Ni wakati muafaka wa Zanzibar kujitenga na Tanganyika

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Ukifuatilia matamko ya Serikali ya Zanzibar baada ya huu ugonjwa wa Korona ni wazi kuwa Zanzibar inajitambua, inapenda wananchi wake na ina uwezo wa kuchukua hatua kwa akili na stahiki kulinganisha na huku bara.

Sasa sijui ilikwaje hadi wakaingia mkenge na kuingizwa kwenye ndoa na Tanganyika.

Sasa nadhani ni wakati wa visiwani kujitoa kwenye hii ndoa.

Inawakwamisha mengi sana na mungeshafika mbali.

Ni mawazo yangu:

Updates:

Baada ya kuanzisha huu uzi kuna jamaa wanajaribu ku hack account yangu.
Ila bora waje pm tuongee kwa sababu Hawataweza. Mimi ni JF kitambo na huwezi kuotea password yangu kindezi ndezi .
Pumbavu.
07D9A6CD-6909-4B15-9122-A4F0DF0FFA69.jpeg
 
Utawaskia wale wasemao Zanzibar si nchi, mbona dodoma haijitolei matamko juu ya mambo yake?? Tarehe 17 Machi aitwae waziri mkuu aliwatangazia Watanganyika kwamba shule zote kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita zifungwe, tarehe kumi na nane wananchi wa Zanzibar walikwenda shule kama kawaida maana huku tuna taratibu zetu na nchi yetu.

Tarehe kumi na nane Mh. Hamad Rashid waziri wa afya wa Zanzibar ndio akawatangazia Wazanzibari kuwa kuanzia tarehe 19 Machi ndio shule zitafungwa na Sisi tukatii agizo hilo.

Tangazo la majaliwa kwa Watanganyika mwisho wake lilikuwa ni Chumbe.
 
Saint Ivuga, Mkuu St Ivuga, enzi hizi tuna bahati sana, Mwalimu Nyerere hayupo, enzi hizo huwezi kutamka maneno haya na ukaangaliwa hivi hivi.

Muungano wetu adhimu unauita mkenge? Je, ni kweli muungano unakwamisha mengi Zanzibar bila muungano ingekuwa mbali?

Kitendo chochote cha kuvunja muungano ni uhaini, hivyo huu sio uhaini?.

Angalia ushauri wangu kwa mtu huyu na nini kilifuatia

Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii - JamiiForums

Watanzania wazalendo wataulinda muungano kwa gharama yoyote!.
P
 
ni mawazo yako kweli ni haki yako ila jitahidi kuongeza sugar kwenye brain uwaze mengine yenye tija zaidi, mawazo yangu ni kuwa ni muungano ndo umekupa nafasi na utulivu ukawaza hayo uliyowaza!!
 
Ukifuatilia matamko ya Serikali ya Zanzibar baada ya huu ugonjwa wa Korona ni wazi kuwa Zanzibar inajitambua, inapenda wananchi wake na ina uwezo wa kuchukua hatua kwa akili na stahiki kulinganisha na huku bara.
Sasa sijui ilikwaje hadi wakaingia mkenge na kuingizwa kwenye ndoa na Tanganyika.

Sasa nadhani ni wakati wa visiwani kujitoa kwenyw hii ndoa.

Inawakwamisha mengi sana na mungeshafika mbali.

Ni mawazo yangu:
Zanzibar ni wajanja wachache kuliko Tanganyika kitambo wao cha Zanzibar ni cha mzanzibar lakini cha Tanganyika ni cha wote, Pesa ya kuwalisha kuwaliea kuwalinda inatoka Hazina hapo Dsm, ni kisiwa kidogo lakini kimejirundikia utitiri wa watumishi wa umma kwa malipo ya mishahara toka Tanganyika, ZRA makusanyo yao ya kodi ni madogo sana hayatoshi hata kulisha kijiji cha Mwanakwereke au miembeni tu, wengi ni chuma ulete wakaa vibarazani hasa unguja mda mwingi kupiga story za kuomba kuolewa na Oman hawataki ndoa ya Tanganyika, ukitaka kujua Zanzibar wana Akili kuliko Tanganyika angalia wao wana baraza lao la wakilishi hakuna mbunge toka Tanganyika anasogea huko , lakini wabunge wao wamefurika Dodoma Bungeni ni wengi ni mawaziri Tanganyika lakini Zanzibar hakuna waziri toka Tanganyika, Pesa nyingi ya Tanganyika inafaidisha Zanzibar kuliko Tanganyika kufaidika na Zanzibar, mtu toka Tanganyika huwezi kumiliki Aridhi Zanzibar lakini mzanzibar yeye ruksa kumiliki Ardhi popote Tanganyika, Zanzibar ni mzigo inaichuna Tanganyika imekuwa buzi la Zanzibar. Wao wana bendera yao wimbo wao wa Taifa na baadhi ya vikosi vyao vya majeshi na pesa zote zinalipwa na Tanganyika ni vioja, pesa inayotumika kuilea Zanzibar ni pesa ambazo zingeweza kujenga Hosptal za rufaa , vyuo vikundi, barabara za lami kila kijiji Tanganyika na pengine Tanganyika ingekuwa ni nchi tajiri kuliko hata China South Africa German, Zanzibar ni mzigo mkubwa unaoifirisi Tanganyika.
 
kwakweli bangi ni mbaya sana ukiivuta kwa kukusudia apo umeandika ujinga mtupu kwamba hela ya kuwapa Zanzibar ingetufanya kuwa kama china?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom