Ni vita kati ya Dr. Mary Mwanjelwa na Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson, wanagombania jimbo

Vita kubwa kati ya mbunge wa viti maalum na naibu waziri Dr Mary Mwanjelwa na Naibu Spika Tulia Ackson. Dr Mwanjelwa anamshtuma Tulia Ackson kuwa kaanza kampeni za uchaguzi mapema na kuleta mpasuko kwenye jimbo lake.
Dr. Mwanjelwa kawepa bayana kuwa Tulia Ackson anakiuka sheria za chama lakini chama kipo kimya.
Je, chama kinamuogopa Tulia?
Je, kuna mkubwa anaemshika Tulia mkono ndio maana analeta mpasuko uko Mbeya?
Je, Tulia ajiamini ndio maana anaanza kampeni mapema hivi?
Kwanini Ccm inakua na upendeleo wa kuachia wengine wafanye kampeni na wengine wamezuiliwa?View attachment 1107052View attachment 1107053
Tulia ajiamini! au Tulia hajiamini? Kiswahili si lugha yetu tujifunze.
Tulia alianza siku nyingi kampeni na jeshi la polisi halijawahi kumgusa.
 
Very strange. Huyo Mary mwenyewe ni Vitu Maalum. Sio mbunge wa kuchaguliwa.
 
Hiyo barua naona kama ya kutengenezwa, or else aliwaachia wasaidizi wake wamwandikie na yeye hakui-vet, unajua wasaidizi wa viongozi wa CCM asilimia 99% ni darasa la 7
nawewe barua kwani ya ikulu hiyo mpaka iwe perfect? unaambiwa ni ya mbunge, ana katibu pale kaofisini kwake
 
mwanjelwa angekuwa na akili angeamua tu kuwa rafiki wa tulia, kwasababu kuna muda si mrefu tulia atashika mpini yeye atashika makali halafu atahitaji kuomba msaada kwa tulia hatapata kwasababu alimletea mambo ya kitoto before. ukiona huwezi kupigana na giant, fanya urafiki naye ili pengine siku akikaa kwenye kitu akusaidia, la sivyo atakuja kukukanyaka kabisa akikalia kiti.
 
CDM MUMTENGENEZA BARUA NA KUJIJIBU WENYEWE. Kazi hii imefanywa kwa ustadi mkubwa na mfungwa aliyetoka kwa msamaha wa Rais ndugu anayejulikana kwa jina la Mwaifunga. Dkt Tulia anawatia kiwewe
 
Haaaa, CCM tushaanza kung'atana mapema, naona Tulia kapiga mahesabu ya jimbo la Mbeya mjini alilitaka sana, kaona hawezi mtoa Sugu, sasa kaamua kumfukuzia Dr. Mwanjelwa..😂 Siasa hizi kazi kweli wakati wa uchaguzi mnageuka maadui, uchaguzi ukiisha mnajifanya marafiki, unafiki ndio siasa zetu.. 😂
 
Sugu unahanya balaa....ngoja watu wakuonyeshe siasa sio kutunga mistari miwili mitatu kama unaimba Hiphop.....muda ndio mwalim mzurii
 
Back
Top Bottom