Ni wakati sasa Twaha Kiduku azichape na Mwakinyo

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,439
12,294
Au mnasemaje wadau?

kiduku-pic-data.jpg
Mwakinyo.jpg

====

9 Sep 2020
Bondia namba mbili kwa ubora Tanzania Twaha Kiduku amesisitiza kuhitaji pambano na Hassan Mwakinyo ili afahamike nani bingwa wa nchi.

Kauli hii aliitoa wiki mbili zilizopita ameirudia tena siku ya jumatano alipokuwa anafanya mahojiano na moja ya kituo cha Radio hapa nchini.

Kiduku ametoka kumchapa kwa pointi Abadallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ katika pambano la raundi kumi.

Baada ya ushindi huo amepaa hadi nafasi ya pili na anahitaji kutawazwa kuwa namba moja endapo atacheza na Mwakinyo na akishinda.

Kiduku ambaye ameweka wazi kuwa hana uongozi unaomsimamia anawakaribisha watu wanaopenda kumsapoti katika kazi zake.

“Sina meneja wa wakala kwa sasa hvyo kama mtu akihitaji kunipa sapoti namkaribisha,” alisema.

Bondia huyo kutoka Morogoro aliye na miaka 28 moja ya hazina mahususi katika ngumi za Tanzania.

Ni bondia ambaye anathamini utu pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika kazi yake.

Huenda imani yake ya kumuogopa Mungu ndio inayompa hofu ya kuto mdharau mtu yoyote.

Huenda kila mmoja anamtazamo wake kwa Kiduku kwa jicho lake na vile anavyoona ila kwa anayetaka kuwekeza hiki ndicho kipindi sahihi kwake.

Makampuni mbalimbali pamoja na bidhaa za vinywaji hasa zile za ‘Energy’ hamuoni kitu kwa Kiduku.

Ni bondia ambaye anamuonekano wa kimatangazo kama watu wakiamua kumpa mashavu hayo.

Pia wakala hii ndio sehemu ambayo mnaweza kupiga pesa kipindi ambacho yuko na uwezo wa hali ya juu.

Mtafutie mapambano makubwa atengeneze hela ndefu na nyie mnakuwa na kiasi chenu.

Uwezo aliouonesha na heshima aliyoiweka kama kweli mtu anahitaji kuwekeza Kiduku ni sehemu sahihi kwa upande wa ngumi za kulipwa.

Kugoma kwa Mwakinyo kucheza naye ni lengo la kibiashara baina yao wawili na wanatakiwa watengeneze hela kweli.

Nimeshangaa kusikia kuwa hela nyingi mtu anaweza kupokea kwa pambano lenye hadhi kama la Mbabe na Kiduku shilingi milioni sita.

Maneno hayo aliyatoa Mwakinyo alipokuwa anamjibu Kiduku juu ya kupigana naye.

Na Kiduku katika mahojiano alisema kuwa kuna pambano moja dhidi ya Mada Maugo alipata hela kuliko hili la Dulla Mbabe aliloshinda hii ina maana alipata chini ya milioni nne.

Kwakuwa yeye ndio kalitaka pambano wakala wanatumia mwanya huo kuwanyonya mabondia.

Hii ni sehemu nyingine ambayo inatakiwa iangaliwe kwa mapana yake, ngumi za Tanzania zina mambo mengi sana ni vizuri kuangalia namna ya kuwasaidia ndugu zetu ili wafike mbali.

Ushabiki upo tangu zamani mfano mimi niliwahi kuwa shabiki wa Mike Tyson mwingine alimshabikia Lenox Lewis lakini haibadilishi kuwa unapotaka kuusogeza mbele mchezo umbane mmoja mwingine apande.

Hivyo ukiniamsha usingizini ukiniuliza mabondia saba bora Tanzania kwa sasa basi sitosita kuwataja , Twaha Kiduku, Hassan Mwakinyo, Dulla Mbabe, Mfaume Mfaume, Tony Rashid, Ibrahim Classic na Cosmas Cheka.

Sasa hawa watu tuwafanye bidhaa zitakazo leta heshima ya ndondi Tanzania.

Tuwainue kwa pamoja na kila aliyebora kwa kiwango chake basi anyanyuliwe kwa kiwango chake.

Kwa upande wangu naamini kabisa Twaha Kiduku, Dulla Mbabe na Hassan Mwakinyo wakipata watu sahihi watafika mbali sana.

Nakumbuka katika pambano la utangulizi baina ya Twaha kiduku na Msauzi Afrika France Ramabolu alimtandika kwa ‘TKO’ uwezo wake aliounesha pale ndio ikawa mwanzo wa kumtaka Dulla Mbabe.

Lakini uwezo wake haujifichi kabisa hivyo ni wakati wa kumbeba na kuhakikishia mtu ambaye unataka kuwekeza kwake ni kijana msikivu aliye na nidhamu ya hali ya juu sana.

Naamini kabisa mtu akijtokeza kumdhamini au kuwa kama Wakala wake, Twaha atalipaisha taifa mbele.

Rekodi zake katika mitandao zina utata lakini mtua anaweza kunirekebishaa amepigana mapambano 21 ameshinda 15 amepigwa 5 na sare moja jina lake kamili alilopewa na wazazi wake ni Twaha Kassimu Rubaha, amezaliwa mkoani Morogoro ila baba yake Mzaramo.

Amezaliwa 05.01. 1992, Kiduku mmoja ya mabondia wachache Tanzania walio na miili yenye muonekano wa kibondia.

Uwezo wake wakuongea kwa busara pamoja na kuishi vizuri na watu wanaomzunguka ndio sababu ya kupendwa na kila rika.

Anatamani naye siku moja awe bondia mkubwa na atakaye tambulika duniani naamini atafika huko kwa uwezo wa Mungu aliyeumba mbingu na ardhi.

Credit: Amini Nyaungo
 
Twaha awekeze Nguvu yake nje ya nchi Kama anavyofanya Mwakinyo.
Hayo ndio mawazo mazur wengne mawazo yao ajabu kweli mbaka unashangaa wanaubongo kweli.! atafute mapambano ya nje huko ili yampe nafasi zaid yakujitangaza na sio mnang'ang'ana apambane na mwakinyo ninyi ndio mnaowalemaza mabondia tumieni nafasi hiyo kumuhamasisha atafute mapambano zaid ya inje kama anavyofanya mwenzake mwakinyo
 
Mwakinyo hawezikubali, anajua atapoteza alafu atampandisha
KIDUKU
 
Kama ana ubavu huyo twaha akaanze kucheza ndondo za nje ya nchi kwanza hususani ulaya au marekani ndio aje kujilinjganisha na mwakinyo. Mwakinyo safi sana aendelee kujibrand
 
Hayo ndio mawazo mazur wengne mawazo yao ajabu kweli mbaka unashangaa wanaubongo kweli.! atafute mapambano ya nje huko ili yampe nafasi zaid yakujitangaza na sio mnang'ang'ana apambane na mwakinyo ninyi ndio mnaowalemaza mabondia tumieni nafasi hiyo kumuhamasisha atafute mapambano zaid ya inje kama anavyofanya mwenzake mwakinyo
Anaogopa changamoto ya ngumi za mzungu.
 
Nonsence….Uzito wao wa sasa ni tofauti hivyo hauwawezeshi kupigana kwa kutumia kanuni yoyote ya ndondi...Labda wapigane kwa kugombea demu
 
Hayo ndio mawazo mazur wengne mawazo yao ajabu kweli mbaka unashangaa wanaubongo kweli.! atafute mapambano ya nje huko ili yampe nafasi zaid yakujitangaza na sio mnang'ang'ana apambane na mwakinyo ninyi ndio mnaowalemaza mabondia tumieni nafasi hiyo kumuhamasisha atafute mapambano zaid ya inje kama anavyofanya mwenzake mwakinyo
Mkuu, Ina maana watu kutofautiana mitazamo unawaita hawana ubongo?

Mmmmh,hii si kweli.
 
Kama ana ubavu huyo twaha akaanze kucheza ndondo za nje ya nchi kwanza hususani ulaya au marekani ndio aje kujilinjganisha na mwakinyo. Mwakinyo safi sana aendelee kujibrand
Kiduku anataka kutembelea nyota ya mwakinyo , Kama ana uwezo kwann hasiende kupigana nje ya nchi !!!
 
.Tukiacha ushabiki maandazi, kwangu mimi sizani kama mawazo yako yatakuwa sahihi.
Ninachojaribu kusema ni kuwa hao unaowajalibu kuwafananisha ni watu wawili tofauti.
Sawa wote ni mabondia wazuri lakini wamepishana pakubwa. Sijawai kufuatilia sana Michezo ya ngumi ila ninachokifahamu mimi Huyo mwakinyo kwanza ana uzoefu wa kupigana na mabondia tofauti tofauti nchi tofauti tofauti.lakini twaha yeye kila siku nikurudiana na dula. Kingine wako na uzito tofauti labda mmja apunguze uzito au azideshe.
Pia kuna suala la status, kwenye upande wa stutus mwakinyo yuko vizuri zaidi ana mikanda kuliko dula huyu mwakinyo unaemzungumzia kumbuka pia alishwai kuwa bingwa wa afrika kwa uzito wake ndo akaenda kupigana na bingwa wa ulaya na akamchapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom