Ni muda muafaka kupeleka hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Kutokana na hali na upepo wa kisiasa, natumaini kwa wabunge wa Tanganyika huu ni Muda muafaka wa kupeleka hoja ya kubadili katiba na kuanzisha serikali ya Tanganyika na kuanzisha vifungu vya kulinda maliasili za watanganyika . That said, Rais JM Kikwete apewe muda wa kuongoza serikali ya Muungano [URT] kwa muda wa miaka miwili kusimamia mchakato wa kuanzisha Katiba mpya ya Tanzania ambayo itakuwa na maudhui ya kuanzisha Federal State.Uchaguzi wa mwaka huu usogezwe mbele hadi 2012. Hii imekaaje?
 
Sipingi uwepo wa Muungano. La hasha. Ila lazima tuwe wakweli ni wakati mwafaka wa kuwa na Serikali ya Tanganyika. Iongozwe na Mtanganyika na asimamie rasilimali za Tanganyika.

Zanzibar iwe huru kama ilivyo sasa na Serikali yake. Ijulikane wazi mchango wa zanzibar na tanganyika katika kuendesha Serikali ndogo ya Muungano.

Nafasi za uongozi katika structure ya Serikali ya Tanganyika ziwe kwa Watanganyika kama ilivyo kwa sasa Zanzibar nafasi za uongozi zipo kwa wazanzibari.

Hawa ma DC waliopo Mkuranga na Kilosa toka Zanzibar sio sawa kwa sasa. Huu muundo ni kero.
 
IMG_8397.jpg

Acha donge mtanganyika, ASALI inalambwa kwa Awamu
 
Nadhan hata kama ni kwakutumia Nguvu, Zanzibar inabidi uwe Mkoa.

Isiwe tena Jamhuri ya Muungano, Bali iwe Jamhuri ya watu wa Tanzania
 
Muungano hauna tija yoyote kwa watanganyika ni gobbledygook mtupu.

Lengo la kuungana harakaharaka baada ya mapinduzi yao lilikuwa kumzuia Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said asirejee Zanzibar.

Utawala wa kisultan hauwezi kurudi tena Zanzibar hata ukirudi sisi hayatuhusu.
 
Sipingi uwepo wa Muungano. La hasha. Ila lazima tuwe wakweli ni wakati mwafaka wa kuwa na Serikali ya Tanganyika. Iongozwe na Mtanganyika na asimamie rasilimali za Tanganyika.

Zanzibar iwe huru kama ilivyo sasa na Serikali yake. Ijulikane wazi mchango wa zanzibar na tanganyika katika kuendesha Serikali ndogo ya Muungano.

Nafasi za uongozi katika structure ya Serikali ya Tanganyika ziwe kwa Watanganyika kama ilivyo kwa sasa Zanzibar nafasi za uongozi zipo kwa wazanzibari.

Hawa ma DC waliopo Mkuranga na Kilosa toka Zanzibar sio sawa kwa sasa. Huu muundo ni kero.
EEEeeenHeeee, Heeee!

Nimekupata vizuri sana mkuu 'The Terrible Teen'; ila hadi iwe hivyo, tayari mapendekezo yako sha pitwa na wakati.

Kiongozi wa Tanganyika kuwa mTanganyika maana yake ni nini; au itakuwa ipi? Watu toka visiwani ambao sasa wanajichukulia mapande ya ardhi na mali za Tanganyika wakati huo watakuwa ni waTanganyika kamili, ambao ndio wataiongoza Tanganyika iliyomo kwenye fikra zako hapa. Huku wakati huo huo, hakuna mTanganyika hata mmoja anayeweza kudai kuwa MZanzibari.

Sasa sijui utasema nini tena?
 
Hawataweza, serikali moja itafikiwa tu, inaweza kuchelewa lakini ndio kituo kinachofuata.
Itahitaji kiongozi imara sana kulisimamia hili. Samia hawezi kabisa, ila anaweka mazingira ya kiongozi huyo shupavu kutimiza haya unayoyasema hapa.
 
Sipingi uwepo wa Muungano. La hasha. Ila lazima tuwe wakweli ni wakati mwafaka wa kuwa na Serikali ya Tanganyika. Iongozwe na Mtanganyika na asimamie rasilimali za Tanganyika.

Zanzibar iwe huru kama ilivyo sasa na Serikali yake. Ijulikane wazi mchango wa zanzibar na tanganyika katika kuendesha Serikali ndogo ya Muungano.

Nafasi za uongozi katika structure ya Serikali ya Tanganyika ziwe kwa Watanganyika kama ilivyo kwa sasa Zanzibar nafasi za uongozi zipo kwa wazanzibari.

Hawa ma DC waliopo Mkuranga na Kilosa toka Zanzibar sio sawa kwa sasa. Huu muundo ni kero.
Asilimia 100 uko sahihi ila kuwa na serikali tatu ni udhaifu mkubwa sana badala ya kuwa na serikali moja tu kisha pasiwepo visingizio kwamba Zanzibar ni kwa Wazanzibar pekee kwamba mtu kutoka bara haruhusiwi kuwa na ardhi au kupata uongozi huko Zanzibar.

Sababu kuu inayofanywa na mkuu wa nchi kwa sasa ni sawa kama walivyofanywa Mwinyi kukulia na kupata uongozi akiwa Zanzibar hadi kuwa rais. Hivi ndivyo inavyoenda kutokea kwa hawa wakuu wa wilaya za Kilosa Morogoro na Mkuranga Pwani kimkakati wanataka kuhodhi maeneo hayo kwa maslahi ya wazanizibari hatimaye kuja kupata uongozi wa juu kama wabara kitu ambacho kitazusha migongono mikubwa ya kiutawala wa nchi siku sio nyingi zijazo ijapokuwa watawala wanadharau wakijua hakuna mwenye uwezo wa kuabdilisha bango.
 
Back
Top Bottom