Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,563
- 729,449
Changamoto za maisha na kutaka kutimiza ndoto nyingi mapema ujanani au uzeeni huwafanya wengi kutaka kupata pesa nyingi za haraka kwa namna yoyote ile...!ila kumbuka NO EASY MONEY...!hakuna pesa rahisi labda iwe hii tu ya kubadilishia mboga
Pesa za fasta nyingi na zisizo na maelezo wala misingi ya kueleweka ni pesa za masharti ni pesa za maagano ni pesa za viapo ni pesa za kuzimu na hupatikana kwa kubadili na damu...wengi wanaishi na mateso ya kimyakimya kutokana na kupata pesa za namba hii
Halafu zinakuja pesa za kichawi...jamaa anakuita ndani anashikashika madawa yake kisha anashika rundo la magazeti ambayo yanageuka pesa..!hiki ni kiini macho..ni pesa inayohitaji kuhalalishwa ili idumu, lakini kwakuwa mganga hawezi kuihalalisha atakwambia uweke zako kadhaa uchanganye na zile ili ziongezeke maradufu...! Wengi hupigiwa hapa!!!kinachofuata pale ni mganga kuchukua pesa yako halisi na kukuachia ya maruhani ambayo lifespan yake ni chini ya masaa 24
Kuhalalisha wizi/utapeli wake atakupa masharti mengi magumu ili ukirudi kwake akwambie ulikosea masharti
Kama yeye angekuwa na uwezo wa kupata pesa ya bure asingehangaika na za kwako
Please take Good care no easy money