Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,769
- 10,650
Ni kawaida katika zama hizi kuona kijana amejitegemea na kuwa na ghetto lake. Hali hii imedumu hata kufikia mahali wazazi kuwataka vijana wao hasa wa kiume kuondoka majumbani na kujitegemea. Jamii forums haibaki salama katika hili, mada nyingi zimeanzishwa humu kuwazodoa vijana wanaopindukia umri fulani kuendela kibaki majumbani mwa wazazi wao. Ukweli ukoje?
Hapo zamani vijana walilelewa kifamilia, wake kwa waume. Lengo lilikuwa kuwafunza stadi za maisha kulingana na kazi wafanyazo wazazi. Kijana angefundishwa kazi za baba mfano uvuvi, useremala, kilimo, ufugaji, biashara n.k. Baba angehakikisha anakuwa bega kwa bega na mwanae katika mambo yake yote. Ilitarajiwa kuwa mwishowe kijana huyu angekuwa na ujuzi wa kutekeleza hayo na zaidi ya hapo, kwani huo ulikuwa ni msingi na unajengwa kuwa tabia ya kijana huyu. Kwa mfano kile wanachofanya jamii ya wahindi leo sio bahati mbaya. Ni utaratibu ambao wamekuzwa nao, na kitu ambacho tumeshindwa kung'amua na kubaki tunawashangaa, wakati ukweli ni kuwa huu uataratibu sio mgeni. Naam, ndio huo huo utaratibu tulioukataa sisi na kukimbilia kuiga akina Puff dady. Kijana angeweza kufanya majukumu ya baba peke yake (kasoro ngono) kuhesabiwa kuwa anatosha kuoa na kujitegemea. Alipimwa uwezo wake wa kufanya maamuzi kutatua changamoto mbalimbali pasipo kumtegemea baba. Mfano wasukuma wana kitu kinaitwa nsumba ntale.
Mabinti nao walilelewa katika mazingira ya kujifunza majukumu ya mama kwenye familia. Hii ilianzia nyumbani mpaka kwenye kazi za kiuchumi. Mfano kama familia ni ya wakulima, familia nzima ingeenda shamba alfajiri, ikifika muda fulani, mara nyingi saa tano, mama na binti zake wangeondoka shamba kwenda kusenya kuni na kuchota maji, huku baba na vijana wakiendelea kulima. Muda wa chakula baba angerejea na vijana wake nyumbani ama chakula kingeletwa shamba. Haya ni mafunzo ya mgawanyo wa majukumu katika familia. Binti angetarajiwa kumudu kutekeleza majukumu ya malezi ya familia kiasi kwamba hata mama asipokuwapo mambo ya nyumbani yanakwenda vema kabisa. Binti wa namna hii alisemwa kuwa tayari kwa majukumu ya ndoa.
Wakati hapo zamani ilikuwa fahari kwa kijana kujitambulisha kwa uhodari wake katika kazi za kiuchumi, leo hii ni fahari kujilinganisha na akina Ja rule. Kama taifa na kama jamii tumepotea. Ungekuta kijana wa miaka 10 anamiliki ekari 5 za mazao ya biashara chini ya uangalizi wa wazazi wake. Kina Mo Dewji hawakutokea tu hewani, ni mfumo uliowaleta hapo walipo sasa. Kina Manji wametengenezwa na wazazi wao. Hebu jiulize wewe mzazi wa zama hizi anamtengeneza mtoto kuwa nani? Mfumo huu ulileta jamii toshelevu, sio kwamba ilikuwa tajiri hapana, ila mahitaji ya msingi yalipatikana muda wote. Hata waliopata utajiri walijiongeza kupitia mfumo huu.
Elimu ilipaswa kumjenga kijana awe na wigo mpana wa kufikiri namna bora ya kuendesha shughuli za kila siku. Haikupaswa kuwa mbadala wa kile kijana anachokipata kutoka kwa wazazi wake. Badala yake elimu imekuja kuandaa vijana wa kutumika maofisini na viwandani. Kama huamini tazama ni wahitimu wangapi wa vyuo wanashinda mabarabarani na vyeti vyao wakitafuta ajira. Ama tafuta humu JF ni mada ngapi zinauliza kampuni inayolipa mshahara mzuri. Elimu imetukomboa kutoka Ujima na kutuingiza kwenye ujinga. Hatufikiri tena ila kila kitu tukifanyacho tunafuata kanuni zilizoandikwa na wasomi waliotangulia. Tumegeuzwa mabingwa wa kukariri na kutoa reference za maisha ya ulaya. Hatutofautiani sana na maroboti. Elimu yetu imetuandaa kuwa watumwa, ingawaje siku hizi kuna neno tamu kidogo, waajiriwa. Wapo ambo elimu imawawezesha kujiajiri, mfano madaktari, waalimu nk. Hao wametumia elimu yao kukamata fursa katika jamii.
Tukirejea kwenye mada, kijana alipofikia umri wa kuoa (yaani uwezo wa kujitegemea), alitakiwa ajiandae kuanza maisha mapya. Wazazi walimsimamia katika hili n kuhakikisha kuwa anajiweka tayari kupokea majukumu. Ni wazazi ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua kwamba kijana amefikia umri sahihi kwke kuoa. Ama wangemshauri aoe, ama angeomba mwenyewe ruksa ya kuanzisha familia yake. Mpaka hapo bado alikuwa mikononi mwa wazazi. Ndipo sasa taratibu zingefanyika za kuposa, ikiwa ni pamoja na wazazi kumuuliza kama jicho lake limepata kuona mahali ambapo kuna binti wa kumfaa. Kama hajawahi wazazi wangempa machagua kadhaa kadri walivyoona tabia na mwenendo wake, na kuoanisha na tabia na mwenendo wa familia ya binti yule, ili waendane.
Idhini ya kijana kuondoka kwenye familia yake na kujitegemea ilikuwa ni kuoa. Kijana akipata mke tayari hapawswi tena kukaa nyumbani kwa wazazi wake, isipokuwa kwa baadhi ya jamii zenye mfumo wa kuishi pamoja kama boma. Huo ndio ulikuwa wakati sahihi kwa kijana kuoa, tofauti na ilivyo sasa. Kwa misingi hii ndoa hazikuwa tendo lla kubahatisha kama ilivyo leo. Ndoa ni mfumo wa kikanuni ambao unawawezesha mke na mume kudumu kwa muda mrefu huku kukiwa na asilimia ndogo ya kuachana. Mfumo huu tumeukataa na kujidai kuiga mfumo wa kimagharibi, kitu ambacho ni machukizo makuu.
Kwa wakristo wengi hawajui kwamba hata Mungu hajamruhusu kijana kujitenga na wazazi wake isipokuwa tu awe ameoa. Hata binti ni ndoa tu itakayomtenga na wazazi wake. Kumekuwa na mafundisho potofu katika zama hizi kwamba kijana wa kiume mwenye miaka 18 ajitegemee na ni aibu kuishi kwa wazazi. Ni mafundisho potofu na yamekuwa chanzo ku kuharibu vijana wengi.
Itaendelea......