Ni wakati muafaka kwa Rais Samia kumpumzisha IGP Sirro

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,619
2,000
Kwa tabia, mwenendo na utiifu alio nao Kamanda IGP Sirro kwa mamlaka ya uteuzi yaani Rais wa JMT Mama yetu mpendwa Mama Samia, inabidi ampumzishe huyu Kamanda na aweke mtu mwingine atakaye msaidia.

Tangu Rais Samia ashike madaraka inaonekana IGP Sirro hatii kabisa maelekezo ya Rais! Kudhihirisha hili ni juzi wakti Rais akiongea na Maafisa wa Polisi HQ na mikoani alipolilaumu Jeshi la Polisi kwa kuendelea kukaidi maelekezo yake ya kubambikia Watu kesi, watuhumiwa kuuawa mikononi mwa Polisi na kuweka watu mahabusu kwa muda mrefu pasi na ushahidi huku wakisingizia @ upelelezi unaendelea! Even kesi ya Mwenyekiti Mbowe iko kwene mlolongo uleule wa kubambikia mtu kumkomoa.

Juzi baada ya shambulio la polisi toka kwa rais Hamza Mohamed na kuua mapolisi 3 na mlinzi 1 kawaida, IGP Sirro ameonekana kutoa maneno ya dharau kwa Watanzania kwa kuwalaumu WASIZAE WATOTO KAMA HAMZA MAANA NI BALAA KWA JESHI LA POLISI...Ebho! Yaani kwa akili ya IGP Sirro polisi wana thamani sana kuliko mamilioni ya Watz. Hivi nnani anawazaa Polisi wa Tanzania??? IGP Sero amefukuza wangapi kwa ukosefu wa maadili? Je, hao mapolisi walizaliwa na nani?

IGP Sirro kesha sahau kabisa kuwa kuna sera ya Jeshi la Polisi inayoitwa: POLISI JAMII AU SHIRIKISHI. Kwamba lazima raia wa Kitanzania washirikishwe kwene ulinzi wa nji hii. Lakini pia IGP Sirro amesahau kabisa kuna mamia ya Watanzania wameuawa na Jeshi la Polisi kwa makusudi kabisa kwa kusingiziwa ni majambazi kwa vile tu walikuwa na fedha au madini yenye thamani ya mamilioni. Watanzania wanajua hizi habari vizuri sana. Mfano ni kesi ya Zombe na askari wenzake!!

Nawasilisha.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
18,495
2,000
Una uhakika Mama ana uwezo wa kumwachisha hiyo nafasi? Unajua Role ya IGP kwenye uongozi wa Mama?
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Ni bora Mkuu wa jeshi la Polisi ndugu Siro akajiuzulu na kuachia japo umri wake umebakia kidogo alitaye,ni bora kwa sasa akajiuzulu na sio aibu wala fedheha,maana mkuu inaonyesha uzee unamvaa vibaya sana,haya maneno anayolipuka nayo kwa sie madakari tunajua ni dalili za umri na zipo aina nyingi kuna watu wanazeeka na akili zao zipo clear and sound well na kuna wengine kila wakizeeka wanakuwa na mambo ya ajabu ajabu maneno ya kiabu aibu yanawatoka hadharani.

Wengine wakizeeka akili zao wanakuwa ni wenye hasira hasira na wakali sana wala hawafikirii wanalosema alimuradi wawe wametoa karipio hata kama hapakustahili,kama Raisi Mgufuli (Marehemu) alikuwa anazeeka na akili za nipishe,ondoka,kaa kando na ndio alikuwa anafanya maamuzi onsite .

Siro uzee unamuandama na akili zake ni zile za kutoa kiburi busara imetoweka ,yaani ni za kujionyesha mimi kama mimi ni mkbwa wa polisi,mmeona mala amewageukia wazazi mala amewageukia polisi hana simile alikuwa anarapu tu,na watu namna hii kama wakiwa na muda wanaweza kusema mpaka mwisho wanakuwa wanatoa matusi ya nguoni wazi wazi bila ya aibu,si wao kama wao bali ni akili za kizee,na wapo wazee mitaani wao ni matusi tu utaweza kusema hawana akili,lakini hapaaaaaaana ni akili za uzee zinamsanifu bila ya kuvuta bangi wala mirungu au tumbaku.

Mheshimiwa Siri kwa sasa akili zake zinapoteza muelekeo wa busara za kiuutuzima zinaelekea kwenye uzee nahisi ni bora akatanabahi na kuachia ngazi ,
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,945
2,000
Anajiandaa kustaafu Sasa,to make clear huu ndo muda wa yeye kupiga dili Ili akasimamie miradi yake ndo Mana anajitoa ufahamu kidogo mpaka anapitiliza.
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,333
2,000
Huo msamiati upo ulaya.
Siro anaifanyia Kazi nzuri Sana ccm usitegemee hilo.
Tushazoea kuumia
 

Zidani

JF-Expert Member
Apr 5, 2021
972
1,000
Rais yupo zanzibar anarekodi ujinga tu badala ya kushugulikia mambo muhimu ya taifa letu.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,691
2,000
Kwa tabia, mwenendo na utiifu alio nao Kamanda IGP Sero kwa mamlaka ya uteuzi yaani Rais wa JMT Mama yetu mpendwa Mama Samia, inabidi ampumzishe huyu Kamanda na aweke mtu mwingine atakaye msaidia.

Tangu Mama Samia ashike madaraka inaonekana IGP Zero hatii kabisa maelekezo ya Rais! Kudhihirisha hili ni juzi wakti Rais akiongea na Maafisa wa Polisi HQ na mikoani alipolilaumu Jeshi la Polisi kwa kuendelea kukaidi maelekezo yake ya kubambikia Watu kesi, watuhumiwa kuuawa mikononi mwa Polisi na kuweka watu mahabusu kwa muda mrefu pasi na ushahidi huku wakisingizia @ upelelezi unaendelea!!! Even kesi ya Mwenyekiti Mbowe iko kwene mlolongo uleule wa kubambikia mtu kumkomoa!!!!

Juzi baada ya shambulio la polisi toka kwa rais Hamza Mohamed na kuua mapolisi 3 na mlinzi 1 kawaida, IGP Sero ameonekana kutoa maneno ya dharau kwa Watanzania kwa kuwalaumu WASIZAE WATOTO KAMA HAMZA MAANA NI BALAA KWA JESHI LA POLISI...Ebho! Yaani kwa akili ya IGP Zero polisi wana thamani sana kuliko mamilioni ya Watz....!!! Hivi nnani anawazaa Polisi wa Tanzania??? IGP Sero amefukuza wangapi kwa ukosefu wa maadili? Je, hao mapolisi walizaliwa na nani?

IGP Zero kesha sahau kabisa kuwa kuna sera ya Jeshi la Polisi inayoitwa: POLISI JAMII AU SHIRIKISHI. Kwamba lazima raia wa Kitanzania washirikishwe kwene ulinzi wa nji hii. Lakini pia IGP Zero amesahau kabisa kuna mamia ya Watz wameuawa na Jeshi la Polisi kwa makusudi kabisa kwa kusingiziwa ni majambazi kwa vile tu walikuwa na fedha au madini yenye thamani ya mamilioni. Watz wanajua hizi habari vizuri sana. Mfano ni kesi ya Zombe na askari wenzake!!

Nawasilisha.

Hawezi kusikia mwache aendelee naye
 

Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
3,260
2,000
Ni bora Mkuu wa jeshi la Polisi ndugu Siro akajiuzulu na kuachia japo umri wake umebakia kidogo alitaye,ni bora kwa sasa akajiuzulu na sio aibu wala fedheha,maana mkuu inaonyesha uzee unamvaa vibaya sana,haya maneno anayolipuka nayo kwa sie madakari tunajua ni dalili za umri,na zipo aina nyingi kuna watu wanazeeka na akili zao zipo clear and sound well na kuna wengine kila wakizeeka wanakuwa na mambo ya ajabu ajabu maneno ya kiabu aibu yanawatoka hadharani ,wengine wakizeeka akili zao wanakuwa ni wenye hasira hasira na wakali sana wala hawafikirii wanalosema alimuradi wawe wametoa karipio hata kama hapakustahili,kama Raisi Mgufuli (Marehemu) alikuwa anazeeka na akili za nipishe,ondoka,kaa kando na ndio alikuwa anafanya maamuzi onsite .
Siro uzee unamuandama na akili zake ni zile za kutoa kiburi busara imetoweka ,yaani ni za kujionyesha mimi kama mimi ni mkbwa wa polisi,mmeona mala amewageukia wazazi mala amewageukia polisi hana simile alikuwa anarapu tu,na watu namna hii kama wakiwa na muda wanaweza kusema mpaka mwisho wanakuwa wanatoa matusi ya nguoni wazi wazi bila ya aibu,si wao kama wao bali ni akili za kizee,na wapo wazee mitaani wao ni matusi tu utaweza kusema hawana akili,lakini hapaaaaaaana ni akili za uzee zinamsanifu bila ya kuvuta bangi wala mirungu au tumbaku.

Mheshimiwa Siri kwa sasa akili zake zinapoteza muelekeo wa busara za kiuutuzima zinaelekea kwenye uzee nahisi ni bora akatanabahi na kuachia ngazi ,
Kama na wewe ni daktari, na haujui walau kufuata kanuni za uandishi, basi tuna hasara kubwa sana kama taifa.
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,619
2,000
Huo msamiati upo ulaya.
Siro anaifanyia Kazi nzuri Sana ccm usitegemee hilo.
Tushazoea kuumia
Mbona huu msamiati hata Africa upo? Bila ya shaka umeyasikia Mr. HH-Rais mpya wa Zambia!! Kama Zambia imewezekana why not Tanzania?
Kusema ushazoea kuumia ni dhambi kubwa sana. Biblia imeainisha KUKATA TAMAA NI DHAMBI!
 

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
6,008
2,000
Una uhakika Mama ana uwezo wa kumwachisha hiyo nafasi? Unajua Role ya IGP kwenye uongozi wa Mama?
Nakazia hapa .... Mama hana uwezo wa kufukuza mkuu yoyote wa chombo cha ulinzi na usalama .... Maana ndio wamemuweka katiba ilikuwa inasiginwa ..wakambeba hana uwezo wa kuwatoa
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,619
2,000
Rais yupo zanzibar anarekodi ujinga tu badala ya kushugulikia mambo muhimu ya taifa letu.
Kweli inashangaza eti Rais anarekodi picha @ za kitalii!!!
Nchi ina watu 60 milioni + ina maana hakuna wasanii wa kufanya kazi hiyo??
Wanawake bhana.....!!!
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,619
2,000
Nakazia hapa .... Mama hana uwezo wa kufukuzwa mkuu wowote wa chombo cha ulinzi na usalama .... Maana ndio wamemuweka katiba ilikuwa inasiginwa ..wakambeba hana uwezo wa kuwatoa
Jamani acheni kujitoa ufahamu! Mamlaka ya uteuzi wa IGP ni Rais(whether ni Mama au baba). Hivo mamlaka ya uteuzi ikiona aliye teuliwa ana boronga basi ina Mamlaka ya KUTENGUA UTEUZI,KUSIMAMISHA ,KUFUTWA AU KUFUKUZWA.
 

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
6,008
2,000
Jamani acheni kujitoa ufahamu! Mamlaka ya uteuzi wa IGP ni Rais(whether ni Mama au baba). Hivo mamlaka ya uteuzi ikiona aliye teuliwa ana boronga basi ina Mamlaka ya KUTENGUA UTEUZI,KUSIMAMISHA ,KUFUTWA AU KUFUKUZWA.
Narudia tena HAWEZI ...japo ana mamlaka hayo ila HAWEZI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom