Ni vizuri Harmonize kumuenzi Dkt. Remmy lakini usimsahau na Halila Tongolanga

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,818
Nakumbuka kwenye moja ya tukio niliona ukimuenzi Marehemu Dr Remmy. Hiyo ni sawa kabisa ila pia kwa upande mwingine kuna Marehemu Halila Tongolanga ambaye umerudia moja ya wimbo wake maarufu wa 'kila munu ave na kwao'.

Naamini umeurudia wimbo ule kwa sababu umeukubali pamoja na Mtunzi wake Marehemu Tongolanga.

Kuhusu wimbo huo:- Mimi nadhani hukuutendea haki kabisa...na ni kama umelipua tu au naweza kusema umefanya bora liende. Naamini unge/unaweza kufanya zaidi ya pale.

Ukilinganisha wimbo wako na ule halisi ni vitu viwili tofauti...huu uliofanya wewe ni mwepesi mno ukilinganisha na wimbo halisi, Mtu anaweza akajiuliza sasa uliurudia wa nini au ili iweje?. wimbo wako hauna instruments kabisa.

Chonde chonde nakusihi utengeneze tena huo wimbo na uonyeshe heshima kwa kuutendea haki. Wimbo ule umebeba urithi na utamaduni mkubwa sana ya kusini haswa Mtwara.

Najua upo kwenye nafasi ya kufanya vizuri kwa Video yenye mandhari na audio iliyoshiba sindimba la Kimakonde.....tendea haki SINDIMBA....tulisikie SINDIMBA watu tuserebuke mpaka tuugue.

Dr Remmy 5.png
tongolanga.jpg



 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom