ni wajibu wangu kuiombea nchi yangu (Tanzania) nawewe ukiwa mzalendo unawajibu huo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ni wajibu wangu kuiombea nchi yangu (Tanzania) nawewe ukiwa mzalendo unawajibu huo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by binti ashura, Apr 18, 2011.

 1. b

  binti ashura Senior Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kuliombea taifa kila mtu anawajibu huo mimi huwa naliombea na sina kanuni kuwa leo nitasema nini mfano sasa nasema hivi
  `BABA YANGU WA MBINGUNI ULIENIUMBA MIMI NA WATANZANIA WENZANGU, NA UMETUUMBA KWA MFANO WAKO KAMA INAVYOSOMEKA KATIKA KITABU CHA MWANZO 1:26 KUWAULIMFANYA MTU KWA MFANO WAKO, MUNGUNAKUOMBA UTUJARIE AFYA NJEMA SISI WATANZANIA ILI TUWEZE KULITUMIKIA TAIFA LAKO VEMA, MUNGU TUNAOMBA UTUPE UPENDO ILI TUPENDANE SISI KWA SISI, MUNGU TUKUMBUKE SISI POPOTE TUNAPOKWENDA KINYUME NA MATAKWA YAKO, ILI TUWEZE KUKUTUMIKIA WEWE MUNGU KWAKUPITIA NJIA NYINGI KAMA VILE KUITUMIKIA SERIKALI KWAKUWA UMESEMA KATIKA BIBLIA KUWA HAKUNA MAMLAKA ISIYOTOKA KWAKO, BABA MUNGU NAKUSIHI UMJALIE RAISI WETU JAKAYA MRISHO KIKWETE ILI ATUONGOZE VEMA, NAMUOMBEA PIA NAMAKAMU WAKE ILI AWEZE KUTIMIZA WAJIBU WAKE WA KUMSAIDIA RAIS WETU, BABA MUNGU NAKUOMBA NA NINAKUSIHI MPE HEKIMA RAIS WETU ILI ATUONGOZE KADRI UPENDAVYO, NAAMINI MUNGU WANGU KUWA NDIYE KICHWA CHA FAMILIA YA TANZANIA, NDIYE MSEMAJI MKUU WA TANZANIA, NAKUOMBA PIA MUNGU BABA WAMBINGUNI UMPE HEKIMA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KWAKUWA YEYE PIA ANAMAJUKUMU MAZITO, BABA MUNGU NALIOMBEA TAIFA LETU LISIWE NI TAIFA LA MFANO KWA UMASIKINI BALI LIWE MFANO KWA UTAJILI, MUNGU NAJUWA HUKUTUUMBA TUWE MASIKINI, BALI ULITUUMBA TUISHI MAISHA YANAYOKUTUKUZA, BABA MUNGU NAKUOMBA UWAKUMBUSHE MAWAZIRI KUWA WAWE NA KAULI MOJA NA RAIS WETU, ISIWE KAMA WANAJENGA MNALA WA BABELI, MUNGU BABA NAKUOMBA UWAPE MAISHA MALEFU WABUNGE WOTE, RAIS PAMOJA NA MAKAMU WAKE, BABA MUNGU, NAJUWA WEWE NDIWE UWEKAE VIONGOZI WETU KWAKUWA WEWE WAJUWA NANI ANAEFAA KUTUONGOZA BILA KUJALI DINI YAKE, KABILA LAKE, CHAMA CHAKE, UPANDE WA NCHI AU MKOA AU WILAYA ATOKAKO, JINSIA YAKE, RANGI YAKE AU KAZI YAKE, NAAMINI KAZI AIFANYAYO MTU HAIWEZI KUMFANYA AWE KIONGOZI MZURI AU MBAYA, MUNGU BABA NAMUOMBEA MBUNGE WANGU ABDRAZZI ABOOD, ILI AWEZE KUTUWAKILISHA VEMA, NA NAMUOMBEA DIWANI WETU NA MWENYEKITI WA KITONGOJI, KWAKUWA WOTE WAMEWEKWA KWA KWA MUJIBU WASHERIA ILIYOWEKWA NA WATANZANIA KUPITIA WAWAKIRISHI WAO (WABUNGE) MUNGU BABA NAIOMBEA FAMILIA YANGU, NAKUOMBA MUNGU WA REHEMA UWABARIKI NDUGUZANGU NA MAJIRANI ZANGU KWAKUWA WANAMCHANGO MKUBWA KATIKA MAISHAYANGU KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE, NAKUOMBA MUNGU WAIBRAHIMU, MUNGU WA ISAKA, NA MUNGU WA YAKOBO NAKUSIHI WABARIKI WATANZANIA, MUNGU WAMENISAIDIA MNO KWA KWAKIASI AMBACHO NASHINDWA NAMNA YA KUWASHUKURU, E MUNGU BABA, WAJARIE WATANZANIA , KWAKUWA WAMENISOMESHA KUANZIA DARASA LA KWANZA MPAKA CHUO KIKUU, MUNGU NITAWALIPA NINI KWA KILE WALICHONIFANYIA, MUNGU NITAWAFANYIA NINI ILI WAJUE KUWA MIMI NAWAJALI NA KUWAHESHIMU KWAKILE WALICHONIFANYIA! MUNGU BABA UNAJUWA MIMI WATANZANIA KUPITIA KODI ZAO MIMI WAMENIWEZESHA KUWA MTU KATI YA WATU, MUNGU TAZAMA KILANINACHOKIFANYA NAHISI BADO NADAIWA NA WATANZANIA KWAKUWA KUPITIA SERIKALI YAO MIE WAMENIFANYA NIWE MTU KATI YA WATU, BABA MUNGU, NAWAPENDA WATANZANIA, NAWAPENDA VIONGOZI WANGU, KUANZIA MWENYEKITI WA MTAA MPAKA RAIS ALIOKO MADARAKANI NA WALIOKWISHA KUONDOKA MADARAKANI, HATA WALE WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI NAKUOMBA UWALAZE MAHALI PEMA PEPONI KWAKUWA WOTE WANAMCHANGO KWANGU, NAAMINI HATA WATAKAOZALIWA KESHO NAO WANAMCHANGO KWANGU KWAKUWA KWANAMNA MOJA AU NYINGINE, SERIKALI ILIKOPA KWAAJILI YANGU, HIVYO HATA VIZAZI VIJAVYO VITAHUSIKA KUNILIPIA MADENI YALIYOKOPWA KWAAJILI YANGU, MUNGU TAZAMA WATANZANIA WALIVYO MASIKINI, LAKINI WALINIWEZESHA MIMI KUWA MTU, NATAMBUA KILA MTU AMECHANGIA KUWA VILE NILIVYO SASA, MUNGU BABA NAKUSHUKURU KWAKUWA UNAILINDA MIPAKA YETU, MUNGU NAKUAHIDI NITAKUTUMIKIA KATIKA HALI ZOTE, MUNGU NAKUAHIDI NITAWATUMIKIA WATANZANIA KWAKUWA WANASTAHILI HESHIMA KUTOKA KWANGU, MUNGU BABA NAKUOMBA, UWAJAARIE WAAFRIKA WENZETU, WAISHI KWA AMANI KAMA SISI TUISHIVYO KATIKA NCHI YETU,BABA MUNGU NAKUOMBA UTULINDE ZIDI YA MAJANGA MBALIMBALI KAMA VILE, NJAA,UKOSEFU WA UMEME, MAGONJWA KAMA VILE UKIMWI, KANSA, KISUKARI, NA MAGONJWA MENGINE YANAYOTIBIKA NA YASIYOTIBIKA, BABA MUNGU, NAJUWA WEWE NI MWAMINIFU, NA UNAUWEZO JUU YA YOTE, EMUNGU TAZAMA VIONGOZI WETU, WATUMIE ILI WATUONGOZE KWA KUKUWAKIRISHA WEWE MUNGU WA MBINGUNI, MUNGU WA BARAKA TUBARIKI WATANZANIA KAMA ULIVYOWABARIKI IBRAHIMU, ISAKA, NA YAKOBO, NATAMBUA KUWA UNAKWENDA KUTENDA, MUNGU BABA UNAJUWA KUWA MIMI KILA NIMUONAPO MTANZANIA NAMUONA KAMA MZAZIWANGU NA KAMA MLEZIWANGU BILA KUJALI UMRI WAKE NA UPANDE AU MKOA ATOKAKO, NI KATIKA UTATU NAOMBA NAKUSHUKURU AMENI``.

  Mimi naamini katika utatu kwakuwa kutoka agano la kale mpaka agano jipya yote yanaonesha mungu ananafsi zaidi ya moja. MFANO MWANZO 1:26 inasema `MUNGU AKASEMA, NATUMFANYE MTU KWA MFANO WETU,KWASURA YETU;WAKATAWALE SAMAKI WA BAHARINI,NA NDEGE WA ANGANI, NA WANYAMA NA NCHI YOTE PIA NA KILA CHENYE KUTAMBAA KITAMBAACHO JUU YA NCHI`

  hivyo ndivyo ambavyo naliombea taifa langu.
  ushauri wangu tu kwamtu ambae ni mzalendo ataiombea nchi yake, pia uonapo serikali haifanyi vile unavofikiria , waombee viongozi kwakuwa nao niwatu. unaweza kuona kiongozi uliyemtaka hakuchaguliwa ujue yule aliyepita ndiye mtu sahihi kwa wakati ule huyo unaemtaka mudawake bado au hafai kuliko kuliko yule aliyepita. kwasasa hakuna Rais anaeweza kufaa zaidi ya kikwete! na kwa awamu ya tatu Mkapa alifaa na kikwete aliambiwa mudawako bado.
   
 2. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa moyo huu..keep it up,
  Tutakuunga mkono muda si mrefu, tunaomba tena na kesho uje uporomoshe maombi hapa, naona ni njia iliyobaki kulinusuru taifa hili na roho chafu za udini, ufisadi na kutokuwajibika.
  Ninaamini huyo Mungu unayemuamini atatengeneza njia pasipokuwa na njia.
  Na iwe hivyo.
   
 3. k

  kituro Senior Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mie natamani niongozane na viongozi kazaa ili akawaombee! kwakuwa huyu ndugu nazani anaumia sana na watanzania pia anaipenda nchi yake! inabidi tumuombe atufundishe tuliowengi ili tuipende bongoland yetu!. amini usiamini kama kungekuwa na watu watano kila mkoa wanaolitakia mema taifa kama huyu mtu, nchi ingekuwa nzuri sana. nahisi huyu mtu anastahili nae kuombewa ili awe na mda wa kutuombea na sisi!.
   
 4. M

  Mary Glory Senior Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  binti ashura God bless you.let us pray for our nation.ndo njia iliyobaki ya kutatua matatizo yanayoikabili nchi yetu.keep it up mamii.
   
Loading...