Ni vita ya Dk. Slaa, mtandao wa fedha - Vijana wengi hawajajiandikisha jimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni vita ya Dk. Slaa, mtandao wa fedha - Vijana wengi hawajajiandikisha jimboni

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nngu007, Mar 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]
  Kinyang’anyiro cha Arumeru
  Waandishi Wetu- RaiaMwema
  [​IMG]


  Nassari asafiria ‘nyota’ ya Mbowe, Chama
  Vijana wengi hawajajiandikisha jimboni
  CCM waumana ndani kwa ndani


  WAKATI zikiwa zimesalia siku zisizozidi tano hadi siku ya upigaji kura za kumchagua Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jumapili wiki hii, wagombea wanaoshindana kwa karibu, Joshua Nassari wa CHADEMA na Siyoi Sumari wa CCM, kila mmoja ushindi wake unategemea vigezo tofauti, ikiwamo kiwango cha ushawishi na kukubalika kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vyao kwa wapiga kura, Raia Mwema, imebaini.


  Uchunguzi wa mwandishi wetu anayefuatilia kampeni hizo jimboni humo umebaini kuwa kwa sehemu kubwa, ushawishi wa wagombea hao unaimarishwa zaidi na haiba ya viongozi wao wa kitaifa wanaoshiriki kuwanadi.

  Changamoto na ‘nguvu’ za Joshua Nassari

  Mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari, licha ya uwezo wake binafsi wa kujieleza lakini kwa sehemu kubwa uzito wake jukwaani unahusisha umaarufu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa, ambaye bado hajapoteza mvuto wa kisiasa kwa wakazi wa Arumeru.

  Pamoja na Dk. Slaa, pia Nassari amebebwa kisiasa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Viongozi hao kwa pamoja au kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitawala kwa sehemu kubwa siasa na mwelekeo wa CHADEMA na wakati mwingine, Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, akichukua nafasi ya mmojawapo kwa kadiri ya mazingira mbalimbali ya kisiasa yanayohusisha chama hicho.


  Tafsiri nyingine inayojitokeza ni kwamba, kivuli cha umaarufu wa Dk. Slaa na Mbowe na baadhi ya viongozi wengine wa kitaifa wa CHADEMA, kwa namna fulani pia kinafunika udhaifu wa Nassari na hivyo kuzidi kumjenga kisiasa na kumng’arisha zaidi katika jukwaa la kampeni hizo zenye ushindani mkubwa.


  Lakini mbali na Nassari kunufaika na umaarufu wa viongozi wa kitaifa wa chama chake, matatizo ya wakazi wa Arumeru Mashariki pia ni sehemu ya kete inayochangamsha mwenendo wa kampeni zake.


  Imekuwa rahisi kwa Nassari kujieleza kwa kuegemea matatizo yaliyopo Arumeru na kuahidi kuyatatua. Matatizo hayo ni migogoro ya ardhi, huduma duni ya maji na mfumuko wa bei ambao, hata hivyo, ni tatizo la kitaifa na hata kidunia.


  Lakini kwa kuzingatia mahudhurio na aina ya ushabiki wa kampeni za CHADEMA, ni dhahiri kuwa wapiga kura wengi wa chama hicho ni vijana.


  Ni katika mtazamo huo ambamo changamoto inajitokeza. Alichokibaini mwandishi wetu ni kwamba, vijana wengi wenyeji wa Arumeru Mashariki hawakujiandikisha kupiga kura katika kata za jimbo hilo.


  Wengi wamejiandikisha katika maeneo wanakoendesha shughuli zao za kujikimu kimaisha, ambazo ni Mererani, kwenye mgodi wa Tanzanite, eneo lililopo Jimbo la Simanjiro, linaloongozwa na Christopher ole Sendeka. Mbali na Mererani, vijana wengi wa jimbo hilo wamejiandikisha kupiga Arusha Mjini, wanakoendesha shughuli zao za kila siku.


  Changamoto na ‘nguvu’ za Siyoi Sumari

  Siyoi Sumari, mgombea wa CCM, licha ya kwa kiasi fulani kutegemea makada maarufu wa chama hicho, nguvu zake kisiasa, zinazomsaidia hasa ni mtandao ulioundwa nje ya mfumo wa chama hicho, pengine kama ilivyokuwa mwaka 2005, kwa Jakaya Kikwete alipokuwa akigombea urais, ilipoundwa timu sambamba na timu ya CCM Makao Makuu.

  Hali halisi ni kwamba, mtandao wa pembeni wa Sumari unaoundwa na wafanyabiashara wakubwa na maarufu mkoani Arusha, ndio wenye kumfanya awe na ‘misuli ya kisiasa’ inayomwongezea kasi ya kampeni.


  Hata hivyo, ndani ya dhana hiyo ya mtandao wa pembeni, kunaibuka hali ya kukatishana tamaa ndani ya timu rasmi ya kampeni za CCM jimboni humo. Timu rasmi inaripotiwa kulalamika kwamba wakati mwingine mtandao umekuwa ukiendesha matukio bila taarifa rasmi kwao.


  Kwa sasa inaelezwa kuwa mtandao huo unaendesha mikutano ya ndani na baadhi ya watu mashuhuri jimboni humo na kuwaomba kura kwa ushawishi unaodaiwa na baadhi ya watu ni kugawa fedha. Inaelezwa kuwa, faida ya Siyoi ni kuendesha kampeni zake bila hofu ya kukosa fedha.


  Uchaguzi huo wa Arumeru Mashariki unafanyika Jumapili, ili hatimaye kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Jeremiah Sumari, aliyefariki dunia kwa maradhi.


  Wagombea watakaoshiriki na vyama vyao kwenye mabano ni Joshua Nassari (CHADEMA), Siyoi Sumari (CCM), Shaban Moyo (SAU), Charles Msuya (UPDP), Abraham Chipaka (TLP), Abdalah Mazengo (AFP), Abdalah Mohamed Abdalah (DP) na Khamisi Kihemu (NRA).


  Kwa mujibu wa msimamzi wa uchaguzi huo, Tracius Kagenzi, jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ni 127,000 na vituo vya kupigia kura vilivyosajiliwa ni 327.
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Vyoyote itakavyokuwa, sioni kama CCM watatamba 2015. Wanaweza kuwanunua baadhi ya viongozi tunaowaamini, lakini hawawezi kutununua sisi wote. Jeshi la vijana litakaloandikishwa kwenye daftari la wapigakura kabla ya 2015 ni tishio. Hizi nyimbo za vijana na ajira tumeshagundua zinalenga wapi.
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kwenye swala la vijana kutokujiandikisha kupiga kura ndiko kunakosababisha wakina ZITTO waonekane wasaliti, sababu vijana hawaaminiki, ni kazi sana kuwaunganisha vijana sijui kama CHADEMA wameishafanya utafiti wa kutosha juu ya nguvu ya vijana. mtu asiyepiga kura is as much as dead.

  Itabidi sasa zianze kupigwa kampeni za urithi. Kwamba kwa sababu wazee wetu wamenyonywa sana na CCM na sasa hawana chochote cha kutuachia watoto na vitukuu vyao, basi watupe urithi wa kura zao. watumbukize CHADEMA.

  tutafanyaje sasa
   
Loading...