Ni wakati sasa Rais Magufuli kurudia mchakato wa katiba uliokwamishwa makusudi na CCM

lingamba lidodi

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
965
1,000
Saalam jf!
Mods uacheni Uzi wangu tena msiunganishe na mwingine wowote please. WE DARE TO TALK OPENLY.

Toka mwanzo wa kuingia madarakani Rais magufuli amekuwa akitamka Mara nyingi kuwa,

1. Mtetezi wa wanyonge na mlinzi wa raslimali za watanzania.

2 Tanzania ni tajiri,anataka iwe donor country,amedhihirisha hilo kwa Malawi.

3, Anainyoosha nchi kwa kupambana na mafisadi,amedhihirisha hilo kwa kuunda mahakama ya mafisadi.
Japokuwa tunawaona mafisadi wawili tu wamo korokoroni( Rugemali na Habinga Singh wengine kawaacha wanapeta mitaani na bungeni)

Mpaka sasa tunaweza sema ameshazunguka nchi nzima na kuuona utajiri wa nchi yetu.

Utajiri huo umekuwepo mpaka anauona ni kutokana na busara na hekima za mwl jk Nyerere.

Viwanda anavyofufua ni Umoja wa watanzania wa wakati ule,wakiongozwa JKN.

Waliomtangulia magufuli wamezifanya raslimali za nchi hii zisombwe na mataifa mengine kama haina wenyewe,na hakuna cha kuwafanya,(kuwawajibisha)

Rais amekuwa akilalamikia waliotangulia kuwa wamegawa utajiri wa nchi yetu huku akiwa hana meno ya kuwang'ata.

Kama anavyoamini kuwa anaijenga nchi upya,imempasa kurudi kwenye rasimu ya warioba ili kupata katiba mpya itakayomuwajibisha yeyote atakayeingia madarakani baada yake pindi atajapofanya madudu kwa kutapanya raslimali zetu kama waliotangulia.

Akifanya ivo,nitaamini Mungu alimuandaa kwaajili ya nchi hii.
Aachane na siasa za sisim kiutendaji,sisim wanasema lakini hawatendi.
Sisim ni sawa na Nguruwe, wanazaa watoto,njaa ikumbana anageuka anawala kushibisha tumbo lake

KUENDELEA KUJAZA MAJI KWENYE PIPA WAKATI CHINI LIMETOBOKA ASITAZAMIE KUKUTA MAJI BAADA YAKE
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,322
2,000
Mmmmm!!!! Watu wanaopenda kuabudiwa hasa jiwe zaidi hata ya MUNGU, ni ndoto kujaribu kuruhusu mchakato wa katiba, ambao utampokonya huo ufalme!! Yaani nikubali ile vote.... CAG, nako afike?!! Nikiteua lazima pawe na watu wa kudhibitisha!!, ushindi wangu mtu akaupinge mahakamani?!! Nasemaaa ni ngumuuu mnooo!!!!
 

Pelle mza

JF-Expert Member
May 15, 2008
3,048
2,000
Katiba tuliyonayo kwa sasa inatosha, ngoja tuendelee kutoa ELIMU ya uzalendo!
 

Kizzy Wizzy

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
3,210
2,000
Kulingana na maelezo yako unataka aanze kudili na katiba mpya,

Ndani ya katiba mpya unataka wapitishe utaratibu Rais awe anashtakiwa right?
Tangu lini ukaona mtu ananoa panga ambalo litaweza kumkata mwenyewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom