Ni wakati Muafaka wanadiplomasia wetu kuisaidia nchi, kumsaidia Rais Magufuli

Huwa nasikia neon Diplomasia ,lakini ukweli Sielewi linamaana gani. Wenye hizo diplomasia huwa wanafanya nini hadi uwaombe wamsaidie rais?
 
Tatizo ni viongozi wa dini ya kikiristo wamechangia pakubwa, badala ya kumpa ushauri rais, wao kazi ni tumuuombee rais? Aombe we ili aharibu nchi kidiplomasia au? Kuvuga democracy au? Wa kulaumiwa ni wengi sana
Anahitaji 'divine intervention' haimudu nafasi
 
JK akiwa waziri wa mambo ya nje kutamfanya raisi aheshimu sheria na kuacha matamko yasiyoeleweka?

Uwepo wa JK hautomfanya awe na nidhamu, atakuwa na kaz ya kusahihisha makosa yk? Kama anashindwa kuheshimu katiba inayowalinda raia wote hyo JK atafanya nn!! Mpaka hapo inaonyesha hamuheshimu JK naamini kila cku wanampa ushaur ila kwakuwa ana kiburi cha uzima kwake c jambo la maana.

Wengine watasema tunaongea sana kwny mitandao no actions, ukwel n kwamba jamaa alipofikia inatosha n heri akapumzike awaachie wengine wenye uwezo wa kuyafanya haya.

Hao wanadiplomasia nguli na wengineo wafanye jitihada za kumshauri apumzike inatosha, tunakoelekea huko n hatar kwa ustawi wa taifa.
Mkuu umeongea vizuri Mno, unajua tatizo linapotokea mawazo mengi pia hujitokeza ktk kuona namna ya kujikwamua. Mimi binafsi toka sikuile anatangazwa kuwa ndiye atakayebeba bendera ya CCM nilipata hofu sana maana I know the man.
 
Mkuu umeongea vizuri Mno, unajua tatizo linapotokea mawazo mengi pia hujitokeza ktk kuona namna ya kujikwamua. Mimi binafsi toka sikuile anatangazwa kuwa ndiye atakayebeba bendera ya CCM nilipata hofu sana maana I know the man.
Ubinafsi/umimi n mbaya sana katika taifa, haya mambo yalishatokea tulitekeza ss tuamke na kuanza safar kila mtu ajaribu kusafisha makosa yk naamini hata hao EU/USA watatuelewa kuwa tuna nia ya kuzilinda haki zetu sio wanadiplomasia wa kuleta propaganda za uongo kwamba hali n nzur huku raia wanateseka.
 
Msaidieni Mzee wetu na isaidieni Tanzania na vizazi vyake. Kwenye vikao vyenu mwambieni ukweli hata kama atapiga ngumi ukuta wa nyumba nyeupe. Hapa tulipofika panahitaji ujasiri. Ni wapi ambapo kuko salama ?

Mjiamini mumwambie ukweli. Tanzania inanuka sasa. Hatuwezi kuwa na mfumo peke yetu wa kujitenga na dunia. Subiri hio fitina itakayowekwa hata EAC, tutaanza kuvurugana kwa kuhisiana kutumiwa na EU. Hawa jamaa wana Strategic Plan Mbaya sana.

Mara Paap. Unaambiwa TZ si Salama kwa uwekezaji. Mara Paap unalazimishwa hiki na kile. Mara Paa uchumi unashuka vibaya huku majirani zako ukipanda mno.

Si wana machineries zote za kudhibiti mambo.

Kurudi nyuma si kushindwa.

Wanadiplomasia isaidieni nchi.
Dah.... Mkuu nyakati zinabadilika sana... Tusikariri....unaelewa kwanini Kuna EU? Dunia IPO kwenye kipindi kigumu cha mpito... Tuiombee....tujiombee...
 
Magufuli anafahamu tatizo na juzi ametangaza vita. Vita ya kiuchumi.
vita ya kiuchumi hatuiwezi, tutaaangamia kama tulivyoangamia wakati wa Nyerere.
Ghaddafi ambae alikuwa na nchi yenye kipato kizuri alipoanza vita ya uchumi ikamuondoa. Hali kadhalika Mugabe na kabla yake Mengistu.

Vita ya kiuchumi inahitaji ipiganwe kidiplomasia "kula uliwe".
Iran ina mafuta ya kumwaga, ina teknolojia ya kisasa lakini hali ni mbaya kwasasa

Iran walimuondoa Ahmadinajad kwasababu alikuwa 'mtemi' kuliko mwanadiplomasia
Iliundwa timu ya wanadiplomasia wakiongozwa na mtu wa msimamo wa kati Hassan Rouhani akisaidiwa na akina Mohamed Zarif

Iran wakatengeneza deal na US/EU/Russia na China ambalo Trump anataka kulifumua
Kutokana na Diplomasia iliyotumika, Israel na US wanaonekana kukwama at least kwa sasa
EU wanaunga mkono deal na sasa wanatafuta njia za kukwepa matumizi ya dola ili wafanye biashara na Iran

Iran inatengeneza nuclear achilia mbali makombora ya masafa marefu n.k.
Wana wataalam wazuri sana wa kila nyanja kuanzia elimu , afya, mazingira n.k.

Pamoja na hayo, Iran wamebaini 'vita' ya uchumi haipiganwi bila diplomasia.

Mugabe akichukua Zimbabwe kutoka kwa Smith hali ya uchumi ilikuwa bora sana ukiachilia ubaguzi

Mbabe Mugabe ameiacha nchi ikiwa inaelea, hatujifunzi kitu hapo?

Nikiitazama Tanzania yetu, nina wasi wasi sana kama kweli hii ni vita tunayohitaji

JokaKuu
 
Tuna gwiji la diplomasia, Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete. Lakini Magufuli hatoafiki ushauri wake.

Ushauri utakuwa, hapa achia ngazi tu ili aje mtu mwengine kuweka mambo sawa.

Atakubali?
Siku siyo nyingi naona kabisa tutaongea lugha moja mama
 
..na kusafisha huu UVUNDO itachukua muda mrefu, nguvu, na akili nyingi.
Sidhani kama ni suala la muda mfupi.
Hawa jamaa wakikuweka katika 'radar' ni kazi kweli kweli. Si kwamba wana uwezo wa kiuchumi tu bali wa mbinu na mikakati.Wanaweza kutumia media zao ikafika mahali 'mtoto akipigwa kibao hadharani' ni issue ya kimataifa

Kutoka NY au London hadi Dar ni chini ya KM 20,000. Hawa jamaa wanazungumzia 'Rover' katika Mars KM Milioni 300+. Inachimba na kuwaletea habari . Yaani wanatafuta 'makanikia' ya dhahabu huko Mars
Mdororo wa uchumi 'waliutengeneza' wao ukaingia kule Mtimbira, Bigwa Marusembe, Nyamato hadi Magoroto

Nikiangalia hii ni ''uncharted waters''
 
Sidhani kama ni suala la muda mfupi.
Hawa jamaa wakikuweka katika 'radar' ni kazi kweli kweli. Si kwamba wana uwezo wa kiuchumi tu bali wa mbinu na mikakati.Wanaweza kutumia media zao ikafika mahali 'mtoto akipigwa kibao hadharani' ni issue ya kimataifa

Kutoka NY au London hadi Dar ni chini ya KM 20,000. Hawa jamaa wanazungumzia 'Rover' katika Mars KM Milioni 300+. Inachimba na kuwaletea habari . Yaani wanatafuta 'makanikia' ya dhahabu huko Mars
Mdororo wa uchumi 'waliutengeneza' wao ukaingia kule Mtimbira, Bigwa Marusembe, Nyamato hadi Magoroto

Nikiangalia hii ni ''uncharted waters''
Hahahaaa, nimeikumbuka issue ya Khashogi. My 6th yrs little boy aliniuliza siku moja, "ba, every time when I watch CNN, ALJAZEERA I read Khashog! Khashogi Khashogi, what is khashogi and what is that about? Media za wazungu noma ukiingia kwenye radar zao.
 
Heshima kwako mama. Kuna mtu humu jana alishauri kuwa huyu JK anaweza kumfaa sana Jiwe na Taifa letu kwa ujumla, kama vipi amteue tu awe mbunge afu ampe uwaziri wa mambo ya nchi kwamaslahi mapana ya taifa letu. Jakaya wa watu pamoja na yooote yaliyotokea ila alikua na uwezo mkubwa sana kuiingiza nchi yetu ktk kurasa za dunia in a positive way. Kila Rais alitamani kuja Tanzania ila sasa huyu Jiwe anaharibu kila kitu halafu kwa akili yake anashangaa kwanini watu hawamuelewi.
Hata mchele uwe mzuri vipi ukipikwa kwa mafuta ya taa hautalika ndugu. Hiyo ni chemistry tofauti.
 
Hapo ulipoanzia sipo.
Tulipiga kelele Mzee afuate katiba mlisema acha anyooshe nchi. Tulipiga kelele kuhusu kuporwa haki za kidemokrasia mlisema aachwe atekeleze ilani. Tulipiga kelele kuhusu ubaguzi na manyanyaso kwa wapinzani mlisema huyu sio JK. tulipiga kelele watu kupotezwa na kuuwawa kinyemela mlinyamaza kimyaa mkidhani ni ya wapinzani tu.

Leo nchi inaanza kuonja machungu ya matendo yenu tunashauri DIPLOMASIA ITUMIKE unaanza kuleta uchuro wa kijani hapa.
Natoa heshima zote KISHADA.
JE yote mnayo Sema hasikii?
Anataka kuwa RAISI WA MAISHA kama MGABE.
Zimbabwe inakaribia.
 
Back
Top Bottom