Wana Jamvi, tukiacha tofauti zetu za hapa na pale tuzungumze tu kama Watanzania, Maana hatuna nchi nyingine bali ni hii yetu Tanzania.
Picha kama hii inatupa watanzania Kiburi cha kujivunia kuwa tuna kiongozi wetu aliyetuwakilisha si tu kama mwenyekitiu wa EAC lakini kama rais wetu wa JMTZ. katika mkutano huu.
Hii naamini inatupa heshima kuheshimika kama taifa.
Hasa ikizingatiwa kuwa rais wetu Magufuli AKIWA Addis Ababa aliweza kutengamana na viongozi wengine wa nchi mbali mbali za Afrika na hata katibu mkuu wa UN miongoni mwa wengi.
Ninaamini huenda wengine walikuwa na hamu ya kujua huyu Magufuli ni nani na yuko vipi
Na huenda pia walibadilishana mawili matatu kama viongozi wa Kiafrika.
Naamini pia hata anaporudi nyumbani, atakuwa freshi kimawazo na kifikra maana kila mwanadamu huitaji muda wake wa kureflect na kutafakari.
Hasa unapokuwa safarini mbali na majukumu mazito.
Matokeo yake hii mara nyingi huleta nguvu mpya na mawazo mapya.
Itakuwa ni vizuri rais Magufuli AENDELEE KUIUZA Tanzania kila wakati unaporuhusu katika mikutano myenye tija kwa taifa letu. Sisemi KILA MKUTANO bali ile ya MUHIMU kama huu.
Maana hii itazidi kutusaidia kama taifa nasi tutazidi kujikonekiti na wengine na hivyo tutaonekana katika ramani kila wakati.
Ninaamini hata mambo ya Malawi YATAISHA hivi karibuni maana kukutana kwenye mikutano kama hii ana kwa ana huwa kunamaliza migogoro midogo midogo bila kuvutana.
Keep it up Mr President!