Ni vyema tukumbuke kuomba na kumshukuru Mungu wana JF

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,373
Ni jumatatu nzuri iliyojaa neema za Mungu wetu .

Si vibaya tukiwa katika kujadili siasa,mapenzi na maisha kwa ujumla tusiache kumkumbuka muumba wetu na kumshukuru kwa wema na fadhira zake anazoendelea kutujaalia siku hadi siku ni mapenzi makuu na ya ajabu kujitoa kwetu.

Kwa mimi Binafsi napenda yeyote aliye na nyimbo hizo hapo chini atuwekee ili tuendelee kupata baraka zake:

1. Upendo Nkone - Unitetee
2. Rose Mhando - Eee mungu nitakushukuru

Mbarikiwe na bwana kutoka katika kitabu cha Zaburi na Mithali

Mithali 22:1-16

Zaburi 142:1-7
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=7U17MapqV1k[/ame]

Nadhani wimbo wa Rose Mhando ndio huo...

Ubarikiwe sana...
 
Taifa letu nalo tusilisahau kulimbea.si unajua mtabiri kasema uchaguzi hautakuwepo? sasa inabidi tuvunje hizi nguvu kwa KWA JINA LA YESU.
"sema amen.....
 
Amen,kweli mungu ni mwema tena si binadam hata aseme uhongo,Ubarikiwe mwanamke wa kwanza
1.Uliniumba nikuabudu
2.Yahwe uhimidiwe

thanx my dear Pearl hope jana ulikuwa church ...Ubarikiwe
 
Mimi, naam, Mimi, ndimi NIYAFUTAYE makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala. SITAZIKUMBUKA dhambi zako Unikumbushe na tuhojiane eleza mambo yako upate kupewa haki yako." Isaya 43:25-26
 
MUNGU baba muumba wa mbingu na nchi!

Asubuhi hii sisi wanao kwa unyenyekevu mkubwa tunakujia mbele ya uso wako tukitanguliza shukrani, kwa kutajalia uhai na afya njema na kutupendelea kuiona siku hii ya leo!

Sifa na utukufu tunakurudishia wewe Baba wa Mbingu na nchi!

Mungu baba wa mbingu na nchi tunaisogeza nchi yetu Tanzania; nchi ya maziwa na asali miguuni pako; tukiwaombea afya na nguvu wanachi wake wote! baba kaisimamiae nci yetu tunakulilia wakati huu inapoelekea kwenye mchakato wa uchaguzi; ukasimamie busara za watanzania ili wale wataokachaguliwa wakapate kibali machoni kwako na wakafanyike baraka na matunda ya uamifu yao yakaonekane miongoni mwetu ; ukawakumbushe baba baba viongozi watakochaguliwa kuwa wanatawala kwa niaba yako na sio kwaniaba yao binafsi na jamaa zao kwa maana tunaamini kuwa mamalaka na sheria ni vitu vitokavyo kwako!

Zaidi ya yote Mungu baba wa mbingu na nchi ukaijalie nchi yetu tukufu amani zaidi na mshikamano zaidi baina yetu Watanzania, ukatuajlei kupiga hatua za kimaendeleo na kujikwamua katika madhila mbalimbali yanayotulemea sasa!

Tunaomba yote katika jina lako tukufu

Amen!
 
Ni jumatatu nzuri iliyojaa neema za Mungu wetu .

Si vibaya tukiwa katika kujadili siasa,mapenzi na maisha kwa ujumla tusiache kumkumbuka muumba wetu na kumshukuru kwa wema na fadhira zake anazoendelea kutujaalia siku hadi siku ni mapenzi makuu na ya ajabu kujitoa kwetu.

Kwa mimi Binafsi napenda yeyote aliye na nyimbo hizo hapo chini atuwekee ili tuendelee kupata baraka zake:

1. Upendo Nkone - Unitetee
2. Rose Mhando - Eee mungu nitakushukuru

Mbarikiwe na bwana kutoka katika kitabu cha Zaburi na Mithali

Mithali 22:1-16
Zaburi 142:1-7

Hii inaonyesha jana madhabahu iliwaka moto. Wapi huko ukikoshukiwa na Roho wa Bwana, akakujaza nguvu nawe ukawa shahidi wake katika JF yote,uyahudi, samaria na hata mwisho wa nchi Matendo 1:8
 
Train a child in the way he should go,
and when he is old he will not turn from it.
Nimeipenda hiyo verse. It is the source of all problems we have now. Our children...let us go back to the word parents!!!
Thanks for the inspiration FirstLady! Ubarikiwe sana...
 
Thanks FL1, this is very useful, mara nyingi huwa rtunatingwa na makashkash ya maisha tunasahau hata kumuomba na kumshukuru Mungu. Mbarikiwe wooote hapa JF, na kwa wazazi wote msisahau kuwafundisha watoto kusali hata kama ana 2years so long as anaweza kuongea hakikisha unasali nae kabla hajalala, huku akifuatisha unavyosema, na hakika mtoto atakuwa katika mwenendo ulio bora.
 
Hii inaonyesha jana madhabahu iliwaka moto. Wapi huko ukikoshukiwa na Roho wa Bwana, akakujaza nguvu nawe ukawa shahidi wake katika JF yote,uyahudi, samaria na hata mwisho wa nchi Matendo 1:8

Siku zote nakuwa katika maombi lakini naona kama ni vyema tuwe tunakumbushana wana JF na pengine popote pale ,najua tunatingwa na pilika za maisha lakini ni vyema tumkumbuke yeye alietuumba

Ninja ubarikiwe
 
Thanks FL1, this is very useful, mara nyingi huwa rtunatingwa na makashkash ya maisha tunasahau hata kumuomba na kumshukuru Mungu. Mbarikiwe wooote hapa JF, na kwa wazazi wote msisahau kuwafundisha watoto kusali hata kama ana 2years so long as anaweza kuongea hakikisha unasali nae kabla hajalala, huku akifuatisha unavyosema, na hakika mtoto atakuwa katika mwenendo ulio bora.

Ni kweli Carmel ni vyema kuwakuza watoto wetu katika misingi ya dini
ili kuwajenga na kuwaweka sawa kiimani
 
Mungu ni Pendo anapenda watu!

Ni kwa Neema zake na Fadhili, hata sasa tuko hai.
Mungu tupe ufahamu tupate kukujua wewe zaidi, na kisha tupate njia bora ya kukutukuza.

Thanks God in the name of Jesus!
 
Siku zote nakuwa katika maombi lakini naona kama ni vyema tuwe tunakumbushana wana JF na pengine popote pale ,najua tunatingwa na pilika za maisha lakini ni vyema tumkumbuke yeye alietuumba

Ninja ubarikiwe

AmeeeeeeeeeeeN!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom