Ni vyuo gani wanaopokea wale waliohitimu foundation program Open University?

mwanakijiji lugusi

Senior Member
Apr 13, 2016
128
96
Wakuu poleni na majukumu naombeni kuuliza ni vyuo gani mpaka sasa wanaopokea wale waliohitimu foundation program open university? Coz mpaka sasa mambo hayaeleweki kabisa nahisi open wametutapeli na kutupotezea muda na ada zetu
 
Ninachojua ukifanya Foundation Program Chuo flani huwezi kwenda kusoma degree Chuo kingine, kumbuka hizo Program zinakuwa zimeandaliwa kutegemeana na mfumo ya Chuo husika, huwezi kusoma Foundation Program Open ukaenda kusoma degree UDSM, na huwezi kufanya foundation program UDSM au Mzumbe ukahamia Open, ndio maana inaitwa Program
 
wakuu polen na majukumu naomben kuuliza ni vyuo gani mpaka sasa wanaopokea wale waliohitimu foundation program open university? Coz mpaka sasa mambo hayaeleweki kabisa nahisi open wametutapeli na kutupotezea muda na ada zetu
Foundation ni program inayokupa sifa ya kusoma shahada kama hukupata alama stahiki za kujiunga chuo kikuu. Unatakiwa uwe na GPA ya kuanzia 3 ya foundation ili uweze kuomba udahili chuo kikuu.. Ukiwa na GPA hiyo na kuendelea uko huru kuomba udahili chuo chochote.
 
Kwa muktadha wa kisiasa (hasa za ccm) uko sahihi. Ila kitaaluma BIG NO!
 
Foundation haina tofauti na resitting ambayo humpa mwanafunzi fursa ya ku make up pale aliposhindwa awali.
 
Wakuu vipi mitihani ya foundation ikoje kwa watu wa sayansi?
 
Foundation ni program inayokupa sifa ya kusoma shahada kama hukupata alama stahiki za kujiunga chuo kikuu. Unatakiwa uwe na GPA ya kuanzia 3 ya foundation ili uweze kuomba udahili chuo kikuu.. Ukiwa na GPA hiyo na kuendelea uko huru kuomba udahili chuo chochote.
Foundation program inatambuliwa na TCU kama njia moja ya kuingia chuo kikuu kusoma degree ya kwanza, soma "Undergraduate Admission Guidebook for 2019/2020 Academic Year (For Holders of Form Six Qualifications)" Mambo yanaharibika ukiingia chuo kimoja kimoja, utakuta ni Open University peke yake walio iweka Foundation Program yenye GPA=3 kama kigezo kimoja wapo cha kuombea. Hii ina maanisha kuwa vyuo vingine BADO havija itambua kama njia ya kuweza kuomba udahili. Sijui huko mbeleni, labda kama watu watapiga kelele na kusikika.
 
Tangu foundation course ianze kutolewa na chuo kikuu huria 2016 hakuna waliohitim na wakaomba chuo kingne il waje watoe ushuhuda??
 
hata guide book ya tcu hakuna sehem walipozungumzia foundtion program
Si kweli mkuu, TCU wanaifaamu OFC na ipo kwenye guide book Kama sifa moja wapo ya kusoma degree, Ila kwenye vyuo vingi hawajaiweka OFC kama entry qualification yao kuweza kusoma degree zaidi ya open university wenyewe, hivyo sio lazima ukasome vyuo vingine Hata open university uliposoma OFC ni chuo, tena na degree yako ina kuwa accepted Kama za vyuo vingine.
 
Tangu foundation course ianze kutolewa na chuo kikuu huria 2016 hakuna waliohitim na wakaomba chuo kingne il waje watoe ushuhuda??
Hakuna mkuu usipate Tabu kupata Ushuuda, vyuo vingine vyote sifa za kujiunga na vyuo vyao kwa ngazi ya degree ni uwe Umemaliza form six au diploma, OFC bado Hawajaiweka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom