokta. Lakini ukiwakuta kwenye makaratasi wanasifia SACCOS kuwa ni mkombozi wa jamii.

Wakulimi na wajasiriamali wadogo sana wanaweza kuhamasishwa na kuunda SACCOS kwa nia njema kabisa lakini wanakuja kufilisiwa na wasomi pale wanapowaajiri kama wafanyakazi wa kuiendeleza na kuisimamia. Unakuta mhasibu na mwanasheria wa SACCOS ya wakulima ambaye hajawekeza hata senti tano zaidi ya kuaminuwa kwa sababu ya elimu yake lakini anataka anufaike ndani ya mwaka mmoja na kuwaacha wakulima wakiendelea kusota na umasikini wao huku akiibia na kuiua SACCOS.
Hawa ndio wasomi wa leo wakiojaa ubinafsi na unafiki. Kamwe hawatakuja kuwa na chama cha kuwakomboa wanyonge zaidi ya kujikomboa wao na matumbo yao kuyajaza vimiminika vyenye kilevi kila siku na kulala wakiwa wamelewa chakari mana hawataki kufikiri wala kuwaza tena baada ya kusoma.
Hawa ni rahisi mno kuwatawala kwa mfumo wowote ule anaotaka mwanasiasa aliyeko madarakani alimradi wahidiwe vyeo tu. Ukishamuahidi msomi cheo basi elimu yake yote inaishia hapo!
 
nadhani lipo tatizo ambalo lazima linasababisha hayo uliyoyasema na sio elimu ya watu.

mfumo wa maisha tuliokuwa nao katika jamii ni tatizo kubwa!

kufuata utaalamu au kutumia elimu ilikuwa ni njia isiyo na tija au isiyo na efficiency. tuliweka mazingira katika jamii yetu ya watu kupata maisha mazuri kwa kupata mapato halamu na njia za watu kupata mapato halali tuliweka vikwazo vingi.

mfano wafanyakazi wa bandarini walisifika sana na kila mtu alitamani kufanya kazi bandarini je ilikuwa ni kutokana na mishahara wanayolipwa? wafanyakazi TRA walikuwa matajiri sana je ilitokana na kutumia utaalamu au kupata mianya ya kukwepesha kodi?

lakini uniambie ni kitu gani ambacho mtu angefanya kwenye jamii kwa kutumia utaalamu na akawa na maisha mazuri? kama ni ajira nzuri zilienda kwa kujuana, kama ni kandarasi zilitolewa kwa rushwa au kujuana vigogo wanatoa kwa familia zao na marafiki zao.

kwa trend kama hiyo nani angeshikilia utaalamu kama sio kila mwana jamii kutafuta mwanya wa wapi na yeye aweke mrija wake kunyonya ili atoke kimaisha?

lakini lazima tukubali kuwa wasomi lazima waone aibu pale wanaposhindwa kutumia usomi wao kuielekeza jamii katika kufanya mambo sahihi na wao wakaanza kuacha utaalamu wao na kuingia kwenye ujanja.

pengine wanaweza kujitetea kuwa mambo haya waliyakuta na ilikuwa vigumu kwa sababu walikwisha tawanywa na kutawaliwa na mfumo huo wa maisha.

rai yangu kwa wasomi ni wakati ndio huu. serikali ya awamu ya tano inaonyesha nia ya kuvunja mitandao hii na kuirudisha jamii katika kutumia utaalamu na uchapakazi ili mtu afanikiwe kimaisha.

watawala wa sasa wamefanya sehemu yao ambayo ni "more than enough"

lakini hatuwezi kuwaachia wanasiasa peke yao wafanye jitihada hizi maana yawezekana wakayaona matatizo yetu kwa macho ya kisiasa lakini sisi tulio katika sekita zetu tunaona kwa undani yanayotendeka. tunajua kabisa kuwa hapa kama tungefanyiwa hili tungefanikisha hili, tunajua kuwa kuna mambo ni ya msingi inawezekana hayajapewa kiupambele.

ni wakati sasa tuanze harakati za kuzifanya taaluma zetu kuwa na tija kwa kukaa sisi wenyewe tukajadili matatizo yetu na kuishauri serikali ni kitu gani itufanyie. tukae pamoja tuwe na uelewa mpana na dira ya pamoja na sio huyu akiibuka huku ana madai yake na huyu akiibuka huku ana madai yake ambayo kila mmoja anatoa ushauri kwa muono wake ambao unaweza usiwe wa tija kwa sasa.

lakini tukikaa pamoja katika taaluma zetu tutachambua hoja zetu kwa vipaumbele kwa kuzikilizana sote na hoja zetu zinakuwa ni hizo hizo.

tukikaa pamoja inaweza kuwa njia rahisi ya kuwezesha serikali kuzisapoti taaluma zote kwa nguvu ileile kwa wakati wote kwa kupima madai yao, kupima uwezo uliopo na kurudisha mrejesho kwao ambao hawabaki kulalamika na kukata tamaa ya kazi kuwa sisi hatusikilizwi bali kuona serikali au wadau wengine wamefanya kadiri ya uwezo wao na kadiri tunavyofanya kazi zaidi ndivyo tutajenga uwezo zaidi na kufanikisha tunayoyataka.

Back
Top Bottom