Ni wakati gani utawala wa sheria huchukua mkondo wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wakati gani utawala wa sheria huchukua mkondo wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jul 27, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ningependa kufahamu ni wakati gani utawala wa sheria huchukua mkondo wake ilihali kumekuwepo na mlolongo mkubwa wa matumizi mabaya ya sheria kukiukwa makusudi ili kuweza kufanikisha lengo la wachache,napata taaabu sana kila napo jiuliza utawala huu wa sheria ni kwa ajili ya kuwakandamiza wanyonge tu na kuwalinda wakubwa au nini hasa mantiki yake.

  Utashangaa wanyonge wanapo nyan'ganywa ardhi yao,au wanapo vunjiwa majumba yao sheria kweli hufuata mkondo wakelakini linapokuja suala linalo wagusa wakubwa wenye meno makali sheria zinabaki kwenye makabrasha,hali kama hii inatufikisha wapi.

  Kwakuwa sisi ni waumini wa sheria iltakiwa ionekane sheria ina chukua mkondo wake kila idara bila kujali wala kubagua nani ni nani.Haiwezekani nchi yenyewe ni moja lakini sheria inagusa wachache na wengine wanakuwa untouchable.Tukiendelea kulifumbia macho jambo hili nchi yetu inakwenda kubaya na kusababisha wananchi kutokuwa na imani na serikali yao waliyoichagua.

  Ikitokea hali kama hii ya kutokuwa na imani na serikali iliyowekwa na wananchi kwa maslahi ya wananchi hatari yake kubwa ni Mungu tu ndiye ajuaye.

  Wananchi wamechoshwa kila mara kusikia taasisi fulani ndani ya serikali imekiuka sheria fulani ilihali watuhumiwa wanaonekana wako huru wanatanua mitaani ni hatari kubwa.Mbaya zaidi sheria hizo zimekuwa zikivunjwa kwenye mambo ambyo nyeti na yanagusa jamii husika moja kwa moja.

  Mahakama kama mhimili mwingine pamoja na Bunge navyo vimeingia kwenye mkumbo huu ulioikumba mhimili mwingine ambao ni serikali.Ikiwa hata mihimili mingine nayo ina shindwa kufuata sheria na kukubali kutumika kugandamiza demokrasia wananchi wake wakimbilie wapi.

  Hali kama hii ndiyo inayopelekea kuwaomba wana JF mjaribu kunijuza nami angalau nipate maana halisi ya utawala wa sheria,serikali imekuwa kila siku ikijinasibu serikali sikivu yenye kufuata utawala bora lakini ndani ya serikali hiyo hiyo kumekithiri uvunjaji wa makusudi wa sheria za nchi.Mambo mengi tu yametendeka pasi na kutia shaka kuhusu uvunjwaji wa sheria unao fanya na serikali yetu kupitia wizara na taasisi zake.

  Lengo hasa la mada hii ni kutaka kupata tafsiri sahihi juu ya utawala wa sheria na nini majukumu ya serikali katika kusimamia sheria hizo.Unapozungumzia utawala bora una maanisha nini.Unapo tumia power of appoint kuteuwa wale wale ambao wanvunja sheria kuna ashiria nini?

  Bwana mkubwa mmoja toka nchi za kaskazini mwa Afrika bwana Ibrahim Mo aliamua kuweka tuzo ili kuweza kuwanusuru viongozi wetu na nchi zao kama wakifanikiwa kuongoza na kufuata utawala wa sheria,lakini tuzo hiyo kwa kiongozi wetu inaonekana haina tija zaidi ya kubariki mali za Watanzania kudhulumiwa na walafi wachache.


  Naomba niishie hapa kwani matukio ni mengi ambayo ni viashiria vya kwenda kinyume na utawala bora ambao kwangu mimi naamini utawala bora ni utawala wa sheria,naomba majibu kwenu ili tuweze kuwauuliza viongozi wetu
   
 2. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Namna ya kuondoa "virus" huyu aliyeko kwenye "system" siyo kwa njia ya "scanning" tena, bali "compyuta" yenyewe (nchi) inahitaji kuwa "formated" na "installation" ya "operating system" mpya ifanyike. Hapo ndo utapata majibu unayoyataka. Vinginevyo kama "operating system" iliyopo itaendelea kutawala tegemea mabaya zaidi huko mbeleni.
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Sheria hufuata mkondo wake kwa masikini tu, kwa tajiri na sheria ni kama 2++ au 2-- poles.
  Lakini uko mkondo wa sheria mbadala kwa masikini, ile ya kujichukulia sheria mkononi mwake.
   
 4. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Yaliyo tokea leo bungeni ni hatari,miongoni mwa watunga sheria wetu ambao ni wawakilishi wa wananchi nao wameingia kwenye mtego wa kurubuniwa ili waweze kupindisha sheria kwa maslahi binafsi,mbaya zaidi hata wale wanao onekana kioo cha jamii nao wameuvaa mkenge.

  Tuna hoji kama mhimili huu wa bunge nao umegeuka kuwa fisadi wapi wananchi wataponea?
   
Loading...