Ni wakati sasa jiji la Dar likafunga kamera za barabarani

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Ni aibu kwamba mji kama Dar, mji wa kibiashara hauna kabisa kamera za barabarani kwa ajili ya security surveillance.

Zanzibar mitaa mingi ina kamera, Nairobi mitaa mingi ina kamera.

■ Hata watalii wanajali sana usalama wao, kuwepo camera kutaongeza trust kwa tourists.

■ Wizi wa magari na mali nyingine kamera zitatoa majibu.

■ Uharibifu wa miundombinu kamera zitajibu hasa usiku.

■ Jinai kama mauaji, ubakaji nk kamera zitajibu.

■ Takwimu za idadi ya magari nk kamera zitasovu

Kwanini kamera haziwekwi?

Vitu vingine to be true ni vidogo sana, na ni aibu kwamba tunashindwa kuviweka Zanzibar tu hapo wana street cameras tangu 90s Dar na miji mingine nini kinakwaza kufunga hii teknolojia. Ifike pahala tuwaambie hawa Madiwani hatuwapi kura mpaka waje na mipango ya usalama kama huu na kufunga street lights etc.

Tumeona juzi jinsi zilivosaidia kupata details za ajali ya basi Moshi mjini, zikiwa zimefungwa na mtu binafsi aliejitolea tu! Pitisheni bajeti huko kamera zifungwe.

Mheshimiwa Rais tunaomba hili umuelekeze Waziri wa Mambo ya Ndani na wa Miundombinu walihakikishe linakamilika, tunakuamini kwenye uboreshaji miundombinu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi hiyo fedha ya kununualia kamera wangeiwekeza kwanza kwenye Jeshi la Polisi, mambo kama kuwalipa mishahara inayotosha kukidhi mahitaji, vifaa vya kufanyia kazi kuanzia sare mpaka magari na training ingesaidia zaidi kuliko kamera, usitoshe kama Nairobi wana kamera mbona uhalifu huko ni zaidi ya Dar ambako hakuna kamera?
 
Camera ni nyenzo itawasaidia hao polisi sana zaidi ya mishahara kuongezwa ....mtoa mada big up umegusa mambo yote sioni la kuongezea

Ni kweli kamera ni nyenzo lkn shida yenu ni ubinafsi mnataka kuwa salama muishi vizuri lkn yule mnayemtaka awaweke salama hamtaki na yeye aishi vizuri, Polisi wetu hata sare na viatu vya kazi hawana za kutosha wengine wanaweka viraka, magari ya kazi hayatoshi na yaliyopo hela ya mafuta na kununua matairi mapya hamna lkn unataka Serikali itumie Mabilioni kufunga Kamera Mitaani kwa ajili yako?
Tanzania nyumba yako ikivamiwa hata Polisi hawawezi kuja hawana mafuta, ...
 
Nakuunga mkono. Kamera ni nyenzo kwa hao polisi. Itapunguza usumbufu kwa maafisa upelelezi na kufupisha muda wa mashauri mahakamani na vituoni. Na itawasaidia hao polisi kutekeleza majukumu yao...alichosema huyu ni kwamba magari sare vipo already lakini street kamera hazipo kabisa

Mfano ni taa za barabarani zimepunguza matukio ya ukabaji hasa Sam Nujoma road.

Sasa kamera zitakuwa nyenzo kwa haohao polisi. They need to be acquainted with latest crime detterance technologies,CCTV ni moja ya hizo.
Camera ni nyenzo itawasaidia hao polisi sana zaidi ya mishahara kuongezwa ....mtoa mada big up umegusa mambo yote sioni la kuongezea

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kamera ni nyenzo lkn shida yenu ni ubinafsi mnataka kuwa salama muishi vizuri lkn yule mnayemtaka awaweke salama hamtaki na yeye aishi vizuri, Polisi wetu hata sare na viatu vya kazi hawana za kutosha wengine wanaweka viraka, magari ya kazi hayatoshi na yaliyopo hela ya mafuta na kununua matairi mapya hamna lkn unataka Serikali itumie Mabilioni kufunga Kamera Mitaani kwa ajili yako?
Tanzania nyumba yako ikivamiwa hata Polisi hawawezi kuja hawana mafuta, ...
Mkuu iv ulichoandika umekielewa kweli?

Yaan walipa kodi wanakamuliwa mpaka wanakua wakavu zaidi ya kapi za alizeti bado unasema sijui nani hawana sare

Mtu anaamishia kila kitu kwake huku akiweka mbele ubaguzi wa kanda alafu bado huogopi kuongea upupu?

Uliambiwa tembea kifua mbele nchi ila pesa alafu bado unajitia upumbavu?

Yaan ww ni wale watu wanaomiliki magodaun ya nafaka alafu nyumban0 watoto wanakula mlo mmoja kwa siku tena kwa tabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada barabara ýa Uhuru kuanzia Kariakoo ilipokuwepo round about ya zamani hadi Buguruni sheli hakuna mataa yanayowaka ya barabarani
 
Sio aibu tu bali inaonyesha hawajali raia na usalama wao
Duniani nchi inayoongoza kwa cctv ni China ambayo ina camera 170m
Kwa haraka maana yake kila camera moja kwa watu 12
UK wanazo camera 6m na London tu zipo camera Laki 5
Hii inasaidia sana kuzuia na kuwajua wahalifu
Ni mda sasa Mkuu wa mkoa kuzitafuta hizo camera na kufunga

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ni kweli kamera ni nyenzo lkn shida yenu ni ubinafsi mnataka kuwa salama muishi vizuri lkn yule mnayemtaka awaweke salama hamtaki na yeye aishi vizuri, Polisi wetu hata sare na viatu vya kazi hawana za kutosha wengine wanaweka viraka, magari ya kazi hayatoshi na yaliyopo hela ya mafuta na kununua matairi mapya hamna lkn unataka Serikali itumie Mabilioni kufunga Kamera Mitaani kwa ajili yako?
Tanzania nyumba yako ikivamiwa hata Polisi hawawezi kuja hawana mafuta, ...

Hatutaki sasa kwani lazima tunataka camera,, mbona unashupalia hivyo
 
Mambo mengine akiwaagiza wasaidizi wake wanatekeleza...kwa mfano aliwagiza wafunge kamera daraja la Mfugale Buguruni in a few days wakawa wamefunga ....sasa akiwapiga order waheshimiwa wahusika kwenye kabineti si miji yote itafungwa kamera na tutakuwa na miji salama sana. Wahalifu sasa hivi wana take advantage kwa kutokuwepo surveillance cameras mitaani. Mtu anagongwa rungu la oblangata anadedi muuaji anatokomea na bodaboda...sasa kamera ingekuwepo angalau ingekuwa rahisi kumbaini
N'yadikwa,

Camera tu unamwomba Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kila siku tunasikia mara watoto wamepotea, au wameibiwa kamera ni muhimu kwanza itaongeza mapato ya serikali kupitia hizi gari zinazovunja sheria za usalama barabarani na wakati huohuo kuzuia uhalifu ni aibu kubwa kwa jiji kama Dr es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha kukosa kamera
 
Kabisa zitakuwa fursa ya kuongeza mapato hasa kwa matukio ya traffic cases nyakati za usiku
kila siku tunasikia mara watoto wamepotea, au wameibiwa kamera ni muhimu kwanza itaongeza mapato ya serikali kupitia hizi gari zinazovunja sheria za usalama barabarani na wakati huohuo kuzuia uhalifu ni aibu kubwa kwa jiji kama Dr es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha kukosa kamera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi hiyo fedha ya kununualia kamera wangeiwekeza kwanza kwenye Jeshi la Polisi, mambo kama kuwalipa mishahara inayotosha kukidhi mahitaji, vifaa vya kufanyia kazi kuanzia sare mpaka magari na training ingesaidia zaidi kuliko kamera, usitoshe kama Nairobi wana kamera mbona uhalifu huko ni zaidi ya Dar ambako hakuna kamera?
Magari tena zaidi ya waliyonayo nguo si wana mpya wameshonewa kwa kamera ni muhimu hawa wahuni wa dar wanatutia sana hasara kwenye miundo mbinu yetu mfano halisi barabara ya mwendo kasi wanavunja mpaka alama za vivuko wapate nondo mifuniko yooote ya jiji wameiba nyambafu kabisa ndio maana hata daraja la jangwani limesuswa mijitu hatuna hata uchungu na kidogo tulichonacho inakera sana kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kamera ni nyenzo lkn shida yenu ni ubinafsi mnataka kuwa salama muishi vizuri lkn yule mnayemtaka awaweke salama hamtaki na yeye aishi vizuri, Polisi wetu hata sare na viatu vya kazi hawana za kutosha wengine wanaweka viraka, magari ya kazi hayatoshi na yaliyopo hela ya mafuta na kununua matairi mapya hamna lkn unataka Serikali itumie Mabilioni kufunga Kamera Mitaani kwa ajili yako?
Tanzania nyumba yako ikivamiwa hata Polisi hawawezi kuja hawana mafuta, ...
Sikatai kuhuusu mazingira yao duni ukizingatia kazi yao ni ngumu sana na mishahara midogo ila kiukweli mshahara hata uongezwaje hauridhishi (haimanishi kwamba wasiongezwe) juzi kati mhe raisi alisema kwnye nyumba zao wanazojengewa wasilipe kodi (sijui ni kweli au siasa) ila vitu vingi wamesaidiwa kupunguziwa ugumu wa maisha .....kilichobakia ni kuongeza ufanisi wa kazi ambao mshahara wala uniform mpya hazitafanya hivyo ila nyenzo za teknolojia mfano kesi ndogo za uwizi wa simu sikuizi zinaogopwa sababu ya kuwepo kwa tcra mifano midogo just imagine camera zikiwepo je ukabaji, vurugu ndogo ,ukusanyaji wa ushahidi kwa haraka itakuwaje mrahisi mifano midogo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom