GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,856
Kwa jinsi ninavyomjua Mtani wangu wa Kihaya, Kaka yangu, Mkuu wangu na Genius IT Guru Maxence Melo akikubali Teuzi yoyote ile ndani ya Tanzania hii ya sasa yenye Siasa za Kinafiki, Kujipendekeza na Tawala zisizojielewa zenye Kuharibu badala ya Kujenga nitamdharau mazima hadi Umauti wangu.Ndugu zangu wa JF
Naongea kwa upendo na uzalendo mkubwa kwa nchi yangu ya Tanzania
Namzunguzia Ndg Maxence Melo
Huu ni wakati muafaka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua na kumpangia Maxence Melo majukumu makubwa ya Kitaifa
Amekuwa na Utumishi uliotukuka akiwa Mtendaji Mkuu wa Jamii Forum kuanzia 2006
Kipaji chake ni kikubwa bila kusahau ubunifu wake wa hali ya juu
Amepitia na kukabiliana na changamoto mbalimbali kubwa na ndogo za amemudu kukabiliana nazo kikamilifu
Amekuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu kupitia jukwaa maarufu la Mtandao wa Jamii Forum
Amepoekea tuzo mbambalimbali za kimataifa kutokana na kazi zake zilizojaa Weledi mkubwa
Anafahamika, anakubalika pakubwa ndani na nje ya nchi yetu
Ni mtu jasiri na mwenye msimamo usioyumba asiyeogopa kusema na kutetea ukweli
Ni msomi mkubwa, mchapakazi, nwenye Weledi mkubwa kwenye fani yake
Ni Wakati wa kuzika tofauti zilizopo na kumpangia majukumu makubwa ya Kitaifa
Nawasilisha
Kwa IQ yake Maxence Melo nchi ambazo nikisikia kapata 'Ulaji' huko na GENTAMYCINE nitafurahi na Kumfurahia ni za Rwanda, USA, Russia, Israel, China, South Africa, Germany, England na Uganda ila siyo Tanzania.
Acheni tu abakie Kututumikia Sisi Watoa Maoni Huru kupitia huu Mtandao wake ambao kiukweli una Faida kubwa Kwetu Watanzania kuliko hata angekuwa katika Teuzi yoyote ile ya Kiserikali.
Ni Cheo Kimoja tu ambacho GENTAMYCINE naona kitamfaa kwa Tanzania hii nacho ni cha Yeye kuwa Head of State ( Rais ) na siyo Vingenevyo na akiwa Rais upesi sana aniteue kuwa Makamu wake ili kwa pamoja Akili za Kihaya na za Kizanaki ( wala Sato na Sangara wanasababisha Akili nyingi Kichwani ) ziwaongoze vyema Watanzania na ndani ya Mwaka Mmoja Tanzania itakuwa mbali sana Kimaendeleo na Kiustawi.