Ni wakati Muafaka kwa CHADEMA kutenda hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wakati Muafaka kwa CHADEMA kutenda hili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Omutwale, Nov 5, 2011.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi ni miongoni mwa watanzania ambao bado sijaridhishwa na ukarimu wa Wafanyakazi na hata viongozi wenziwe Zitto katika kumfariji na ugonjwa. Kiasili, tofauti za Watanzania hufungua mipaka katika dhiki, shida, ugonjwa, msiba hatuna tabia ya kuendeleza tofauti zetu wakati wa matukio tajwa. Ukiachilia Dr. Slaa ambaye hata Zitto amekiri, binafsi sikuridhishwa na ukarimu wa Viongozi wa juu wa CDM wakati Zitto akiwa katika hospitali za hapa ndani na sijaridhishwa nao pia hata baada ya kupelekwa nje ya nchi. Yawezekana sina taarifa na nimepitwa na mambo.....

  Imekuwa bahati mbaya kwamba mara nyingi majanga yanayowagusa viongozi wa juu wa CDM yanapotokea au kuelekea kutokea Mbowe huwa nje ya nchi au mbali na eneo la tukio. Japo hii inaweza kuwa inatokea kwa nasibu lakini kiubinadamu haileti tafsiri nzuri kama hafanyi zitihada za maksudi kuondoa utata anaporejea. Inatoa mwanya mzuri wa kueneza propaganda potofu juu ya tafsiri ya Mwenyekiti kutokuwepo katika matukio au kutoonekana akiwafariji waathirika. Mtakumbuka wakati wa ajali iliyosababisha mauti ya Mh. Wangwe M/Kiti alikuwa SA. Na sasa katika kuugua kwa Zitto binafsi sijaona ushiriki wake. Matukio haya machache yanajenga taswira mbovu ya kimausiano katika safu ya uongozi wa juu wa CDM na inatoa mwangwi (yawezekana usio sahihi) kwa jamii kuwa hawa si wamoja.

  Kuondoa utata huu nashauri uongozi wa CDM ufanye ziara rasmi India kumjulia hali Zitto. Na acheni ziara hii iwekwe wazi na vyombo vya habari. Hii itasaidia kukata mzizi wa propaganda potofu. Kiungwana, si jambo la kufanyia matangazo kwenda kumwona mgonjwa lakini kwa sababu hali ya kisiasa inalazimisha basi hamna budi kufanya hivyo.

  Haitakuwa vema hata kidogo, na rai yangu ni kwamba kiongozi yeyote wa juu hasa Dr. Slaa au Mbowe wasithubutu kwenda kumjulia hali Lema gerezani au mahakamani kabla ya kufanya Ukarimu huu kwa Zitto.
   
 2. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Omutwale
  Mbona tumeishaenda India na kurudi. Acha uchochezi wewe. Kwani Zitto kakutuma? Amesema nani hajaenda na nani kaenda?
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Baija,

  Sijatumwa na nina nia njema yawezakana tena kubwa kuliko ya kwako...

  Kama kuna kitengo goigoi ndani ya CDM basi ni kitengo cha HABARI. Yaani bila msaada wa wanachama na watu nje ya chama wenye kupendezewa na harakati za CDM huwezi kujua nini kinaendelea ndani ya CDM au kuna mpya gani. Mara nyingi Mh. Regia amekuwa akijarbu kuwafichia aibu hii ya udhaifu katika kuhabarisha umma. Nashindwa kuelewa Erasto Tumbo kazi yake nini? Mna gazeti Tanzania Daima badala ya kutoa taarifa kama hizi lenyewe limezama kwenye kumsafisha Lowasa na kumponda Sitta.

  Kwanza elewa vema hoja yangu. Nina hakika hutonishutumu.
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,015
  Trophy Points: 280
  acha upuuzi wewe, hiyo gharama ya kwenda India si wafungue matawi nchi nzima! Kwani huyo Zitto amesema anataka atembelewe na Mwenyekiti wa CDM? kati ya viongozi wa CDM na daktari yupi ni muhimu wakati huu wa ugonjwa wake?
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Omutwale nimekuelwa.
  Tatizo ni vigumu kuelewa nia yako unapoamua kuleta maswala haya hapa jamvini wakati unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja na hasa kwa masuala haya yaliyo nyeti. Ugonjwa wa mtu siyo kitu cha kufanyia Public Relations.
  Niwie radhi kama umeshtushwa na majibu yangu. Tutafutane.
   
 6. koo

  koo JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Niuhuni kutumia ugonjwa wa mtu kama mtaji wa kisiasa cdm sio chombo cha kihuni kunavitu vingi vya msingi vyakutangaza kuliko kujitangaza kwenda kumuona zito hilo limefanyika inatosha hakuna haja kujitangaza nape ndio anaweza kazi hiyo alienda igunga kuhani msiba akajitangaza huo ni uhuni
   
 7. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakiri mgando hizi, kwa hiyo Mbowe hasipoenda kumjilia hali Kabwe Zito ni tatizo? kama kweli hajaenda unafahamu kitu gani kimemzuhia? Dkt Slaa ni kiongozi wa ngazi ya juu chadema kwenda yeye kawakilisha chama kwa ujumla.
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu umenena vizuri tena sana na nadhani kwa nia njema tu ya kukisaidia CDM lakini kama kawaida naona unashambuliwa. sijui wapenzi wa CDM kwao jema ni lipi? Hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. kuna watu humu JF wanadhani wana haki milki ya CDM na hawataki kusikia CDM ikikosolewa. Hivi CDM okiingia madarakani itahimili matusi na uhuru huu tulionao humu wa kuwasema viongozi wa CCM na serikali yake? Napata tabu sana kwa jinsi wapenzi wa CDM wanavyopokea changamoto mbalimbali humu.
  Hivi ni siri kwamba kitengo cha habari cha CDM kiko mahututi na kinahitaji kijana wa kukihuisha? Kisiasa suala la mwenyekiti kuyoonekana akimtembelea Zitto wakati spika ameenda si zuri hata kidogo, linaweza kusababisha minong'ono isiyo ya lazima! Fanyieni kazi mawazo hayo mazuri. Siyo kila anayeikosoa CDM ana nia mbaya!
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,015
  Trophy Points: 280
  we usilete utaratibu wa Kikwete mwenye muda wa kutembelea kila mtu hospitali au kuhudhuria misiba yoote ikawa ndiyo lazma kila mtu afanye hivyo! Mbona Mkapa na Mwinyi walipokuwa wenyeviti wa CCM hawakuwa wanafanya hivyo? na huulizi?
   
 10. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nyie wapuuzi mtu anaeleza ukweli mnamuona mjinga. Mbowe alikuwa nje wakati wakifo cha wangwe ili kuua soo..zitto anautaka wenyekiti wa mbowe hivyo anakuwa ni adui wa mbowe. Ilivyokuwa wangwe aliutaka wenyekiti wambowe hivyo akapotezwa kwa njama za ajali
   
 11. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Soma tena mstari huu:
   
 12. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Rejea maelezo kwenye rangi nyekundu

   
 13. l

  luckman JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  we mtwale wa wapi?omurushaka au kanyigo, byazi au ishozi, kashasha au kamachumu!make najaribu kutafuta we ni wapi hasa!noyenda kwita obumo bwa banachadema??nowa yakutuma kyoma!noyendakisi!chadema ni chama imara, zitto hana neno na viongozi!akiwa muhimbili kila kiongozi na wanachama walienda kumuona labda wale ambao hawakuwa nchini!chadema sio chama cha matangazo kwamba kila wanachofanya lazima watangaze, cdm hawawafati waandishi warushe habari zao zilizo nyingi bali waandishi ndo wanawafata cdm!hizo ni sera za magamba!so tuache tuendeleze mapambano na mwish tutashinda!!!!!!!!!
   
 14. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huyu ni Omutwale wa Kanyigo.
  luckman, kila mara ninawakumbusha kutopenda kujifanya Wakatoliki kuliko Papa. Na kwa anayenisoma na kunielewa vizuri atabaini kuwa naloandika si uchochezi bali najaribu kuonyesha Udhaifu wa kitengo cha habari-CDM. Na pia najaribu kuwaonyesha nini athari ya kuuacha umma usipate habari sahihi na kwa wakati. Mnatuacha "kina Omutwale, MS and the like" tunaanza kujitungia za kwetu mara Ooh CDM wamtelekeza Zitto na kadha wa kadha. Dawa hapa si kumtusi Omutwale and the like bali kuangalia UDHAIFU uko wapi na kuufanyia kazi. Aliwahi kuandika Mwana JF- Umaraika wa CHADEMA Utakiua.
   
 15. l

  luckman JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  asante we kama mwanakanyigo,we ni wa kigarama, nshumba, lukunyu, kashenye, kigarama, bukabuye, bwanja, nyungwe!kikukwe, byazi au wapi!mi ninavyojua, chama ka chadema lazime kionekane threat kwa chama tawala na hila nyingi zitaibuka kukiangamiza, ni nawashukuru sana wanachadema popote walipo na viongozi imara chini ya mbowe kwa kuwa na msimamo wa dhati wa kwa kuonekana kutaka kumletea mtazania maedeleo yaliyopotea tangu aondoke muasisi mwalimu na kamanda wa ukweli muite sokoine! suala la zitto sio issue ka watu wanavyoliona!chadema walienda na wametoa tamko sasa sijui ni nani anayeendeleza uvumi wa namna hii kwamba hawakwenda kumuona!zitto bado ni asset kubwa ndani ya chama na sisi kama vijana tunamtegemea sana katika upambanaji wa kuleta maendeleo ya kweli na si ubabaishaji uliodumu tangu angatuke mwalimu!
   
 16. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  kama unamapenzi mazuri na cdm ungewatafuta viongozi husika ukawaeleza hilo swala kabla ya kulitundika sasa humu jf unadhani utaisaidia au unatafuta umbea
   
 17. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Heri yenu ninyi wenye ukaribu na hao viongozi. Mwenzenu nikiwatumia barua pepe hawajibu, nikiwapigia simu hawapokei ila nikiwaandikia hapa wachomoka waliko na marungu, matusi, na vimbwanga kibao.

  Hivi, injili ya Ukweli, Uwazi na Uwajibikaji ni kwa ajili ya kuikosoa ccm tu?
   
 18. L

  Lsk Senior Member

  #18
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....wachangiaji WENGI wa maada hii ukiwasoma vizuri unajua kuwa ni wana-CHADEMA kama mimi. Bahati mbaya sana wamemsoma mtoa maada juujuu mno na wakaishia kumshambulia. Jamani someni vizuri thread hii,huyu mtoa maada anakipenda chama. Mlio na namba za ma-tycoon wa CHADEMA wapigieni waambie waisome thread,kina Slaa wataielewa na kuifanyia kazi kwa ustawi wa CDM.
   
 19. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mwandosya,mwakyembe,chami na wengine wako india mbona JK hajaenda kuwaona?
  watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hasa wewe wa kanyigo!
   
 20. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Siongezi wala kupunguza neno. Maandishi ya kwanza hapo pekundu yanajitoshereza.
   
Loading...