Ni Wakati Muafaka kwa Serikali Kulisaidia Kundi Hili la Vijana Lililosahaulika

pex

Member
Nov 20, 2009
57
13
Kuna wimbi la vijana wengi mtaani wasio na kazi. Wengi wao aidha ni kutokana na kufeli masomo shuleni na wengine ni kukosa fursa za kufanya kazi. Nguvu kazi hii ni kubwa na ni hasara kwa serikali ikiiacha ipotee. Lakini pia utakuwa ni mzigo kwa Serikali siku zijazo. Tukumbuke kuwa idadi kubwa ya vijana hawa wako chini ya miaka 30 na bado wana mchango mkubwa sana katika jamii zao na kwa nchi kwa ujumla. Kwa mujibu wa takwimu za sensa nafikiri ndio kundi kubwa zaidi linaloongoza katika population structure ya Tanzania.

Ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kuchukua hatua madhubuti kulisaidia kundi hili la vijana. Moja ya hatua ambayo naona inafaa ni kutoa fursa kwa vijana hawa kusoma bure katika vyuo vyetu vya VETA ili waweze kujipatia maarifa ya kuweza kutoa mchango wao kwa taifa. Haitoshi tu kwa serikali kuhimiza watu kufanya kazi, ni lazima ichukue jitihada za maksudi kulisaidia kundi hili kubwa la vijana linaloshinda vijiweni kila kukicha pasipo kujishughulisha na kazi yoyote ya ujenzi wa taifa.

Serikali inapasa kuchukua hali hii ya kuwa na idadi kubwa ya vijana nchini kama fursa ya kujijenga kiuchumi. Ninaamini kama fursa ya kusoma bure katika vyuo vyetu vya VETA itatolewa kwa vijana hawa mwitikio utakuwa ni mkubwa sana, kama ilivyokuwa kwenye elimu ya msingi na sekondari na fursa ilivyotolewa kwa vijana kujiunga na jeshi la kujenga taifa.

Vyuo vya VETA viandae program maalumu kwa vijana hawa ambao wote watapewa fursa, wenye vyeti na wasio na vyeti. Ambapo wenye vyeti vya uhitimu wa elimu ya sekondari wataanza moja kwa moja mafunzo ya program mbalimbali za VETA ambazo zitalenga mahitaji ya soko la sasa kama vile construction, electronics, mechanics, carpentry, sewing, shoe making, food processing na nyingine nyingi. Wale wasio na vyeti wataanza na mafunzo ya QT ili wapate vyeti na hatimaye kuendelea na program zingine kama wengine. Kwa njia hii tunaweza kusaidia idadi ya vijana wengi mtaani waliokata tamaa na maisha.
 
Back
Top Bottom