Ni wakati sahihi wa serikali kufungua shule na vyuo na kuwaacha wananchi wafanye shughuli zao?

Jembekillo

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
4,245
2,000
Habari wanajamvi

Kutokana na maendeleo ya ugonjwa wa Covid-19 kwa upande wa bara kuonesha matokeo mazuri sana kwa sababu tangu tarehe 22 Aprili mwaka huu hakujaripotiwa kisa kipya angalau kimoja cha ugonjwa huu.

Je, ni sahihi sasa Serikali itangaze kufunguliwa kwa shule na vyuo? Pia itangaze sasa watu warejee maisha yao ya kawaida kwa kuchukua tahadhari kiasi za ugonjwa huu maana inaonekana ushauri wa Rais wetu genius wa kujifukiza umezaa matunda.

Mashuleni na vyuoni kuwekwe utaratibu wa kujifukiza kabla ya kuingia darasani pia kwenye daladala konda na dereva wahakikishe wana ndoo ya maji ya moto na mwarobaini ili kuwafukiza abiria.

Pia ni wakati sahihi wa Rais wetu kurudi toka likizo aliyojipa ili awe anajifukiza mwenyewe akiwa ikulu.

#Korona ni kaugonjwa kadogo!
#Tujifukize
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
6,833
2,000
Kwanza hakuna kilichofanyika chenye tija katika kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya hiyo corona,nachokiona ni kuharibu tu utaratibu na kuleta usumbufu kwa baadhi ya mambo hali ya kuwa mambo mengine yako kama yalivyo. Hiyo corona ingekuwa ya kutupiga kama tunavyoona huko ulaya basi hadi sasa tungekuwa tunakufa kama kuku.

Wamewavuruga tu wanafunzi na kuleta usumbufu kwenye usafiri.
 

computerarsenal

JF-Expert Member
Jan 27, 2020
431
500
Kwanza hakuna kilichofanyika chenye tija katika kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya hiyo corona,nachokiona ni kuharibu tu utaratibu na kuleta usumbufu kwa baadhi ya mambo hali ya kuwa mambo mengine yako kama yalivyo. Hiyo corona ingekuwa ya kutupiga kama tunavyoona huko ulaya basi hadi sasa tungekuwa tunakufa kama kuku.

Wamewavuruga tu wanafunzi na kuleta usumbufu kwenye usafiri.
Una uhakika sababu haujafiwa?sijui hata niseme nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Shombe la Kisomali

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
4,048
2,000
Kweli kabisa,, naana ugonjwa haupo sasa, kwann masomo yashindwe kuendelea..?
Fungueni vyuo bhna maisha yaendelee
 

jikafhplgmb

JF-Expert Member
Sep 29, 2018
639
1,000
Afu w2 wanaogoma kufungua sio wanafunzi, Kwa Mikusanyiko ya watoto mitaani bora shule zifungue naunga mkono hoja.
 

Kashaulo

JF-Expert Member
Jun 14, 2019
990
1,000
Kwani tukiacha walimu na taasisi zake za elimu kufungwa, ni nani wengine ambao kazi zao zilisitishwa na serikali hadi uombe “maisha yao yarudi kawaida”.?
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
6,833
2,000
Una uhakika sababu haujafiwa?sijui hata niseme nini

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu toka corona ianze hadi sasa ilitakiwa tuwe tunakufa kama kuku na sio sasa tunabishana juu ya vifo vya corona et serikali inaficha,tangu lini vifo vikafichwa? Hakuna hatua yeyote ambayo unaweza kusema Tanzania imefanya yenye tija ili kuzuia maambukizi ya hiyo corona,huku kunawa mikono,kufunga mashule na level seat ndio utasema unazuia maambukizi? ndio maana nasema kama kweli corona inayowauwa wazungu ndio hii tuliyonayo Tz basi hadi sasa tusingekuwa tunabishana kuhusu idadi ya vifo vya corona sijui serikali inaficha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom