Ni vizuri dada kumuunganisha kakake na rafiki yake.. kaka je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni vizuri dada kumuunganisha kakake na rafiki yake.. kaka je?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 13, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni swali najiuliza kuwa kama dada yako anajaribu kukuunganisha na rafiki yake

  sexy-black-couple-kiss.jpg
  ukimkatalia inaonekana anajua taste zako na kuwa anakutakia mema? Ukimkatalia si uonaonekana humuamini? Inakuwaje sasa kama ukimkubalia halafu uhusiano wako na huyo mtu mwingine ukawa mgumu sana kweli haitaharibu uhusiano wako na dada yako?
  Upande mwingine ni je kaka anaweza kumuunganisha dadake na rafiki yake akiamini kuwa ni pair nzuri? Au ni "no no" kwa kaka kumuunganisha dadamtu? Hili ni muhimu kupata mawazo kwani kiakili "namfahamu" mtu mmoja ambaye anajua kuwa mdogo wake wa kike anaweza akawa na mahusiano mazuri na rafiki ya mtu huyo ambayo yanaweza kufikia hata ndoa. Yaani, jamaa anamuona rafiki yake ni bora awe shemeji yake. Sasa Kitanzania inaruhusiwa.
  Ushauri wa haraka tafadhali.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji......mie hapa sioni tatizo kwa sababu ni katika kukutakia mema but............inatakiwa kuwa makini katika kufanya hivi yaani hao wanaokuunganishia wajitahidi kutoinfluence uamuzi wako....kama ni kukusajestia wasajesti tu na kukuacha uamue mwenyewe kwa sababu siku isipokwenda vizuri hutokuwa na wa kumlaumu wala wao hawatajisikia vibaya sana kwa kuwa uliamua mwenyewe.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hamna tatizo lolote sema sio common kwa kaka kumuunganishia dada yake.Tena baadhi nnaowajua hata rafiki akionyesha kua interested na dada mtu ataambiwa aachane kabisa na hayo mawazo!Ila wadada hua wanapeana moyo!
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  MM aisee hiyo ni ngumu sana kama wapo basi ni wachache sana unajua wengi wao huwa wanakuwa so protective kwa dada zao hasa ukizingatia hatopenda kuoana mwanaume mwenzake anamzengea dada yake huku akiona so automatically dada mwenyewe ndio huwa anakuja kusema mwenyewe hapo baadae kuwa ana mtu.
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haina tatizo ila kwa wakaka inakuaga ni ngumu kumwunganisha dadake kwa rafiki yake. Tena kuna wengine wakigundua unammezea dada mate urafiki unakufa.
   
 6. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Dada wengi wanawaunganishia kaka zao baada ya kaka zao kuonyesha nia. Hii huwa mara nyingi inalipa na imepewa yes. Kwa nini, sijui.

  Kaka kumuunganishia dada, hutokea mara chache, na kaka huwa anahakikisha anaunganisha kwa mtu (rafikiye) makini, na ikifanikiwa huzaa ndoa. Kina kaka wengi hawapendi hii kitu. kwa nini, sijui.
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kweli, kuna wakaka wana uchungu na dada zao. Lol!
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Kaka yangu na rafiki yangu
  Walikutana UNI waka date kwa
  Muda wakaachana sikuwa na shida yeyote ..
  na kaka yangu alimjua rafiki yangu kupitia mimi
  kila tukitoka kwenye sports alikuwa anakuja kwetu..
  Sikuwaonganisha Chemistry zao zilikutana...

  kama kweli wakipendana
  sioni shida..

  Lakini me personal sintakaa ni date marafiki zake..
  Napenda wa mbali lol..
   
 9. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  dada kumwunganishia kaka ni jambo la kawaida
  lakini kwa wakaka sio sana nafikiri ni ile hali ya kaka
  kuona anakuwa kuwadi kwa dada yake na pia inampa hofu
  kama huyo rafiki atakula na kuacha maana inakuwa fedheha
  kwake
   
 10. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Kwa akina dada inawezekana kabisa wakaunganisha marafiki zao kwa kaka zao. Na huwa wanachukua nafasi muhimu sana kushawishi hao marafiki zao wawe mawifi zao. Sasa uhusiano ukianza hayo ni matokeo kama vile ambavyo yangekuwa kama wangekutana wenyewe.
  Kuhusu kina kaka hapo pagumu sana. Siku moja nilimuomba rafiki yangu anisindikize out na wadogo zangu wakike wawili, jamaa akawa beneti sana na mmoja wa wadogo zangu. Nilimpa warning kali kuwa amuache mdogo wangu.

  My take akina dada hushawishi marafiki zao kwa sababu huamini katika mapenzi ya kweli. So wanafikiri hata kaka zao watakuwa hivyo hivyo.
  Kina kaka hujua sababu most of them ni 'hit and run' hujua hata mshikaji atakuwa hit and run kwa dada yake.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mimi sijawahi kumuunganishia dada wala kaka.....

  Wajitafutie wenyewe....

  Na rafiki yangu akianza mahusiano na dada yangu navunja urafiki....

  Tutabaki mashemeji tunaoheshimiana but not best friends
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ndio naweza muunganishia kaka yangu kwa mdada amtakaye ikiwa huyo mdada namkubali (nilishawai kumuunganishia mjomba wangu)
  HAIWEZEKANI KAKA KUMUUNGANISHIA DADA YAKE hii itajaleta dharau acha kabisa.........

  By the way KAKA KAMUUNGANISHIA DADA panachekesha
   
 13. M

  Marytina JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Vipi ikitokea umempenda rafiki ya kaka yake and no way unaweza kuwa naye alone just kwa mazungumzo hata ya dakika tano utatumia ujanja gani bila KAKA kukushtukia?
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,665
  Likes Received: 82,492
  Trophy Points: 280
  Hakuna ubaya wowote lakini kwa maoni yangu inapendeza zaidi Kaka akichacharika kivyake vyake badala ya kutaka kutafuniwa kila kitu na kutengewa mezani.
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Dada anamuunganishia Kaka na Kaka anamuunganishia Dada, eventually Kaka na Dada wanaunganishana - Convergence Of Love!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehehe ntapotezea tu maana hata nikiwa nae mwenyewe siwezi kumtongoza!
   
 17. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  DADA KUM UNGANISHIA KAKA RAFIKI YAKE INAFANYIKA LAKIN MIMI NAKUWA SIPENDI HASA KAMA URAFIKI WAO UTAKUWA WA HIT N RUN.
  BORA KAMA WATAOANA NA NDOA YAO IKADUMU. UZURI WA MAPENZI WAKUTANE HUKOOO ,WATONGOZANE ,WAKUBALIANE WENYEWE HUKOOO PASIPO MIMI KUWA KIUNGANISHI CHAO.

  KAKA KUM UNGANISHIA DADA YAKE HAIPENDEZI , BASI OMBA HAYO MAHUSIANO YADUMU NA YAWE MAZURI lakin YAKIWA MABAYA mm!! naona ni aibu kwa kaka mtu.

  BORA KAKA NA DADA MSIUNGANISHIANE BALI KILA MTU ATAFUTE MPENZI WAKE MWENYEWE KWA MUDA WAKE.
   
 18. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  MM, wadada wengi ambao hupenda kuwaunganishia kaka zao maranyingi ikifikia kaka akachukua jumlajumla, urafiki wahawa akina shosti (wengiwao) haudumu sijui ni kwa nini! akiwa shosti mzuri akiwa wifi tatizo. Mi nadhani ni vizuri ukatafuta kivyako hatakama ni rafiki wa dada yako.. Tatizo ni kwa sisi akina kaka, kumuunganishia dada yako inakuwa ngumu kidogo!
   
 19. CPU

  CPU JF Gold Member

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mi nadhani mambo yako hivi

  Uhusiano wa Kaka na rafiki wa Dada yake
  Kwa hili wadada wapo makini sana kama ukiomba uhusiano na rafiki yake. Kama ni rafiki yake wa muda mrefu basi atakueleza mengi anayofahamu juu ya rafiki yake, hasa ktk suala la tabia. Lakin linapokuja suala la kuridhika kimapenzi, dada ako hawezi kujua nani atakufaa na nani hakufai.

  Uhusiano wa Dada na rafiki wa Kaka yake
  Hapo juu kuna watu wamesema kwamba wakisikia umeanzisha uhusiano na dada ake, urafiki unakufa. Mwingine anasema hawezi kuthubutu kumtafutia dada ake mwanaume. Unajua ni kwanini????
  Ktk suala zima la mapenzi, tumeshajenga dhana kwamba MWANAUME NDIE ANAKULA MAPENZI, NA MWANAMKE ANALIWA MAPENZI na wala sio kila mmoja anakula mapenzi ya mwenzake. Sasa mwanaume gani ataruhusu rafiki yake amle dada ake kwa ruhusa yake??? Na hasa ukizingatia mapenzi ya wanaume wengi ni kuonja-onja tu???

  Hitimisho
  Kuunganishiana marafiki kuingia mahusiano na kaka/dada zetu ni jambo jema kwa vile linalenga kutafutiana watu wazuri kitabia. Lakin ktk kukidhi haja nyinginezo za kimapenzi inawezekana asipatikane mtu sahihi.
   
Loading...