Ni vyema Afya na Furaha ya maisha viende pamoja

M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
1,126
Points
2,000
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
1,126 2,000
Habari Waungwana!! natumai ni wazima na maisha yanaendelea licha ya changamoto za hapa na pale tunazokumbana nazo katika Jamii....

Kuna muda nafikiria Je tujikite kwenye Kujenga Afya au tuendelee kula maisha na Afya ifuate baadae, Nashindwa cha kufanya ila sasa najiuliza tena nifurahishe nafsi nipate Furaha au Nifuate Afya na mtindo bora wa maisha+?? E bwana enhe nadhani tule maisha huku tukizingatia Afya pia....


Kumekuwa na Changamoto kadhaa na imefika mahali inachanganya mijadala kuhusu afya na jinsi ulaji mbovu unavyosumbua na kuleta magonjwa kadhaa,Kiukweli inashtua kidogo....

Tunaambiwa vyakula vya Wanga ni vibaya katika mwili kwani huchangia kuongeza Sukari na mafuta mabaya katika mwili hali inayoweza kusababisha Ugonjwa wa Kisukari,Moyo na mengine yasiyoambukiza...Kumbuka vyakula vya Wanga ni pamoja na Viazi,Mkate,Wali,Tambi,Vyakula vya nafaka n.k...


Pia Tunaambiwa tusinywe Soda na vitu vya baridi ni hatari kwa afya....Hapa wataalam wanasema unywaji wa Soda huiingiza zaidi ya vijiko kumi na mbili vya Sukari na ikiwa sukari inayohitajika mwilini ni kama kijiko kimoja tu...

Anyway tumekubali hayo yote juu ila bado tunaambiwa ulaji wa Vyakula vya Protini kwa wingi kama Nyama nyekundu mfano Mbuzi,Nguruwe na Ng'ombe ni hatari kwa afya na hupunguza sana umri wa kuishi...

Achilia Mbali kuhusu Monde ama Kilaji ambacho hupingwa na wataalamu kuwa inaleta magonjwa ya Figo, Ini,Kisukari pamoja na Presha.....


Sasa tule na tunywe nini Jamani??Yan kweli tuishi kwa kula Matunda na Mboga aisee! !Tumekuwa Mbuzi mpaka tuishi kwa Matunda na Mboga za majani???

Yan Kilevi nacho tusitumie??Sahau kuhusu Wali ulivyo mtamu vile mnadiriki kutuambia nacho tusile? ?Hvi madaktari mnaujua utamu wa wali Nyama rosti??..Mnasahau vipi kirahisi tunavyofurahia Heinken Baridi ikienda sambamba na Nyama choma? ?Eti Nyama ya kuchoma nayo ni Mbaya kwa Afya???Duh.....

Katika Jamii zetu tunazoishi hizi ni changamoto kubwa sana kufuata mlo kamili cha msingi tujitahidi kupunguza vyakula kadhaa vya Wanga na Mafuta na muda huo tuyafurahie maisha kwa kula na kunywa vile tuvipendavyo ila nidhamu tu iwepo tusiwe na Ulaji na unywaji mbovu uliopitiliza.....

Yote kwa Yote nakubaliana na Suala zima la mazoezi kwa maana kwangu ndiyo njia sahihi ya kuweza kupata Afya njema na angalau kupunguza magonjwa yasiyoambukiza. ..

Tunaweza kufanya jogging,Kutembea kwa haraka kwa umbali mrefu,Kuruka Kamba,Squarts na tukafanikiwa kupunguza sumu na Kalori katika mwili....

Naamini Hakuna zoezi bora la mwili kama Jogging,Kutembea na Kuruka Kamba na wala haihitaji muda mwingi dakika 45 zinatosha kuufanya mwili kuwa sawa na kuendelea na mishe nyingine,Hatuna sababu ya kujitesa kwenda Gym huko na kulipia pesa nyingi...

Faida za Mazoezi haya ....Hulinda Moyo, huchoma mafuta na kurahisisha kupunguza mwili na hivi vitambi vyetu pia hupungua kwa mazoezi haya mepesi tu....

Baada ya yote tukapate baridi na moto aisee maisha yanataka nini bana na mazoezi nishafanya.... Si vibaya kumalizia na Nyama choma lainii ili mradi tuna uthubutu wa kulinda afya zetu pia.

Basi ni kama hivyo naona hamna lingine.
 
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
1,126
Points
2,000
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
1,126 2,000
Hahah muda huo nishakata calories kadhaa...

Si vibaya bia na nyama choma ikichukua nafasi yake..

Tuyaache yote. ...Ushauri wako pia nauhitaji.
Wewe kupungua sahau kabisaaa jamanii...
Unamalizia zoezi na bia na choma
 
Sakayo

Sakayo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Messages
43,675
Points
2,000
Sakayo

Sakayo

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2015
43,675 2,000
Hahah muda huo nishakata calories kadhaa...

Si vibaya bia na nyama choma ikichukua nafasi yake..

Tuyaache yote. ...Ushauri wako pia nauhitaji.
Yaani unakata calories kadhaa unaongeza hapo hapo!

Ukimaliza mazoezi kula matunda mchanganyiko, mboga mboga za kutosha na maji mengi!
 

Forum statistics

Threads 1,303,715
Members 501,078
Posts 31,489,772
Top