Ni wakati sasa kumfichua anayemtuma Musiba kuleta taharuki

Taharuki katika jamii ni jambo lenye kuchukuliwa kwa hadhari kubwa sana.
Tumeona zipo habari za taharuki ambazo huwa zinaweza kuleta hata mtikisiko wa kiuchumi, mfano kushuka ghafla au kupanda kwa masoko ya hisa au wawekezaji kukimbia au kukimbiza mitaji..
Tumeshuhudia huyu mtu (ambaye ukimuangalia kwa umakini ana tatizo kisaikolojia) akija na tuhuma kedekede kwa watu mbalimbali na ambao wanaheshimika katika jamii, lakini la kusikitisha ni kuwa hachukuliwi hatua yeyote hata ya kuonywa tuu. Jee yeye ni nani? Au yeye anatumwa na nani?
Jana magazeti yake yametoa taarifa kuwa kuna watu wanataka kumuua, Polisi wakasoma magazeti hao mbio kuwahoji waliotajwa kama vile hizo tuhuma zimekuwa FILED kwao. Nani tumepata kuona anapewa huduma hii first class na jeshi letu la polisi? Lazima kuna mtu mzito ambaye yeye ndiye "Musiba" na huyu mropokaji ni photocopy tuu, jee ni nani huyo anayeogopwa na wahusika wa tasnia hizo za habari na wa usalama?
Maana sio Dr Abass au Mwakyembe anaye furukuta, na wala sio Kamanda Sirro au Kangi mwenye kuweza kukohoa kwa Musiba.
Tuwe sasa wakweli, ni nani huyo ndio mwamvuli wa Musiba? Ndiye backup yake kiasi cha kujiaibisha kwa kuonyesha kazi hawawezi?
Ukiona polisi wanamuita Max ahojiwe kwa tuhuma nzito kama hizo kisha wanamuachia bila masharti ujue tuhuma hizo ni baseless na zimedharaulika lakini wao wametaka kumuonyesha huyo wamuogopaye kuwa wamechukua hatua.
NI NANI HUYO TUMFICHUE?
Mbona anajulikana kuwa ni yule boss anayejua sana chingeleza na ana Phd fake
 
Wabongo bwana,
yeye mwenyewe alisha tamka wazi kwamba anamtetea yule wa pale ufukweni mwenye nguvu kuliko wote kikatiba. Cha ajabu kwa nguvu aliyonayo yule wa ufukweni bado haja mkemea huyu musiba.... Sasa unadhani anaye mtuma musiba kuleta misiba kwenye jamii ni nani?
Anajulikana ila ni mmoja ya wale ambao hatuwajui.
 
Majasusi siku ZOTE wanatengeneza scenario ya kumalizana na chambo. Huyu Musiba hajitambui atafaidi sana kutumia na majasusi lakini mwisho wake ni hatari tupu kwake. Sijui ni vipi hawezi kuwasoma hao wanaomtuma?
 
Taharuki katika jamii ni jambo lenye kuchukuliwa kwa hadhari kubwa sana.
Tumeona zipo habari za taharuki ambazo huwa zinaweza kuleta hata mtikisiko wa kiuchumi, mfano kushuka ghafla au kupanda kwa masoko ya hisa au wawekezaji kukimbia au kukimbiza mitaji..
Tumeshuhudia huyu mtu (ambaye ukimuangalia kwa umakini ana tatizo kisaikolojia) akija na tuhuma kedekede kwa watu mbalimbali na ambao wanaheshimika katika jamii, lakini la kusikitisha ni kuwa hachukuliwi hatua yeyote hata ya kuonywa tuu. Jee yeye ni nani? Au yeye anatumwa na nani?
Jana magazeti yake yametoa taarifa kuwa kuna watu wanataka kumuua, Polisi wakasoma magazeti hao mbio kuwahoji waliotajwa kama vile hizo tuhuma zimekuwa FILED kwao. Nani tumepata kuona anapewa huduma hii first class na jeshi letu la polisi? Lazima kuna mtu mzito ambaye yeye ndiye "Musiba" na huyu mropokaji ni photocopy tuu, jee ni nani huyo anayeogopwa na wahusika wa tasnia hizo za habari na wa usalama?
Maana sio Dr Abass au Mwakyembe anaye furukuta, na wala sio Kamanda Sirro au Kangi mwenye kuweza kukohoa kwa Musiba.
Tuwe sasa wakweli, ni nani huyo ndio mwamvuli wa Musiba? Ndiye backup yake kiasi cha kujiaibisha kwa kuonyesha kazi hawawezi?
Ukiona polisi wanamuita Max ahojiwe kwa tuhuma nzito kama hizo kisha wanamuachia bila masharti ujue tuhuma hizo ni baseless na zimedharaulika lakini wao wametaka kumuonyesha huyo wamuogopaye kuwa wamechukua hatua.
NI NANI HUYO TUMFICHUE?

Wewe tatizo lako ni lipi hasa? Musiba anacho kisema kina mantiki sana sio kwamba anakurupuka tu - nyie watu baki mnaojifanya kukwazwa na uwazi wa Musiba basi you are obviously an ardent supporter of the gang hell bent to unseat JPM by throwing a monkey spanner in his bid for a second term in office - hamtafanikiwa.
 
Wako Watatu tu wa Kwanza yupo Jirani na Mahakama ya Samaki Jijini Dar es Salaam Kikazi na Kimakazi, wa Pili yupo Masaki anaishi karibu na Hotel ya Sea Cliff japo Kikazi hayuko mbali na Shule ya Ilala Boma na Soko la Ilala Karume na wa mwisho ( wa Tatu ) ana Kazi za aina mbili ya Kimedani na ya Kiuchungaji na muda wake mwingi wa Utumishi upo Oysterbay mkabala na Shule ya Chekechea ya Mtakatifu Peter. Nimeshangaa sana wanavyohangaika na Watu kama akina Maxence Melo ambao ukipima na Kuchunguza Kiumakini hawahusiki na hizo Tuhuma zao za Kiduduna ( Kipumbavu ) kabisa dhidi yao.
Maxine ni njia tu ya juicing a JF
 
Wewe tatizo lako ni lipi hasa? Musiba anacho kisema kina mantiki sana sio kwamba anakurupuka tu - nyie watu baki mnaojifanya kukwazwa na uwazi wa Musiba basi you are obviously an ardent supporter of the gang hell bent to unseat JPM by throwing a monkey spanner in his bid for a second term in office - hamtafanikiwa.
Mtu yeyote Mwoga na asiyejiamini ndio anaweza kumtumia Musiba kama propagation man wake.
Musiba ni kichaa hivyo lazima amtumiaye hana ujasiri wa kuruhusu ukweli uwe wazi
 
Hili limekuja kututoa kwenye maada ya mwandishi Azory Gwanda. Najaribu kuwaza tu
 
Nakumbuka Siku za nyuma vikao vya ccm vilikuwa vinaweza kumhoji yeyote mwenye kadi ya chama. Nasema YEYOTE yule kama alikuwa anakwenda kinyume na Sera na desturi za chama hicho.
Jee jeuri hiyo imepotelea wapi?
Mmiliki Wa kigoda unamuonaje kwani?
 
Mtu yeyote Mwoga na asiyejiamini ndio anaweza kumtumia Musiba kama propagation man wake.
Musiba ni kichaa hivyo lazima amtumiaye hana ujasiri wa kuruhusu ukweli uwe wazi
Msifikiri tumezaliwa jana, haya mambo ya kutaka kuwania Urais come rain or shine utatufikisha wapi kama Taifa? Au mnafikiri yaliyo tokea Liberia na sasa Sudani Kasikazini ni vigumu kutokea hapa kwetu? Hatutaki vurungu za kijinga - mtu mmoja anakuwa nogwa kwa nini, ana kitu gani cha kujivunia mbona wakati wote alipo kuwa Waziri wa Wizara nyeti ambayo ndio ingekuwa msitari wa mbele kuleta wawekezaji wa kujenga viwanda na miundo mbinu , ingawa alikuwa na fursa ya kutekeleza hayo hakufanya hivyo badala yake aliishia ku-rove Dunia kama Ferdinand Magellan au James Cooke licha ya kudumu Wizarani zaidi ya miaka kumi.

Sasa jaribu kulinganisha uwajibikaji ulio tukuka wa JPM na huyo jamaa utashangaa anapata wapi ujasiri wa kutaka kuwania higher office let what comes may!!

Back to main point, JPM ameongoza Taifa letu kwa miaka karibu minne lakini ndani ya kipindi hicho kifupi ameanzisha mega projects nyingi tu ambazo zimeiletea Taifa letu heshima Kimataifa, ubunifu wa JPM na udhubutu wake umekuwa mfano wa kuigwa Africa Nzima, hao ndio Viongozi wanao takiwa ndani ya Bara la Afrika.
 
Msifikiri tumezaliwa jana, haya mambo ya kutaka kuwania Urais come rain or shine utatufikisha wapi kama Taifa? Au mnafikiri yaliyo tokea Liberia na sasa Sudani Kasikazini ni vigumu kutokea hapa kwetu? Hatutaki vurungu za kijinga - mtu mmoja anakuwa nogwa kwa nini, ana kitu gani cha kujivunia wajkati wote alipo kuwa Waziri wa wizara nyeti ambayo ndio ingekuwa msitali wa mbele kuleta wawekezaji wa kujenga viwanda na miundo mbinu, amekaa pale zaidi ya miaka kumi - JPM ameongoza Taifa lakini ndani ya miaka minne amefanya maajabu na umekuwa mfano wa kuigwa Africa Nzima.
Mfano wa kuigwa Africa nzima? Taja hizo nchi zilizoiga mfano wa haya yanayotokea nchini kwetu ndani ya hii miaka 4!
Msipende kudanganyika kwa propaganda za kishamba shamba!
 
Back
Top Bottom