Ni wakati gani huwezi kumuadhibu mkosaji?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,780
Sisi sote ni uzao wa damu na nyama.. Uzao huu si kamilifu.. Hivyo makosa hayaepukiki popote
Makosa wanafanya wengi na kila mmoja wetu anakosea kwa viwango vyake.. Kuanzia udogoni mpaka ukubwani.. Watoto huchapwa, hufinywa ama hupewa adhabu nyingine mbadala kulingana na umri, aina ya kosa na mtoa adhabu
Adhabu zipo za kila aina kwenye jamii yetu..
Zipo majumbani
Zipo mashuleni
Zipo vyuoni
Zipo makazini
Zipo barabarani
Na ili kudhibiti makosa na adhabu zake kila Taifa lina taratibu zake, makosa yake na namna zake za kuadhibu.. Lakini vyovyote iwavyo kuna mazingira hatuwezi kutoa adhabu popote! Labda tu liwe ni kosa lisilovumilika... Mazingira hayo ni yepi?
. Mbele ya wageni nyumbani
. Mbele ya shughuli maalum
. Ikiwa ni siku maalum ya mkosaji nknk
Ukikurupuka kuadhibu hapo mbele ya wote tatizo linakuwa lako na si la mkosaji
Huwezi kumuadhibu mtu siku yake ya kuzaliwa, siku yake ya kipaimara, siku yake ya kufuzu daraja fulani, siku yake ya harusi nknk

Miaka ile ya 90 kuna mtuhumiwa aliruka dhamana na akahukumiwa bila kuwepo mahakamani.. Vyombo husika viliendelea kumtafuta zaidi ya mwaka na kuja kumpata siku ya harusi hapa hapa Dar... Walichofanya wakamsubiri mpaka akamaliza shughuli yake ya harusi kuanzia kanisani mpaka ukumbini...
Ni wakati anatoka kwenda honey moon baada ya sherehe kwisha ndio askari wakamtia nguvuni na kumpeleka moja kwa moja gerezani kutumikia kifungo chake

Waziri wa utalii kafanya kituko ambacho kimetafsiriwa kama kituko cha karne.. Ni wakati wa kutoa vyeti kwa ma luteni usu baada ya mafunzo mbele ya wageni waalikwa na mbele ya waandishi wa habari..
Haikuwa uungwana
Haikuwa sahihi
Haukuwa utu
Hayakuwa maadili
Kigwangala alikuwa na nafasi ya kutoa adhabu husika ama nyingine baada ya shughuli ile... Picha aliyoonesha ni kielelezo cha kukosa kufahamu kama kiongozi anatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani...!!?
Huyu ni waziri mwenye dhamana ya wizara muhimu kama hii.. Je kama kayafanya haya hadharani mbele ya kadamnasi je ya huko sirini anafanya mangapi?

Jr
 
Ninadhani ametoa adhabu kujinadi hasa Kwa namna ya mfumo ulivyo kwa sasa (politics)

Amelitumia jukwaa kwa faida yake binafsi pasipokujari nafasi (haki) ya muazibiwa

Amepuyanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutoa adhabu ni kitendo chenye kuhitaji target Sana kwani ukikosea ni muda gani utoe adhabu inakosa ile positive results kutoka kwenye hiyo adhabu mfano ndo kwa huyo kigwangala

Kuna Aina flani flani kama kujionyesha kuwa yeye ni mwamba, kuwadharau wengine na Aina flani ya majivuno

Hii inafanya pia watu kuona Kama uongozi huu umekaa kutaka sifa maana matukio ya mfano wa hivi yamekua yakionekana hapa na pale

Lastly inabidi wajue kwamba uongozi ni dhamana na pia wakati si milele (hawezi kudumu kwenye hiyo nafasi)
Kuna muda utafika itabidi aachie na ajue Hana Kinga kikatiba anayemwiga anayo Kinga kikatiba

  • Thanks
Reactions: a45
Kigwangala ana inferiority complex na nadhani kuna watu anajaribu kuwaprove wrong kua he has made it.
 
Back
Top Bottom