Ni wakati gani haturuhusiwi kuamulia ugomvi wa mme na mke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wakati gani haturuhusiwi kuamulia ugomvi wa mme na mke?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by KIDUNDULIMA, Oct 14, 2010.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Leo usiku jirani yangu katoa kichapo cha nguvu kwa mwamamke wake (nyumba ndogo yake). Mwanamke kapiga mayowe kuwa jamani nisaidieni nakufa. kweli watu tukatoka mbio na tulipofika tukakuta mwanamke anavuja damu na mwanamme anamburuza mwanamke kumpeleka mahali kusiko julikana. majirani zangu walisimama pembeni kimya wakitazama tu.

  Nilipofika nikauliza kulikoni. Yule mwanamme akasema nimuulize mkewe aseme nani kamlipia kodi ya nyumba wakati yeye hajampatia hiyo hela. nilipomuuliza mkewe jamaa kanibadirikia nakuanza kunitukana, mara ho naingilia mambo yasiyonihusu. Mbaya zaidi mkewe alikuwa anakataa katakata kuondoka akisema kuwa huko anakotaka kumpeleka atakwenda kumuua. Mi kuona vile nikamwambia jamaa kuwa nakwenda kumwita mjumbe. Jamaa akasema kuwa hatishiki na mjumbe na hawamfanyi lolote.

  Kweli mjumbe (mjumbe mweenyewe hana hiyana maana ni baunsa na alipofika tuu alitoa mkwala mzito kwa jamaa kuwa kwa nini anasumbua watu usiku wa manane) Jamaa alinyong'onyea na kuanza kuomba msamaha. Akasema kuwa ni kiloba kimoja cha konyagi kimemfanya afikie kufanya ukatili wa namna ile. Mjumbe aliwasii jamaa na mwanamke wake warudi ndani, lakini mwanamke aligoma akalala nje mpaka asubuhi. mwanamme hasira zilipomuisha alirudi kumbembeleza mwanamke, mwanamke akakubari kurudi ndani na stori ya huko ndani hakuna anaeijua.

  Ndipo ninapo uliza ni wakati gani tusiingilie ugomvi wa mme na mke na huku kukiwa na taarifa lukuki za wanawake kuuawa na kuwekwa ulemavu wa maisha.

  karibuni wana JF tujadiri
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Unaikumbuka hii "Ndugu wakigombana shika jembe ukalime" Hiyo ndo maana yake. Usithubutu kuingilia ugomvi wa mke na mume, Kuna mtu mmoja aliwahi kuniambia ugomvi wa mke na mume msuluhishi wake KITANDA.
   
 3. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Even pale mtu anapoomba msaada wa kuwaidiwa asisaidiwe?
   
 4. Mpenzi

  Mpenzi Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona hakuna haja ya kutomsaidia mtu wakati anapigwa, What if huyo mtu anapigwa hadi anakufa kisha wewe unaangalia tu? Kidundulima umefanya kitu cha maana na unastahili pongezi, Huu ni ujinga mwanaume kumpiga mwanamke nor it is acceptable for any woman to do that either! Hakuna haja ya kubeba jembe ukalime, Msaada ni msaada na nisingependa kuona kipingamizi cha kutomsaidia mtu wakati wa ugomvi.:A S thumbs_up:
   
 5. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wengine hutamani kupigwa...unaweza enda amulia...mwanamke anakwambia mwache anipigi mwache anipige hafanyi effort za kujinasua...kesho anasimulia kwa wenzie mume wake anampenda...kapimpiga jana kisa...kodi ya nyumba ....wewe una nafasi gani ya kutaka kuingilia.Dah haya mambo...ni kuyaangalia kwa umakini wa hali ya juu sana...kabla ya kuyakurupukia.
   
 6. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  huyo anayesema mwache anipige sidhani kama atapiga mayowe ya kuomba msaada wa kuokolewa.
   
Loading...