LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,146
- 11,192
Kwa hali nnayoiyona kimara mwisho kila siku asubuhi, jinsi tunavyopata tabu kutokana na huu mradi wa UDART kutetereka sasa ni mda mzuri wa serikali kuruhusu Daladala za zamani zipate kibali cha kubeba abiria kuanzia mbezi mwisho kuelekea mjini
Mateso tunayoyapata kila siku asubuhi na jioni ni makubwa, mradi huu wa UDART ulianza vizuri lakini sasa kazi imewashinda, abiria tunabanana kwenye mabasi mwishowe tutaambulia kifua kikuu sasa,
Huu ni mda wa serikali kuyapa leseni baadhi ya daladala za zamani hasa zile kubwa zenye milango miwili kama EICHER nazo zibebe abiria katika njia ya pembeni ili kuleta ushindani na kusaidia abiria wanaoteseka
Kila siku tunachelewa makazini hadi vibarua vinataka kuota nyasi na waajiri ukiwaeleza hawaelewi, yote kisa UDART, biashara yoyote ili iwe imara ni lazima ipate mshindani hapo heshima itakuwepo, UDART imekosa mshindani na ndio maana wanafanya wanavyojiskia wakiamua kupaki mabasi wanapaki wakiamua kubeba abiria wanabeba kisa tu wapo wenyewe
Ni mda muafaka kwa serikali yetu kutoa leseni kwa baadhi ya daladala kubwa nazo zibebe abiria katika njia ya pembeni, usumbufu hautokuwepo tena na hii iawasaidia UDART au kama atatokea mwekezaji mpya kuwa na ufanisi kwenye kazi ila wakiachiwa wenyewe hawa hawatakaa wabadilike