Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,797
- 71,216
Taharuki katika jamii ni jambo lenye kuchukuliwa kwa hadhari kubwa sana.
Tumeona zipo habari za taharuki ambazo huwa zinaweza kuleta hata mtikisiko wa kiuchumi, mfano kushuka ghafla au kupanda kwa masoko ya hisa au wawekezaji kukimbia au kukimbiza mitaji.
Tumeshuhudia huyu mtu (ambaye ukimuangalia kwa umakini ana tatizo kisaikolojia) akija na tuhuma kedekede kwa watu mbalimbali na ambao wanaheshimika katika jamii, lakini la kusikitisha ni kuwa hachukuliwi hatua yeyote hata ya kuonywa tuu. Jee yeye ni nani? Au yeye anatumwa na nani?
Jana magazeti yake yametoa taarifa kuwa kuna watu wanataka kumuua, Polisi wakasoma magazeti hao mbio kuwahoji waliotajwa kama vile hizo tuhuma zimekuwa FILED kwao.
Nani tumepata kuona anapewa huduma hii first class na jeshi letu la polisi? Lazima kuna mtu mzito ambaye yeye ndiye "Musiba" na huyu mropokaji ni photocopy tuu, jee ni nani huyo anayeogopwa na wahusika wa tasnia hizo za habari na wa usalama?
Maana sio Dr Abass au Mwakyembe anaye furukuta, na wala sio Kamanda Sirro au Kangi mwenye kuweza kukohoa kwa Musiba.
Tuwe sasa wakweli, ni nani huyo ndio mwamvuli wa Musiba? Ndiye backup yake kiasi cha kujiaibisha kwa kuonyesha kazi hawawezi?
Ukiona polisi wanamuita Max ahojiwe kwa tuhuma nzito kama hizo kisha wanamuachia bila masharti ujue tuhuma hizo ni baseless na zimedharaulika lakini wao wametaka kumuonyesha huyo wamuogopaye kuwa wamechukua hatua.
NI NANI HUYO TUMFICHUE?