Ni wakati sasa CoSoTa na BASATA wakaungana ili iwe rahisi kutetea maslahi ya wasanii nchini

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,528
Wasanii nchini wanaibiwa sana. Kama ifuatavyo: -

1. Wasanii wa muziki kwa mfano pamoja na waandaaji na watunzi wa nyimbo, kwaya na bendi za muziki zinapaswa kupata mgao kutoka kwa vyombo vya habari vinavyocheza nyimbo zao....LAKINI ni bahati mbaya HAWALIPWI; TATIZO kubwa hapa ni kwamba COSOTA haina wafanyakazi kwa sasa ina wafanyakazi kama Kumi na Sita tu wanaohudumia ETI nchi nzima. Hebu tuwe serious kidogo.

2. Wasanii wa muziki wanapoteza fedha nyingi sana kwa nyimbo zao kuuzwa nje ya nchi bila wao kufaidika....udhaifu hapa upo kwa COSOTA ambao bado naamini wanashindwa kufuatilia kwa sababu ya uchache wao;.....ukiingia kwenye sites za kuuza nyimbo kimataifa k.v. SONY,Amazon, nk utaziona nyimbo za akina chidumule, akina Mbaraka Mwinshehe, akina Ulyankulu nakadhalika zinauzwa huko bila wenyewe au familia zao kunufaika.

3. Wasanii wamekuwa hawalipwi mirahaba yao kwa wakati kutoka COSOTA...Tatizo la msingi lipo kwenye uchache wa staff na udogo wa hii society yenyewe;

4. BASATA imeshindwa kuwa organise wananchi kote nchini nayo pia kwa sababu ya udogo wake....HUWEZI niambia kwamba BASATA itawahudumia wasanii wote nchi nzima eti kwa ofisi moja tu iliyopo pale Shariff Shamba!!!;

5. BASATA na COSOTA zinafanya majukumu ambayo kwa namna fulani yanashabihiana hivyo ni muhimu zikaunganishwa kama inavyofaa kwa TBS na TFDA kuwa chombo kimoja....

6. BASATA na COSOTA waonane na WIPO ili ku harmonise sector ya sanaa nchini kwa kuendesha semina za kila mara zinazowakusanya wasanii wote nchini......

WASANII WATHAMINIWE

SASA....Sasa mie natoa maoni kwamba COSOTA na BASATA ziunganishwe na ziongezewe bajeti ili kusimamia maslahi ya wasanii nchini....tatizo ni kwamba vijana wetu wanafanya sanaa kwa upana wake na wanajitahidi mno....lakini hawanufaiki.............tunao:-

- wachonga vinyago
- wahunzi
- wasanii wa muziki (watunzi,maprodyuza nk)
- waigizaji filamu na soap operas
- wasusi
- wachoraji
- nk

hawa wote kama COSOTA na BASATA wataunganishwa na kuongezewa uwezo vijana wetu waliojiajiri kwenye sanaa watapata manufaa sana kwa sanaa........tofauti na ilivyo sasa wakenya wanakuja kununua vinyago wanaenda kuviuza nje huku wasanii waliovichonga wakikosa hata hakimiliki na stahili za sanaa zao....

Hivi leo wasanii wa muziki kwa mfano wana fedha nyingi sana ambazo zimelala kwa wamiliki wa vyombo vya habari vya redio na televisheni.......kwa taarifa yako ni kwamba kila wimbo uliopo kwenye media unapochezwa msanii anatakiwa anufaika kwa kupata share yake.....lakini ni bahati mbaya media hazina leseni ya BASATA wala COSOTA hivyo kuwa vigumu wasanii kupata haki zao. Serikali iingilie kati COSOTA na BASATA viunganishwe na viongezewe uwezo kusimamia kwa uthabiti maslahi ya wasanii nchini Tanzania.

wASALAAM,
N'YADIKWA

WhatsApp Image 2017-06-13 at 14.58.39.jpeg
 
Back
Top Bottom