miamiatz
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 504
- 927
Tanzania na Africa kwa ujumla bado tunasua sua kwenye kasi ya maendeleo ya kiteknolojia. Vipaji vingi sana kwenye sector ya teknolojia vinakosa muendelezo na njia sahihi za kupita.
Nadhani inatakiwa viongozi wetu waamke sasa na wajue kuwa hata kwenye IT kuna watu wanaoweza kufanya mambo makubwa wakipata majukwaa sahihi.
Serikali zinaonesha kuthamini wafanya biashara wadogo wadogo kwenye upande wa bidhaa ila zinasahau kuwa hata kwenye huduma za ki IT kuna wafanya biashara wadogo wadogo.
Kuanzishwa kwa startup hubs za ki IT itasaidia sana kuleta mageuzi ya matumizi ya IT kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili jamii.
Kama vile ilivyo kwa upande wa viwanda na wawekezaji wakubwa kuwekewa EPZ, IT sector nayo inatakiwa kuwekewa startup hubs ambazo humo ndani kunakuwa na masharti nafuu ya kuanzisha na kuendesha biashara.
Wengi tunafahamu kuwa ili ujiajiri unatakiwa kujisajili. Usajili wa kitanzania ni ule wa kizamani ambapo unatakiwa kukadiria kodi ya mwaka wa kwanza na kulipa robo yake kabla hata hujapewa TIN, Tax Clearence wala Business License
Pia tunafahamu kuwa IT inahitaji kutest concept na feasibility of the concept kabla hujawekeza kwa kasi.
Huwezi mwambia kijana ajisajili, alipe kodi, apange fremu ili akatest concept yake. If it fails hasara yake.
Changamoto hii inatatuliwa kwa kuweka startup hubs kadhaa na kusajili wote wenye vipaji vya kufaa kuwa humo. Wafanye testing ya concepts zao backend na frontend (ikimaanisha kujaribu pia soko).
Startup hubs za aina hii zinafaa kutokuwa na gharama yoyote ya kujiunga. Cha msingi ni kuthibitisha kipaji chako. Iwe kama sehemu ya kuwapitisha watu wajaribu idea zao kama zina uhalisia ama ni ndoto.
Courtesy of miamiatz