Ni vizuri kufahamu maana na asili ya jina lako!

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,841
Ni vizuri kuelewa jina lako au la mtoto na maana yake, kuna mambo mengi hukutokea kwa uzuri au ubaya lakini yawezekana na jina lako linachangia au asili ya jina lako …
Kuna wengi wetu wamepewa majina yao kutoka kwa mababu zao ambao walikua na roho fulani labda ya umasikini, uzinzi, magonjwa n.k. Wengine wamepewa majina kutoka kwa waganga wa kienyeji au mizimu, ndio maana kuna vifungo fulani unavyo kwenye maisha yako.
Jina lako linang’ang’ania ubaki pale pale, hakuna kusonga mbele, wewe ni wa hivyo hivyo au unajimilikisha magonjwa fulani kwasababu bibi au babu zako walikua nayo.
Mfano unasema mimi ugonjwa wangu ni kisukari, TB au sie kwetu ndio ugonjwa wetu! nk
Tukatae misingi mibaya ya majina yetu, tusikubali wala usikubali kumpa mtoto wako majina ya laana
Kwa mfano Shida,Matatizo,Makusudi n.k.
Ni vizuri kukubali au kuwapa watoto majina yenye baraka na kibali katika maisha yetu.
Barikiweni sana!
 
Wewe sasa unachokoza Wanyamwezi kina Funga Meza, Mpini, Jembe Butu na wengineo. 🈸
 
Kuna vitu ukianza kuvitilia sana maanani unafulia tu. Unajiwekea hofu nyiiingi.

Mie jina langu hata sijui maana yake, na sioni uzito.
 
kuna ukweli katika post yako ndugu,hata mimi mwalimu mmoja wa kiimani aliwahi kunipasomo kuhusiana na jambo kama hilo..Kunavitu tunaita maagano nikweli kabisa unakuta jina unalorithi unarithi nakila kitu kutoka kwa huyo mtu,kama ni ulevi,uzinzi na mengine kadha wa kadha ..Lakini solution sio tuu kuyachunguza hayo majina kujua maana au nini,sababu hakuna jina ambalo halijawahi kuitwa na kilajina lina Character zake,sasa basi kikubwa hapa kama nilivo pewa somo nikuwa unapompa mwanao jina,kama nila bibi,mjomba,baba,babu au dada unatakiwa lipite kwenye maombi utayo fanya wewe ya kumuepusha huyo mtoto kurithi yale yote yalio juu au ndani ya jina hilo..Sasa baada yahapo jina lile lile linakuwa jipya kwake bila kurithi yale maagano toka kwa mtangulizi wakwanza wahilo jina katika familia
 
Kwa sie waislam huo unakuwa ni Ushirikina.
Mungu anapewa nafasi yake kwa lolote atakalo litokee kwa mtu na jina halihusiani kabisaa.
Muogopeni Mungu na mumpe mamlaka yake
 
Sijui maana yake na sion umuhimu wake
Am happy kwa jina langu
 
je, ukishagundua jinalako ndo linasababisha matatizo yako unafanyaje na ndo limeishazoeleka

Cha kufanya mkuu nenda kiongozi wako wa dini akavunje hiyo laana ya hilo jina au ikiwezekana unabadili tu
Mimi nina jamaa yangu alikuwa anaitwa makusudi
Alipata sana shida na hilo jina ila kabadilisha ukubwani na sasa tushazoea anaitwa john
 
Ni vizuri kuelewa jina lako au la mtoto na maana yake, kuna mambo mengi hukutokea kwa uzuri au ubaya lakini yawezekana na jina lako linachangia au asili ya jina lako …
Kuna wengi wetu wamepewa majina yao kutoka kwa mababu zao ambao walikua na roho fulani labda ya umasikini, uzinzi, magonjwa n.k. Wengine wamepewa majina kutoka kwa waganga wa kienyeji au mizimu, ndio maana kuna vifungo fulani unavyo kwenye maisha yako.
Jina lako linang’ang’ania ubaki pale pale, hakuna kusonga mbele, wewe ni wa hivyo hivyo au unajimilikisha magonjwa fulani kwasababu bibi au babu zako walikua nayo.
Mfano unasema mimi ugonjwa wangu ni kisukari, TB au sie kwetu ndio ugonjwa wetu! nk
Tukatae misingi mibaya ya majina yetu, tusikubali wala usikubali kumpa mtoto wako majina ya laana
Kwa mfano Shida,Matatizo,Makusudi n.k.
Ni vizuri kukubali au kuwapa watoto majina yenye baraka na kibali katika maisha yetu.
Barikiweni sana!

Text na title ya thread mm.Jitahidi next time.
 
Cha kufanya mkuu nenda kiongozi wako wa dini akavunje hiyo laana ya hilo jina au ikiwezekana unabadili tu
Mimi nina jamaa yangu alikuwa anaitwa makusudi
Alipata sana shida na hilo jina ila kabadilisha ukubwani na sasa tushazoea anaitwa john

Mambo ya kuvunja laana ni ubatili mtupu.
 
Back
Top Bottom