Ni wakati sahihi wa Baraza la Mitihani Taifa "NECTA" kubadili utaratibu wa adhabu zake kwa wizi wa Mitihani

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,844
3,129
Habari wanabodi.

Kuna jambo ambalo nimekuwa kwa muda mrefu limekuwa likigharimu mustakabali wa maishaya vijana wetu kutokana na adhabu zinazotolewa na Baraza la Mitihani Taifa NECTA kila mara yanapotangazwa matokeo.

Suala hili siyo jingine bali ni kufutwa kwa matokeo ya shule nzima badala ya aidha wanafunzi pekee waliothibitika kufanya udanganyifu au wahusika wengine kuadhibiwa.

Ni ukweli usiopingika kwamba mdanganyifu wa aina yoyote kwenye mitihani kwa ngazi yoyote haukubaliki, hivyo hatua lazima zichukuliwe, lakini hatua hizo na adhabu zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kiweka mizani sawia. Ipo mifano kadhaa ya shule ambazo zimefutiwa matokeo yake na hata wazazi, walezi pqmoja na wanafunzi waliofutiwa kubaki na mshangao.

Unapozungumzia udanganyifu, wizi au kuvuja kwa mitihani hapa unaongelea mnyororo mzima wa udanganyifu kama ifuatavyo.

A. Wasimamizi wasio waaminifu na wenye tamaa wanaoruhusu kwa namna yoyote mitihani kuwafikia wanafunzi kabla ya muda wa kuwatahini.

B. Wasimamizi, wamiliki wa shule au yeyote anayetengeneza mazingira ya wanafunzi kufanya udanganyifu ndani ya chumba cha mtihani. Hii ni kwa kuoneshana majibu au maswali kufanyika nje ya chumba cha mtihani nk.

C. Wamiliki au viongozi wa shule wanaoshawishi wasimamizi kuhusika kufanya udanganyifu.

D. Wanafunzi watahiniwa wanaotumia udhaifu wa wasimamizi wao kufanya udanganyifu.
Ukiangalia sababu zote hizo (a) - (c) haziwahusishi wanafunzi moja kwa moja, lakini athari za uamuzi wa kuwafutia zinawakumba wao moja kwa moja na kuharibu future yao.

Naomba ifahamike kwamba, wanafunzi hawa kwa umri wao na akili zao hawana nguvu ya kiushawishi kwa wataalamu walioaminiwa na Baraza kusimamia mitihani hiyo, ikizingatiwa kuwa wasimamizi wanapatikana kwa vigezo vilivyowekwa pamoja na kutambua masharti ya kazi zao.

Wajibu wa Baraza pamoja na majukumu yaliyotajwa kwenye kanuni na miongozo yake ni kuhakikisha mitihani inaandaliwa katika mazingira salama toka hatua ya utungaji, uchapishaji, usambazaji na upatikanaji wasimamizi.

Hapa hakuna mwanafunzi anahusika.
Yeye ni mtu wa mwisho na anayeathirika na adhabu za udanganyifu. Labda kwa sababu ndiye mtu anayepimwa.

Athari za kufutiwa matokeo kwa shule. so
Wanafunzi na wazazi kwa ujumla wamekuwa wahanga wakubwa huku wengine wakiwa hawajui chochote kuhusu wizi/udanganyifu unaofanyika kwenye shule zao.

Fikiria mtoto wa darasa la 7 ambaye shule yake imefutiwa matokeo anakuwa ndoto yake ya kujiendeleza kielimu imefutika.

Tazama umri wao, uchanga wa akili zao na namna wanavyoweza kukabiliana na changamoto za maisha.

Mzazi nao kubaki katika sintofahamu huku asijue ampeleke wapi mwanaye kwa ajili ya maisha yake baadaye.

Mtoto anayetokana na shule husika kujiona mwenye hatia ambayo huenda hakushiriki au kuonekana mdanganyifu katika maisha yake yote.

Psychologically inawaathiri.

MAPENDEKEZO
Baraza lisikwepe kuwajibika, kwani kupitia taratibu zake wanaweza kujua chanzo kwa usahihi nani mhusika mkuu wa udanganyifu huo.
Hivyo nashauri yafuatayo:-
1. Wasimamizi, walimu au yeyote aliyehusika hadi mtihani kufanyiwa udanganyifu kabla au ndani ya chumba cha mtihani wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria na kanuni za baraza.
2. Wanafunzi wapatiwe nafasi nyingine ili wasipoteze haki zao kwa uzembe wa watu wengine.

Kama kumbukumbu yangu itakuwa vizuri, mwaka 1999 mitihani ya kidato cha nne ilivuja na badala yake kurudiwa, mwaka 2008 hali kadhalika somo la hisabati pia lilirudiwa baada ya kuonekana kuwafikia wanafunzi kabla ya muda wa kutahiniwa.
Hii tafsiri yake ni kwamba Baraza linatakiwa kuwa na mifumo imara ya kulinda mitihani.

Kama hii haitishi, mwaka fulani nikiwa kanda fulani hapa nchini nilishuhudia shule moja kupokea mwalimu kama first appointment ya ajira, lakini kazi yake kuu ilikuwa kufanya uchunguzi wa wizi wa mitihani shuleni hapo. Finally ukweli ulinainika, sasa kama hili linawekekana kwanini kukimbilia adhabu ambayo naiona kuna watu wanastahili kuwajibika kabla?

Mwisho nipende kuiasa jamii kuanzia wazazi na walezi, walimu na wanafunzi wote kila mmoja kutambua athari za udanganyifu wa mitihani huku tukitambua kwamba kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Kila mmoja atambue adhabu anayoweza kukumbana nayo, lakini tujue athari zake ni pamoja na kuwa na utumishi usiokidhi viwango kutokana na kupata wasomi wasio na sifa.

Naomba kuwasilisha
reslt-pic-data.jpg
 
Back
Top Bottom