Ni wakati muafaka watumishi wa Umma kumuadhibu Rais Magufuli

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Sina mengi ila ni wito tu nautoa kwa watumishi wote wa umma kutoa adhabu kali kwa Rais Magufuli kwa kuupigia kura upinzani ili kumkumbusha nguvu mliyonayo kwa jamii.

Maana licha ya mchango mlioutoa (hasa watumishi wa halmashauri) kwenye kumuweka madarakani mwaka 2015, amejifanya kuwasahau kwa miaka yote mitano. Kipindi chote amewafanyia mambo mabaya na ya aibu ili kujipatia umaarufu miongoni mwa jamii.

Udhalilishaji: Rais Magufuli amekuwa akidhalilisha watumishi kwenye mikutano ya wazi mbele ya camera ili apate umaarufu kinyume na kanuni za utumishi wa umma. Je, mtapenda hali hiyo iendelee? UAMUZI NI WENU

Mishahara: Licha ya kwamba kupandishwa mishahara na kulipwa stahiki mbalimbali ni kwa mujibu wa Sheria na kanuni za utumishi wa umma, yeye kwa jeuri, kibri na dharau, amesimamisha vyote kwa miaka mitano. UAMUZI NI MWENU KUTOA ADHABU KALI KWENYE SANDUKU LA KURA

Ubaguzi kwenye kuadhibu: Tumeshuhudia watumishi wengi wakiondolewa makazini kwa kuwa na vyeti feki, hii ni sawa, lakini kaifanya kwa ubaguzi mkubwa. Baadhi ya sekta hajagusa. Pia, baadhi ya watu hajawagusa, mfano Makonda. NI WAKATI WA KUMKUMBUSHA KUHUSU USAWA.

NI HAYO TU
 
CreativityCode,

Hakuna kundi la hovyo kama wafanyakazi wa serikali. They are highly stupidly divided. Kuna wenye vinafasi vyao, wanapata kila aina ya upendeleo, wana vi project vyao wanapata vijisenti, kuna askari, hao ni mitulinga bila akili! akipata rushwa ya kumbambikia mtu, anadhani ndio maisha yalivyo! Hao wanamuona Jiwe kama Mungu! Hili ni kundi baya sana tena la usaliti mkubwa.

Waliobaki ni bora liende, ana kamradi ka kuuza vitumbua, basi inatosha!
 
Hakuna kundi la hovyo kama wafanyakazi wa serikali. They are highly stupidly divided. Kuna wenye vinafasi vyao, wanapata kila aina ya upendeleo, wana vi project vyao wanapata vijisenti, kuna askari, hao ni mitulinga bila akili! akipata rushwa ya kumbambikia mtu, anadhani ndio maisha yalivyo! .....hao wanamuona Jiwe kama Mungu! Hili ni kundi baya sana tena la usaliti mkubwa.

Waliobaki ni bora liende, ana kamradi ka kuuza vitumbua, basi inatosha!
Naunga mkono hoja,acha nyongeza,acha kupandishwa madaraja hata increment tu Hakuna.
 
CreativityCode,

Hakuna kundi la hovyo kama wafanyakazi wa serikali. They are highly stupidly divided. Kuna wenye vinafasi vyao, wanapata kila aina ya upendeleo, wana vi project vyao wanapata vijisenti, kuna askari, hao ni mitulinga bila akili! akipata rushwa ya kumbambikia mtu, anadhani ndio maisha yalivyo! Hao wanamuona Jiwe kama Mungu! Hili ni kundi baya sana tena la usaliti mkubwa.

Waliobaki ni bora liende, ana kamradi ka kuuza vitumbua, basi inatosha!
Waliowengi wanaamini ccm ndio imewaajiri hili ni tatizo kubwa
 
Sina mengi ila ni wito tu nautoa kwa watumishi wote wa umma kutoa adhabu kali kwa Rais Magufuli kwa kuupigia kura upinzani ili kumkumbusha nguvu mliyonayo kwa jamii....
Wanafunzi wa vyuo na wafanyakazi wa umma mpigeni za uso huyo mtu maana amewaumiza sana kwa miaka mi5 yake.
 
Wanyonge tunaenda kuchana mkeka na kupindua meza Ni yeye 2020 kadi ya mpiga kura naitunza mbali sana kwajili ya kiburi cha 28/10/2020
 
Nitamchagua magufuli, mbunge wa chadema na diwani wa chadema.
Magufuli anafaa sana, tena sana. Tatizo kuna wapumbavu wachache hawamwelewi hasa wachaga na chadema yao
Naona mkuu ujumbe wako umejaa contradiction. Kama wewe Magufuli anakufaa, nenda kampigie kura waache wengine wapigie yule wanao amini anawafaa-usiwalazimishe. Nashangaa unaingiza ukabila hapa.
 
Hawajielewagi hawa viumbe, pamoja na msoto wa kilio na kusaga meno wa miaka 5 naona kabisa wakijichagulia hii adhabu kwa Mara ya pili.
Umasikini wa akili mbaya sana.
 
Nitamchagua magufuli, mbunge wa chadema na diwani wa chadema.

Magufuli anafaa sana, tena sana. Tatizo kuna wapumbavu wachache hawamwelewi hasa wachaga na chadema yao
Wewe ndio bure kabisa. Unamchagua aliyewaondolea meno wabunge. Wabunge wa magufuri umewaonea. Wewe piga baba kisha lea watoto wake hakika hawatokuangusha.
 
Sasa hapa ni bora CCM kuliko nyie mnaowatukana.

Back
Top Bottom