Ni wakati Muafaka wanadiplomasia wetu kuisaidia nchi, kumsaidia Rais Magufuli

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Wakati ni huu. Hizi dalili sio nzuri hata kidogo kwa ustawi wa diplomasia yetu na historia yetu. Dunia ya leo unalazimika kumuhitaji kila mtu kila nchi.

Tanzania inaelekea kusiko kuhusu mahusiano yetu na nchi za Ulaya. Uvunjivu wa haki za binadamu na demokrasia, kukosekana uwazi, ndani ya nchi na kushughulikiwa kila anayekosoa utawala wetu limekuwa tatizo sasa si ndani ya nchi pekee lakini hata nje sasa.

Tumeshindwa kuwa na viongozi wenye uwezo wa kupima kauli zao na vitendo vyao.Kumekosekana mbinu tu za kuendesha mambo.

Sio kwamba yote wanayoyataka watu wa ulaya kuwa ni mazuri kwetu, hapana. Na wala huu upinzani wa matakwa yao haujaanza kwenye awamu hii tu. Ifahamike kuwa awamu zote zilipingana na matakwa lakini tofauti iliyopo ni NAMNA

Awamu hii ya tano mpaka sasa kwa maoni yangu imeshindwa kutumia APROACH za kidiplomasia zinazokubalika kushughulika na hao watu.

Kwanza ndani ya nchi kuna fukuto, kwenye CCM (chama tawala) kuna fukuto na sasa ni fukuto ndani na nje.

Kuna hatari sasa ya nchi kuchukuliwa maazimio mazito zaidi .

Kabla hakujapambazuka zaidi, Nawaomba wanadiplomasia wetu nguli kutumia uzalendo wa hali ya juu ili kuinusuru Tanzania na mtengo. Bado hatujajimudu kiasi cha kushindana na nchi za Magharibi.

Yajayo hayafurahishi.

Kishada
 
Kuna mahali hakuko sawa. Siasa ya ndani imevurugwa na kujenga uadui. Hali hio inatoa mwanya kwa adui. Wapi pa kuanzia ? Jee watawala wako tayari kurejesha umoja wa kitaifa huku kuna watanzania lukuki wamepotea kusikojulikana ? Vipi hao wapinzani wenye mikesi ya kuunda na wengine bado wanasota Tuanzie wapi ?

Tuanze kusafisha Diplomasia au tuendelee na jeuri na kiburi cha kusema tusiingiliwe?

Kwa hali ilivyo wazungu wameshatuingiza kwenye 18 zao. Tusubiri hizo Policy review zao na tusubiri maamuzi yao kwenye Jumuiya za Kimataifa .
 
Hawa watu wana fitina mbaya. Lazima tupate watu wanaoweza Diplomasia sio kujifungia ndani ya nchi na kurusha maneno tu. Dunia ni kijiji. Fedha yetu itashuka mno, watatuachia mazingira ya kuonana maadui sisi wenyewe na watatubana kila kona
 
Wakati ni huu. Hizi dalili sio nzuri hata kidogo kwa ustawi wa diplomasia yetu na historia yetu. Dunia ya leo unalazimika kumuhitaji kila mtu kila nchi.

Tanzania inaelekea kusiko kuhusu mahusiano yetu na nchi za Ulaya. Uvunjivu wa haki za binadamu na demokrasia, kukosekana uwazi, ndani ya nchi na kushughulikiwa kila anayekosoa utawala wetu limekuwa tatizo sasa si ndani ya nchi pekee lakini hata nje sasa.

Tumeshindwa kuwa na viongozi wenye uwezo wa kupima kauli zao na vitendo vyao.Kumekosekana mbinu tu za kuendesha mambo.

Sio kwamba yote wanayoyataka watu wa ulaya kuwa ni mazuri kwetu, hapana. Na wala huu upinzani wa matakwa yao haujaanza kwenye awamu hii tu. Ifahamike kuwa awamu zote zilipingana na matakwa lakini tofauti iliyopo ni NAMNA

Awamu hii ya tano mpaka sasa kwa maoni yangu imeshindwa kutumia APROACH za kidiplomasia zinazokubalika kushughulika na hao watu.

Kwanza ndani ya nchi kuna fukuto, kwenye CCM (chama tawala) kuna fukuto na sasa ni fukuto ndani na nje.

Kuna hatari sasa ya nchi kuchukuliwa maazimio mazito zaidi .

Kabla hakujapambazuka zaidi, Nawaomba wanadiplomasia wetu nguli kutumia uzalendo wa hali ya juu ili kuinusuru Tanzania na mtengo. Bado hatujajimudu kiasi cha kushindana na nchi za Magharibi.

Yajayo hayafurahishi.

Kishada
Kukichwa kutambazuka lakini kabla jua halijachomoza.... Kiza huwa kinene na totoro....! Kunakaribia kupambazuka
tapatalk_1544428086255.jpeg
 
Kwa Mtazamo wangu aina ya Utawala uliopo Tanzania utajitia kiburi na hautakubali kutekeleza hayo mambo. Kwa nini tulifika huku haraka hivi ? Kuna tatizo. Ina maana hawakuwepo Top Diplomat wetu wakamshauri mzee ? Au walimuacha ajikaange kwa mafuta yake akiamini yeye ni jasiri ? Hawa watu wakiamua kukuvuruga hawashindwi. Naomba Mungu tusifike mahali Mzee akajakulazimishwa kujiuzulu na hao waliomzunguka na mitutu leo. wake up saidia Tanzania. Msaidieni Mzee sasa.
 
Msaidieni Mzee wetu na isaidieni Tanzania na vizazi vyake. Kwenye vikao vyenu mwambieni ukweli hata kama atapiga ngumi ukuta wa nyumba nyeupe. Hapa tulipofika panahitaji ujasiri. Ni wapi ambapo kuko salama ?

Mjiamini mumwambie ukweli. Tanzania inanuka sasa. Hatuwezi kuwa na mfumo peke yetu wa kujitenga na dunia. Subiri hio fitina itakayowekwa hata EAC, tutaanza kuvurugana kwa kuhisiana kutumiwa na EU. Hawa jamaa wana Strategic Plan Mbaya sana.

Mara Paap. Unaambiwa TZ si Salama kwa uwekezaji. Mara Paap unalazimishwa hiki na kile. Mara Paa uchumi unashuka vibaya huku majirani zako ukipanda mno.

Si wana machineries zote za kudhibiti mambo.

Kurudi nyuma si kushindwa.

Wanadiplomasia isaidieni nchi.
 
Wale wastaafu waliosifia hivi majuzi wanatwambiaje sasa ? unaona Vipi Chuo Pendwa UDSM mnasemaje tuko sawa ? Hamuoni hili gap ? kwani limeanza leo tu ghafla ilikuwa hamuoni mienendo Au mmemsusa Mzee kiaina ?
 
Mimi ningekuwa ndo Jiwe ningemuomba JK nimteue ubunge kisha nimfanye awe waziri wa mambo ya nje tushirikiane tujenge nchi. Hilo linawezekana na katiba haijazuia Raisi mstaafu kuwa mbunge au kuwa waziri, imezuia kuwa raisi tena tu!

Mbona akina Netanyahu , Ehud Barak na wengineo wamewahi kuwa wakuu wa serikali kisha wakawa mawaziri wa kawaida kabisa katika awamu nyingine?

Tujifunze kutumia resources zetu zote
 
Ufipa nyinyi mnapiga kelele kila siku kuwa TZ tutengwe kimataifa.... Leo mnataka tutafute suluhu kidiplomasia

Hao watu wameshasikia vilio vyenu vya kutaka tz itengwe Leo mnataka mpatane nao
 
Ufipa nyinyi mnapiga kelele kila siku kuwa TZ tutengwe kimataifa.... Leo mnataka tutafute suluhu kidiplomasia

Hao watu wameshasikia vilio vyenu vya kutaka tz itengwe Leo mnataka mpatane nao
Hapo ulipoanzia sipo.
Tulipiga kelele Mzee afuate katiba mlisema acha anyooshe nchi. Tulipiga kelele kuhusu kuporwa haki za kidemokrasia mlisema aachwe atekeleze ilani. Tulipiga kelele kuhusu ubaguzi na manyanyaso kwa wapinzani mlisema huyu sio JK. tulipiga kelele watu kupotezwa na kuuwawa kinyemela mlinyamaza kimyaa mkidhani ni ya wapinzani tu.

Leo nchi inaanza kuonja machungu ya matendo yenu tunashauri DIPLOMASIA ITUMIKE unaanza kuleta uchuro wa kijani hapa.
 
Endeleeni kumwambia sisi hatupangiwi. Mjazeni upepo sana, subirini Ban zianze. Subirini zije kauli za list ya watu waliotolewa Arrest warrant ya Kimataifa ndio mtaamini kuwa hawa watu wanaweza fitina.
 
Ufipa mnabadili gia angani ... haya hamieni huko kwa wanadiplomasia
Hapo ulipoanzia sipo.
Tulipiga kelele Mzee afuate katiba mlisema acha anyooshe nchi. Tulipiga kelele kuhusu kuporwa haki za kidemokrasia mlisema aachwe atekeleze ilani. Tulipiga kelele kuhusu ubaguzi na manyanyaso kwa wapinzani mlisema huyu sio JK. tulipiga kelele watu kupotezwa na kuuwawa kinyemela mlinyamaza kimyaa mkidhani ni ya wapinzani tu.

Leo nchi inaanza kuonja machungu ya matendo yenu tunashauri DIPLOMASIA ITUMIKE unaanza kuleta uchuro wa kijani hapa.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom